Rafiki
Isaya ni nani?
Machi 2024


“Isaya ni nani?” Rafiki, Machi 2024, 24–25.

Jifunze kuhusu Kitabu cha Mormoni

Isaya ni nani?

Kwenye Kitabu cha Mormoni, tunasoma maneno ya mtu aliyeitwa Isaya. Isaya alikuwa nabii wa Agano la Kale. Aliishi zamani kabla Yesu Kristo hajazaliwa.

Picha
alt text

Isaya alifundisha kuhusu maisha ya Yesu Kristo. Alisema kwamba Yesu angeleta amani katika ulimwengu. Alifundisha kwamba Yesu angekufa, na kufufuka na kurudi tena duniani siku moja.

Picha
alt text

Mamia ya miaka baadaye, Nefi aliandika maneno ya Isaya katika Kitabu cha Mormoni ili kutufundisha kuhusu Yesu Kristo. Wakati Yesu alipowatembelea Wanefi, Yeye alishiriki maneno ya Isaya. Yeye alituomba tujifunze maneno haya. Tunapojifunza maneno ya Isaya, tunaweza tukauhisi upendo wa Mwokozi na kuja karibu Naye.

Changamoto ya Maandiko

  • Soma 2 Nefi 19:6. Kuna majina mangapi ya Yesu katika mstari huu?

  • Ni kiumbe gani kilitokea ili kuonyesha kwamba Roho Mtakatifu alikuwa katika ubatizo wa Mwokozi? Dokezo: 2 Nefi 31:8

  • Ni nani atafufuliwa? Dokezo: Alma 11:44

Ninaweza Kusoma Kitabu cha Mormoni!

Baada ya kusoma, paka rangi sehemu ya picha. Unaweza kusoma maandiko haya yanayoenda sambamba na usomaji wa kila wiki kutoka Njoo, Unifuate.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Ben Simonsen