Rafiki
Shida kwenye Bustani
Ubatizo na Uthibitisho


“Shida kwenye Bustani,” Rafiki, Agosti 2023, 46– 46.

Shida kwenye Bustani

Hunter alivuta pumzi ndefu. “Mimi sisemi maneno hayo.”

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Hunter alikimbia bustanini na rafiki zake. Alicheka alipohisi upepo ukivuma kumpita. Alihisi kuwa kasi sana na mwepesi!

Kyle aligusa ua kwanza. “Nimeshinda!” alipaza sauti.

Hunter alifika kwenye ua muda mchache baadaye. “Hii sio haki! Ulianza kwanza.”

“Ndiyo,” Miguel alisema. “Tukimbie hadi kwenye mti!”

Hunter alianza kukimbia tena. Wakati huu, aligusa mti kwanza. Lakini Miguel alikuwa nyuma yake.

“Nimeshinda!” Miguel alisema.

“Hapana, Hunter ameshinda,” Piper alisema.

“Ndiyo,” Kylel alisema.

Miguel alikunja mikono. Kisha akasema neno baya.

Watoto wengine walicheka. Miguel akasema lile neno tena, na walicheka hata zaidi.

Hunter alihisi huzuni ndani. Yeye alijua hilo neno halikuwa zuri kusema. Lakini hakutaka kutaniwa. Hakusema chochote.

Piper akasema neno lingine baya. Kisha Kyle akasema lingine.

“Sasa sema neno moja, Hunter,” Kyle alisema.

“Ndiyo, sema,” Miguel alisema. “Sema neno jipya la kuapa.”

Hunter alivuta pumzi ndefu. “Mimi sisemi maneno hayo.”

“Sema neno haitakudhuru,” Kyle alisema.

“Sitaki kufanya hivyo,”alisema Hunter.

“Unaogopa sana?” Miguel alicheka.

Uso wa Hunter ulihisi moto. “Mimi nitaenda kucheza mahali pengine.”

Watoto wengine waliendelea kucheka na kusema maneno mabaya. Hunter alitaka kuondoka. Bustani haikuhisi kuwa burudani sasa. “Tutaonana baadae,” alisema.

Picha
alt text

Hunter aliweka mikono yake katika mifuko yake na polepole akaondoka akiwaacha watoto wenzake. Hakuhisi kuwa kasi au mwepese tena. Alihisi uzito mkubwa.

Alimkuta Mama na Baba wameketi kwenye benchi. Baba aliweka chini kitabu chake. “Je, uko SAWA?”

Hunter akapandisha mabega. “Walianza kusema maneno mabaya. Sikutaka kufanya hivyo, kwa hiyo nikaondoka.”

Mama alitabasamu. “Huo ulikuwa ujasiri.”

“Umefanya vizuri,” Baba alisema. “Ni vigumu kufanya chaguzi nzuri wakati watu wanaotuzunguka hawafanyi hivyo.”

Hunter alishusha pumzi. Alifurahia alifanya chaguo sahihi, lakini yeye bado hakuhisi vizuri.

“Je, unataka kwenda nyumbani?” Mama aliuliza.

Hunter alifikiria. “Bado,” alisema. Aliwatazama kundi lingine la watoto likicheza kuruka kamba. “Mimi nitaenda kule.”

Hunter alipokuwa anaenda huko, mmoja wa wavulana alimpungia mkono. “Halo, mimi ni David.”

“Mimi ni Hunter. “Ninaweza kuruka na wewe?

“Hakika!”

Hunter akachukua zamu kwenye kamba na kuhisi upepo ukivuma. Alipokuwa akicheza na David na wengine, alihisi kuwa kasi na mwepesi tena. Alikuwa amefanya kile kilichokuwa sahihi, hata ingawa ilikuwa vigumu. Alifurahi kuwa alifanya chaguo zuri.

Picha
alt text
Picha
alt text here

Vielelezo na Shawna J. C. Tenney