Rafiki
Yungiyungi za Kutengeneza za Pasaka
Machi 2024


“Yungiyungi za Kutengeneza za Pasaka,” Rafiki, Machi 2024, 15.

Kitu cha kuburudisha

Yungiyungi za Kutengeneza za Pasaka

Yungiyungi za Pasaka zinaweza kutusaidia tukumbuke Ufufuko wa Yesu Kristo. Tunguu za yungiyungi zinakua chini mchangani kwa muda mrefu kabla ya kuchanua katika majira ya kuchipua. Baada ya Yesu kufa, mwili Wake uliwekwa katika kaburi. Lakini baada ya siku tatu, Yeye aliishi tena!

Tengeneza yungiyungi zako mwenyewe za Pasaka kwa kufuata hatua hizi.

  1. Chora mkono wako kwenye kipande cha karatasi na kikate.

  2. Kikunje katika umbo la pia na tumia gundi kugundisha. Acha tundu dogo kwa chini.

  3. Kunja kila kidole kuzunguka penseli.

  4. Weka kijiti ndani ya tundu katika ua lako kutengeneza shina. Gundisha ua kwenye kijiti. Hiari: Paka rangi sehemu ya juu ya kijiti kwa rangi ya njano na sehemu ya chini kwa rangi ya kijani. Ongeza majani ya karatasi.

Picha
PDF ya hadithi

Kazi ya sanaa na Anna Oldroyd