Rafiki
Njooni kwenye Ubatizo Wangu!
Ubatizo na Uthibitisho


“Njooni kwenye Ubatizo Wangu!” Rafiki, Agosti 2023, 14.

Njooni kwenye Ubatizo Wangu!

Picha
alt text here

Kazi ya sanaa na Ana Oldroyd

Tengeneza kadi maridadi za kuwaalika watu kwenye ubatizo wako! Ni nani unataka kumwalika? Tunaweza kuomba na kumsikiliza Roho Mtakatifu kwa ajili ya baadhi ya mawazo.

  1. Kunja kila karatasi nusu mbili zinazolingana. Upande wa mbele au ndani ya kadi, andika ujumbe wa kuwaalika watu kwenye ubatizo wako.

  2. Ongeza tarehe, muda, na anwani kwa ajili ubatizo wako.

  3. Chovya kidole chako katika rangi ili kuongeza mapambo! Tazama mawazo kwenye ukurasa huu.

  4. Toa kadi kwa rafiki zako na familia yako!

Nilitaka kushiriki ubatizo wangu na watu ninaowapenda. Kwa hiyo kwa msaada wa mama yangu, dada yangu pamoja na mimi tuliwaalika rafiki zangu na watu wa darasa langu kwenye ubatizo wangu. Siku ya ubatizo wangu, kila kitu kilienda vyema. Kulikuwa na watu wengi pale. Nilihisi furaha sana nilipobatizwa!

Eve O., umri miaka 8, Fort-de-France, Martinique