Rafiki
Mbio za Tunda
Machi 2024


“Mbio za Tunda,” Rafiki, Machi 2024, 33.

Kitu cha kuburudisha

Mbio za Tunda

Picha
alt text

Huu ni mchezo unaoweza kuucheza na marafiki pamoja na familia!

  1. Weka alama kwenye mstari wa kuanzia na kumalizia. Chagua mtu mmoja awe mkimbizaji.

  2. Kila mtu anasimama kwenye mstari wa kuanzia na kwa siri anachagua tunda. Mkimbizaji anasimama nyuma ya mstari wa kuanzia mgongo wake ukiwaelekea wachezaji wengine.

  3. Mkimbizaji anasema jina la tunda.

  4. Wachezaji ambao walichagua tunda hilo wanakimbia hadi kwenye mstari wa kumalizia. Mkimbizaji anageuka na kujaribu kuwagusa.

  5. Yeyote anayeguswa atakuwa mkimbizaji anayefuata.

Utayarishaji wa Mlo

Katika Neno la Hekima, Yesu alituambia vyakula ambavyo vingekuwa vizuri kwa ajili ya kula. Soma Mafundisho na Maagano 89:10–12, 14. Kisha chora baadhi ya milo yako pendwa kwenye sahani zilizopo hapa chini!