Rafiki
Pasaka ya Kukumbukwa
Machi 2024


“Pasaka ya Kukumbukwa,” Rafiki, Machi 2024, 14–15.

Pasaka ya Kukumbukwa

Jonas alihisi upendo wa Yesu wakati alipoimba.

Hadithi hii ilitokea huko Finland.

Jonas alicheka alipowakimbilia kaka zake sebuleni kwa ajili ya jioni ya nyumbani. Bado angehisi harafu tamu ya kondoo wa kuchomwa kutoka kwenye mlo wa jioni wa Pasaka. Na bado angelionja pasha tamu, kitindamlo cha utamaduni wa Pasaka.

Baada ya familia kuketi kimya, kaka mkubwa wa Jonas aitwaye Tristan alisimama.

“Pasaka Njema!” Tristan alisema. Alianzisha jioni yao ya nyumbani kwa wimbo na sala. Kisha ulikuwa muda kwa programu maalumu ya muziki. Kila mmoja alikuwa ameandaa wimbo wa kushiriki kuhusu Yesu Kristo.

Tristan alipiga gitaa, akipiga kila waya kwa makini. Kisha kaka yake mkubwa aitwaye Einar alipiga kinanda. Vidole vyake vilitembea kuvuka vibao. Mama, Baba na kaka wengine wa Jonas pia walipiga nyimbo. Jonas alipenda kusikiliza muziki wa familia yake.

Hatimaye ikafika zamu ya Jonas. Alivuta pumzi ndefu na kuanza kuimba

Picha
alt text

“Wakati mwingine ninajaribiwa kufanya chaguzi mbaya, lakini ninajaribu kusikiliza ile sauti ndogo ikinong’oneza, ‘Mpendane kama Yesu anavyowapenda.’”*

Jonas alipokuwa anaimba, moyo wake ulijawa na upendo. Macho yake yalijawa machozi ya furaha. Ilikuwa ni kama Roho Mtakatifu alikuwa anamwambia Jonas kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu walimpenda.

“Asanteni nyote kwa kushiriki talanta zenu,” Baba alisema. Aliinua juu picha. Ilimuonesha Yesu Kristo amepiga magoti na akisali karibu na mti. “Ni nani anajua kinachotendeka katika picha hii?”

Jonas aliinua mkono wake. “Huyo ni Yesu akisali Gethsemane.”

Baba aliitikia kwa kichwa. “Ndiyo. Hapo ndipo Yeye alipohisi uchungu na huzuni yetu yote.”

“Yeye alienda kwenye Bustani ya Gethsemane kabla ya kufa,” Mama alisema. “Baada ya Yeye kufa, Yeye aliishi tena. Hii yote ni sehemu ya Upatanisho Wake. Yesu alifanya haya yote kwa sababu Yeye anatupenda.”

Mama alifungua video kuhusu Pasaka ya kwanza. Video ilipoisha, kila mmoja alikuwa kimya kwa muda. Jonas alihisi tena upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

“Na sasa si ni wakati wa shughuli yetu?” Jonas aliuliza.

Mama alisimama kutoka kwenye kochi na kwenda kwenye kabati. “Ndiyo! “Jonas, utanisaidia?”

Jonas na Mama walitoa gundi, mkasi na rundo la magazeti ya Kanisa. Wakayatandaza kwenye sakafu. Kisha Mama akampa kila mmoja shajara yao maalumu ya Pasaka. “Acha tutengeneze sanaa ya picha ya Yesu Kristo katika shajara zetu za Pasaka.

Picha
alt text

Jonas aliketi chini sakafuni na kufungua daftari lake.

Baba akatwaa kalamu ili kuandika katika shajara yake. “Karibu na picha zako, unaweza kuandika kile utakachofanya ili kumfuata Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ili kuwa zaidi kama Wao.

Jonas alifungua kurasa za mojawapo ya magazeti. Akapata picha ya Yesu Kristo akitabasamu.

Jonas alikata picha ile na kuigundisha katikati ya ukurasa wa shajara yake. Alifikiria kuhusu upendo wote ambao alikuwa ameuhisi kutoka kwa Mwokozi siku ile. Kisha aliandika, “Mimi nitamfuata Baba wa Mbinguni na Yesu kwa kumsikiliza Baba na Mama na kusaidia kazi za nyumbani. Nitawapenda kaka zangu zaidi.” Aliinua juu ili kumuonesha Mama. Mama alisoma kile ambacho Jonas alikuwa ameandika na kutabasamu.

Jonas angeweza kukumbuka Pasaka hii kwa muda mrefu. Alihisi upendo wa Yesu Kristo wakati alipoimba na kujifunza kumhusu Yeye. Na alihisi upendo wa Yesu wakati alijaribu kuwa kama Yeye.

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kweli walimpenda Jonas. Na Jonas aliwapenda Wao pia.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Steliyana Doneva

  • “I’m Trying to Be Like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78).