Rafiki
Kumfuata Yesu huko Papua New Guinea
Machi 2024


“Kumfuta Yesu huko Papua New Guinea,” Rafiki, Machi 2024, 6–7.

Kumfuata Yesu huko Papua New Guinea

Kuhusu Erwin

Picha
alt text

Umri Miaka: 7

Kutoka: Mkoa wa Kati, Papua New Guinea

Lugha: Kingereza na Kitok Pisini

Malengo: 1) Kuwa rubani 2) Kuwa mmisionari.

Anavyovipenda: Kucheza dansi na kuvua samaki

Familia: Mama, Baba, kaka wakubwa watatu na dada mmoja mkubwa

Jinsi Erwin Anavyomfuata Yesu

Picha
alt text

Erwin anamfuata Yesu kwa kuwasaidia wazee katika mji wake. Anasaidia kusafisha ua wao na kuwapelekea chakula. “Nina furaha ninapowasaidia wao. Nataka kusaidia zaidi,” anasema.

Erwin pia humfuata Yesu kwa kusali kwa Baba wa Mbinguni. “Ninaposali, ninahisi kama vile Mungu yupo nami,” anasema.

Erwin alisali kumwomba Baba wa Mbinguni kuisaidia familia yake kuwa pamoja milele. Erwin na familia yake walienda hekaluni huko Tonga kuunganishwa kama familia. Anasema, “Nilimhisi Roho ndani ya hekalu. Kulikuwa na amani sana na ukimya.”

Mambo Ayapendayo Erwin

Hadithi ya Kitabu cha Mormoni: Wakati nefi alipojenga mashua (ona Nefi 17–18.)

Desturi ya Familia: Kukusanyika kwa familia yote katika kijiji ili kula pamoja

Tunda: matufaha

Rangi: Nyekundu

Wimbo wa Msingi: “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2)

Picha
alt text

Erwin na familia yake wakiwa kwenye Hekalu la Nuku’alofa Tonga.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Mina Price