Rafiki
Yesu Kristo yu Hai
Machi 2024


“Yesu Kristo yu Hai,” Rafiki, March 2024, 2–3.

Kutoka Urais wa Kwanza

Yesu Kristo yu Hai

Ilitoholewa kutoka kwa “Roho Wake awe Nanyi,” Liahona, Mei 2018, 86–89 na “He Is Risen,” Liahona, Aprili 2013, 4–5.

Picha
alt text

Kipindi hiki cha mwaka hutusaidia tukumbuke dhabihu ya Mwokozi na ufufuko Wake kutoka kaburini.

Niliwahi kusimama na mke wangu nje ya kaburi huko Yerusalemu. Ndani, tuliona benchi la jiwe kwenye ukuta.

Lakini taswira nyingine ikaja akilini mwangu. Nikamfikiria Mariamu hapo kwenye kaburi tupu. Alikuwa akilia kwa sababu Mwokozi alikuwa amekufa. Hakujua pale ulipokuwa mwili Wake.

Kisha “akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu” (Yohana 20:14). Mariamu alidhani Yeye alikuwa mtunza bustani.

“Yesu akamwambia, Mariamu” (Yohana 20:16). Sasa Mariamu akamjua Yeye. Alijua Yeye Alikuwa amefufuka.

Kwa sababu Yesu Kristo alishinda kifo, watoto wote wa Baba wa Mbinguni wanaozaliwa duniani watafufuka katika mwili ambao kamwe hautakufa.

Ninamshukuru Baba yetu wa Mbinguni kwa ajili ya Zawadi ya Mwanawe Mpendwa. Nina shukrani kujua kwamba Yeye alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka katika ufufuko. Nashuhudia kuwa Yesu ni Kristo aliyefufuka, Mwokozi wetu na mfano wetu kamili.

Hadithi ya Gurudumu la Pasaka

Kata miduara na uweke duara la kwanza juu ya jingine. Toboa shimo katikati na uzishikamanishe kwa pini au msumari bapa wa chuma. Kisha geuza mzunguko wa juu ili kusimulia hadithi ya Pasaka.

Hadithi ya Pasaka

  1. Yesu aliingia Yerusalemu katika Jumapili ya Matawi (ona Marko 11:7–11).

  2. Yesu aliwapa wanafunzi Wake sakramenti (ona Mathayo 26:26–28).

  3. Yesu alisali katika Bustani ya Gethsemane (ona Marko 14:32–36).

  4. Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu (ona Luka 23:46).

  5. Mwili Wake ulikaa kwenye kaburi kwa siku tatu (ona Mathayo 27:59–64).

  6. Yesu alikuwa hai tena. Na Yeye yu hai leo! (Ona Mathayo 28:6–9.)

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Alyssa Tallent