Rafiki
Kumfuata Yesu Pamoja
Machi 2024


“Kumfuata Yesu Pamoja,” Rafiki, Machi 2024, 20–21.

Kumfuata Yesu Pamoja

Picha
alt text

Watoto wa Msingi katika Shefa, Vanuatu, wanajifunza kuhusu historia ya familia yao. Walitengeneza mabango ya miti ya familia zao na kushiriki kile walichojifunza katika shughuli ya Msingi.

Picha
alt text

“Bustani ya Gethsemane,” Mitchell H., umri miaka 10, Arizona, Marekani

Picha
alt text

“Yeye Hayupo Hapa, Amefufuka,” Rachel O., umri miaka 7, Arkansas, Marekani

Picha
alt text

Clara na Brighton S., umri miaka 5 na 7, Bavaria, Ujerumani

Picha
alt text

Adelyn B., umri miaka 12, Texas, Marekani

Picha
alt text

Tunapenda kupaka rangi mayai na kufanya mawindo ya yai la Pasaka. Daima kuna yai moja la plastiki ambalo ni tupu. Linatukumbusha juu ya kaburi tupu baada ya Yesu kufufuka!

Eli W., umri miaka 6, California, Marekani

Picha
alt text

Katika asubuhi ya Pasaka, tunaenda kanisani na kurudi nyumbani ili kujifunza zaidi kuhusu Mwokozi wetu. Tuna mayai 12 ya Pasaka ambayo yanawakilisha vitu alivyovifanya. Yai la mwisho daima linakuwa tupu kwa sababu linawakilisha kwamba Yesu alifufuka!

Scarlet A., miaka 10, New Mexico, Marekani

Picha
alt text

Mimi najua Baba wa Mbinguni anatupenda na alimtoa Mwanawe ili kutuokoa sisi. Ninapenda kwenda kanisani na familia yangu na kukutana na rafiki zangu katika Msingi. Ninawapenda walimu wangu wa Msingi kwa sababu wanaimba pamoja nasi darasani.

Melanie C., umri miaka 6, Blantyre, Malawi

Picha
alt text

Nimekuwa nikipiga kinanda tangu nikiwa na miaka mitano, na ninafanya mazoezi sana. Ninahisi furaha ninapopiga kinanda. Ninapenda kuwapigia kinanda rafiki zangu katika ubatizo wao.

Julián G., umri miaka 7, Maule, Chile

Picha
alt text

Nilijifunza Makala ya Imani ili kujiandaa kwa ajili ya ubatizo wangu. Wazazi wangu walinisaidia nijifunze kuhusu maagano ambayo ningefanya wakati wa ubatizo wangu.

Logan M., umri miaka 9, Coahuila, Mexico

Picha
alt text

Familia yangu inahama sana. Nimejifunza jinsi ya kupata marafiki wapya katika sehemu mpya. Ninawauliza watu kama ninaweza kukaa karibu yao wakati wa mlo wa mchana. Ninapata marafiki ninapouliza maswali na kuzungumza na wengine.

Annie W., umri miaka 11, Capital Governorate, Bahrain