Rafiki
Mazungumzo na Will kuhusu Kuwasaidia Wakimbizi
Machi 2024


“Mazungumzo na Will kuhusu Kuwasaidia Wakimbizi,” Rafiki, Jan. 2024, 40–41.

Mazungumzo na Will kuhusu Kuwasaidia Wakimbizi

Will anatokea Pennsylvania, Marekani. Tulimuuliza maswali kadhaa kuhusu mradi alioufanya ili kuwasaidia wengine.

Tuambie kuhusu wewe mwenyewe.

Picha
alt text
Picha
alt text

Nina umri wa miaka 11. Ninapenda kucheza soka na lacrosse, kuoka biskuti, kuogelea, kuteleza kwenye barafu, na kutembea kwa viatu telezi. Mimi pia ninapenda kupiga kinanda na fidla. Rangi yangu pendwa ni samawati iliyokolea, na chakula changu pendwa ni mayai (yaliyokaangwa, ya kuchemsha—ninayapenda yote!). Nitakapokua mkubwa, natumaini kuwa daktari kama baba yangu.

Ni nini kilichokupa wazo la kusaidia?

Nilisikia kwamba familia nyingi kutoka nchi nyingine walikuwa wanatoroka kwa ajili ya usalama wao. Baadhi yao walikuwa wakihamia eneo la karibu. Wakati huo huo nikawaza, “Ninawezaje kuwasaidia?

Nilisali ili kujua jinsi ambavyo ningeweza kusaidia. Kisha mama yangu akapata barua pepe kutoka kwa Muungano wa usaidizi wa kigingi. Walikuwa wanawaomba watu kuchangia vitu vya kuwapa familia za wakimbizi. Nilijua sala yangu imejibiwa!

Ulisaidia vipi?

Picha
alt text

Ninapenda kuoka (uhodari wangu ni katika biskuti) kwa hiyo niliamua kuuza biskuti ili kupata fedha kwa ajili ya familia hizi. Nilitengeneza vipeperushi na kuendesha viatu vyangu telezi katika ujirani ili kuzipeleka. Mbwa wangu Coco, pia alienda nami.

Wengi wa jirani zangu walikuwa na shauku ya kununua biskuti zangu. Kwa fedha nilizopata, nilinunua vyungu na masufuria ya kuchangia.

Je, ulihisi vipi?

Picha
alt text
Picha
alt text

Nilihisi vizuri kujua familia hizi zingeweza kupika zikitumia vyungu na masufuria. Ninaweza tu kufikiria jinsi inavyofariji kupata ladha ya mlo uliopikwa nyumbani katika nchi ya ugeni.

Nilijifunza katika Msingi kwamba “mnapotumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu” (Mosia 2:17). Nilihisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yangu na kwa ajili ya watu waliohamia katika eneo letu.

Ni ushauri upi ungempa mtu ambaye anataka kusaidia?

Picha
alt text

Tafuta njia za kutumikia katika kata yako au kigingi. Ungeweza pia kusaidia wenye mahitaji katika eneo lako. Kuna njia ya kusaidia kila mahali!

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Dave Williams