Rafiki
Si Mpweke Kamwe
Ubatizo na Uthibitisho


“Si Mpweke Kamwe,” Rafiki, Agosti 2023, 22–23.

Si Mpweke Kamwe

Itakuwaje kama Ethan ataumia tena wakati hakuna mtu hapo kumsaidia?

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Picha
alt text

Ethan alisukuma miguu yake kwenye bembea. Akaenda juu na juu zaidi. Upepo ulimfanya ahisi kama alikuwa anapaa!

Kisha kengele ikagonga. Ethan akasusha pumzi. Hakuwa tayari kwa mapumziko kwisha.

Watoto walisimama kwenye mstari kurudi ndani. Ethan aliruhusu bembea yake itulie. Kisha akashuka kutoka kwenye bembea ili arudi darasani.

Lakini wakati mguu wa Ethan ulipokanyaga chini, alisikia uchungu mkali katika mguu wake. Akaanguka mavumbini. Alijaribu kusimama, lakini alihisi mguu wake kama ulikuwa kwenye moto. Ulikuwa unauma vibaya!

“Nisaidie!” Ethan alipaza sauti. Machozi yalidondoka kwenye mashavu yake. Watoto na walimu walikimbia kumsaidia.

“Nini kimetokea?” mwalimu aliuliza.

“Mguu wangu umevunjika!”

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Ethan kuvunjika mfupa. Wala haikuwa mara ya pili au ya tatu! Ethan ana maradhi ya mifupa miepesi kuvunjika, ugonjwa ambao husababisha mifupa yake kuvunjika kwa urahisi. Hata vitu vidogo, kama vile kuzuia kwa mguu au kugongana na mtu, kungeweza kuvunja mifupa yake.

“Tutawaita wazazi wako wakupeleke kwa daktari,” mwalimu alisema. “Kila kitu kitakuwa SAWA.”

Ethan alifurahi watu walikuwa pale ili kumsaidia. Mguu wake uliuma sana, lakini alijua angekuwa salama.

Mama na Baba yake walienda shuleni na kumpeleka Ethan hadi kwa daktari. Aliwekwa plasta ya samawati kwenye mguu wake na alikwenda nyumbani kupumzika.

Kwa sababu ya mguu uliovunjika, Ethan alitumia muda mwingi kitandani. Alikuwa na vitabu vingi vya kusoma. Wakati mwingine rafiki zake walikuja kucheza naye michezo. Lakini bado alichoka.

Usiku mmoja Ethan aliamka na hakuweze kulala tena. Alijaribu kutulia, lakini aliendelea kuwa na wasiwasi. Itakuwaje kama nikivunjika mfupa na hakuna mtu wa kunisaidia, kama vile usiku wa manane? Ethan aliwaza. Moyo wake ulidunda kwa kasi. Alihisi woga.

“Baba!” Ethan alipiga yowe.

Baba yake alikimbia kwenda chumba cha Ethan. “Kuna tatizo gani?”

“Mie naogopa,” Ethan alisema. “Itakuwaje kama nikivunjika mfupa mwingine na hakuna mtu wa kunisaidia?”

Baba aliketi karibu naye kitandani. “Hilo ni wazo la kutisha,” alisema. “Hata wakati tunapojaribu kuwa makini na salama, mambo mabaya bado hutokea. Bila kujali chochote, Baba wa Mbinguni anakulinda wewe.

“Kwa hivyo hiyo humaanisha Yeye daima atakuwa pamoja nami?” Ethan alisema.

“Kabisa.” Baba alimkumbatia Ethan.

Ethan alifikiria kuhusu jinsi Baba alivyokuja upesi kumsaidia. Alijua Baba anampenda na daima atakuwepo kumsaidia. Labda Baba wa Mbinguni alikuwa hivyo pia.

Siku iliyofuata, Ethan alisoma maandiko katika gazeti la Rafiki. Yalisema, “Kwa hiyo, changamkeni, na msiogope, kwani Mimi Bwana nipo pamoja nanyi, na nitasimama karibu yenu.”*

Ethan alihisi utulivu na salama wakati aliposoma maandiko, kama vile alivyohisi wakati alipozungumza na Baba yake. Alijua alikuwa ni Roho Mtakatifu akimfariji. Ilikuwa kama vile anamkumbatia Baba tena.

Pengine nitavunjika mifupa zaidi, Ethan aliwaza, lakini sihitaji kuogopa. Alijua kamwe hatakuwa peke yake.

Picha
alt text
Picha
alt text here

Vielelezo na Simini Blocker