Rafiki
Yakobo na Nefi Walimwona Yesu
Machi 2024


“Yakobo na Nefi Walimwona Yesu,” Rafiki, Machi 2024, 26–27.

Hadithi za Maandiko

Yakobo na Nefi Walimwona Yesu

Picha
alt text

Vielelezo na Andrew Bosley

Picha
alt text

Yakobo alikuwa kaka mdogo wa Nefi. Alizaliwa baada ya familia yake kuondoka Yerusalemu. Yakobo alifika kwenye nchi ya ahadi kama mtoto.

Picha
alt text
Picha
alt text

Yakobo na Nefi wote walimwona Yesu. Walishiriki shuhuda zao na familia zao ili kuwasaidia wao kujifunza kuhusu Yesu.

Picha
alt text
Picha
alt text

Pia walishiriki maneno ya nabii Isaya. Isaya alikuwa pia amemwona Yesu na kuandika kumhusu Yeye katika maandiko. Yakobo na Nefi walitumia maneno ya Isaya kutoka kwenye maandiko ili kuzifundisha familia zao kuhusu Yesu.

Picha
alt text

Walifundisha kwamba Yesu angekuja duniani. Angekufa na kuishi tena. Walishiriki ushuhuda wao wa Yesu Kristo ili kwamba familia zao zingetazamia kuja Kwake.