Rafiki
Kumfuata Yesu kwa Pamoja
Ubatizo na Uthibitisho


“Kumfuata Yesu kwa Pamoja,” Rafiki, Machi. 2023, 49.

Kumfuata Yesu kwa Pamoja

Picha
alt text

Nilichagua kutembea kwenye njia mpya na kumfuata Yesu Kristo nilipobatizwa. Ubatizo wangu ulikuwa rahisi lakini wenye hisia nyingi, na nilihisi kuwa mpya. Ninataka kutumikia misheni.

Happiness D., umri miaka 9, Accra, Ghana

Picha
alt text

Ninajaribu kumfuata Yesu tangu nibatizwe kwa kuwa mkarimu kwa mdogo wangu. Ninasaidia kwa kusukuma gari lake. Ninajisikia furaha ninapokuwa mkarimu, ninajua hilo humfanya Yesu kuwa na furaha pia.

Simon P., umri miaka 9, Massachusetts, Marekani

Picha
alt text

Ninamfuata Yesu kwa kusali, kuwapenda wengine, na kuwa na imani.

Yoreli T., umri miaka 6, Zumpango, Mexico

Picha
alt text

Siku ya Krismasi mimi na baba yangu tuliwapelekea chakula watu wasio na makazi. Ilikuwa ya kuburudisha sana! Kumfuata Yesu Kristo hunifanya nijisikie furaha.

Akari F., umri miaka 9, Chiba, Japani

Picha
alt text

Ninamfuata Yesu kwa kusoma maandiko yangu na kufuata amri Zake.

Luke W., umri miaka 9, Wyoming, Marekani

Picha
alt text

Ninamfuata Yesu kwa kuipenda familia yangu na kuwa msaidizi mdogo wa mama yangu.

Chloe, umri miaka 4, National Capital Region, Ufilipino

Picha
alt text

Ninaposali, kusoma maandiko au kufanya kitu kizuri, ninajisikia furaha. Ni kama hisia ya kumbatio la mtu ninayempenda. Ninajua ni Roho Mtakatifu.

Caileen D., umri miaka 6, National Capital Region, Ufilipino

Picha
alt text

Ninamhisi Roho Mtakatifu wakati ninapopitia nyakati ngumu. Ananisaidia nijisikie vyema.

Hunter O., umri miaka 11, Carolina ya Kaskazini, Marekani

Picha
alt text

Ninamhisi Roho Mtakatifu wakati ninapoituliza akili yangu na kuchagua kile kilicho sahihi. Ninapowasikiliza mama na baba yangu, ninaweza kumhisi Roho Mtakatifu karibu.

Oliver B., umri miaka 10, Washington, Marekani

Picha
alt text

Roho Mtakatifu huleta hisia za ukunjufu na kuimarisha. Roho Mtakatifu yupo kwa ajili yako wakati unapomhitaji, kitu ambacho hufanya iwe maalumu.

Aisea A., umri miaka 9, Central Division, Fiji

Picha
alt text

Roho Mtakatifu hunifanya nihisi furaha, vizuri, na mwenye nguvu.

Hailey G., umri miaka 7, Santa Cruz, Bolivia

Picha
alt text

Wakati nilipobatizwa, nilihisi baridi kwa sababu ya maji. Kisha ubatizo ulipomalizika, nilihisi joto na msafi. Kwa kubatizwa nilipiga hatua kubwa sana kusonga karibu na Kristo na Baba yetu wa mbinguni.

Malayla S., umri miaka 8, Yukon, Canada