Rafiki
Kuku na Vifaranga
Machi 2024


“Kuku na Vifaranga,” Rafiki, Machi 2024, 4–5.

Kuku na Vifaranga

“Yesu Kristo aliongelea kuhusu hili kwenye maandiko,” Baba alisema.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Picha
alt text

Vifaranga vitano vilivyojaa manyoya vilikuwa vikimtazama Clara. Pip, pip, pip!

Kila majira ya kuchipua familia ya Clara ilinunua vifaranga vya kufuga. Leo Clara amemsaidia Baba kuvipeleka nyumbani kuungana na kuku wengine.

Njia waliyokuwa wakipita kwa gari ilikuwa ya mabonde. Lakini Clara alishikilia boksi la vifaranga kwa uthabiti katika paja lake. Tararatibu alikipapasa kimoja kwa ncha ya kidole chake. kilikuwa laini sana!

Wakati Clara na Baba walipowasili nyumbani, walielekea kwenye banda la kuku nyuma ya nyumba. Banda la kuku lilikuwa na kivuli sehemu ndogo ambapo kuku wote waliishi na kutengeneza viota vyao.

“Kuku yupi tumpatie vifaranga hawa?” Baba aliuliza.

Clara aliangalia huku na huko. Kuku mmoja alikuwa akivuta nyasi kutengeneza kiota. Nyasi hizo zingetengeneza kiota kizuri kwa ajili ya vifaranga wapya. Pengine angekuwa mama mzuri.

“huyu hapa,” Clara alisema, akimnyoshea kidole yule kuku.

Baba taratibu alinyanyua kifaranga kutoka kwenye boksi na kukiweka karibu na yule kuku. Kuku yule alimwangalia yule kifaranga. Kuku yule alinyanyua bawa lake na ghafla kifaranga kikapotea!

“Kimeenda wapi? Je, kifaranga kiko salama?” Clara aliuliza

Baba aliitikia kwa kichwa. “Tazama.”

Kifaranga kilichomoza kichwa chake nje kutokea chini ya manyoya ya yule kuku.

“Kwa nini kuku alifanya hivyo?” Clara aliuliza.

“Ili kukilinda kifaranga,” Baba alisema. “Kuku huyo atakiweka kifaranga salama na chenye joto chini ya mbawa zake.”

Clara alimsaidia baba kuviweka vifaranga vingine kwa mama yao mpya. Yuke kuku alinyanyua mbawa zake kuvikusanya vifaranga vyote karibu yake.

“Unajua, Yesu Kristo alizungumza kuhusu hili katika maandiko,” Baba alisema.

“Kweli?” Clara aliuliza “Alisema nini?”

“Nitakuonyesha.”

Clara na Baba waliingia ndani. Baba alitoa maandiko yake. Kisha alianza kusoma.

“Ni mara ngapi nitawakusanya kama vile kuku hukusanya vifaranga wake chini ya mabawa yake, ikiwa mtatubu na kunirudia kwa lengo moja la moyo.”*

Clara alimfikiria kila kifaranga chini ya manyoya ya kuku. “Kwa hiyo Yesu hutukusanya sisi kama kuku anavyowaweka vifaranga chini ya mbawa zake?” Clara aliuliza.

“Uko sahihi,” Baba alisema. “Hutuweka salama, kama vile kuku anavyowaweka salama vifaranga vyake. Lakini Yesu hutulinda kwa vingi vingine zaidi ya baridi. Yeye anajua pale tunapoumizwa au tunapoumwa au wenye huzuni. Yeye hutupatia amani na faraja. Yeye anatujali.”

Asubuhi iliyofuata, Clara aliwalisha kuku na vifaranga wake wapya. Hilo lilimfanya afikirie kuhusu andiko ambalo Baba alilisoma. Alitabasamu alipokuwa akiwaza kuhusu Yesu. Clara alijua Yesu alimpenda na kumjali, kama vile kuku alivyowajali vifaranga.

Picha
PDF ya hadithi

Kielelezo na Assia Ieradi