Rafiki
Salamu kutoka Papua New Guinea!
Machi 2024


Salamu kutoka Papua New Guinea! Rafiki, Machi 2024, 8–9.

Salamu kutoka Papua New Guinea!

Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.

Papua New Guinea ni nchi ya kisiwa katika Bahari ya Pasifiki. Inachukua nusu ya kisiwa cha New Guinea. Zaidi ya watu milioni 8 wanaishi huko.

lugha

Picha
alt text

Papua New Guinea ina lugha nyingi zaidi ya nchi yoyote ulimwenguni—karibia lugha 840!

Makanisa

Picha
alt text

Mafuriko hutokea kila mara huko Papua New Guinea. Kwa hiyo majengo ya kanisa huko yanajengwa juu ya nguzo. Wakati mafuriko yanapokuja, waumini wanaweza kutumia mitumbwi yao kufika mlangoni mwa kanisa!

Ndege wa Msituni

Picha
alt text

Ndege wa paradiso ni ndege wa msituni wenye haya. Ndege wa kiume wana mabawa mazuri yenye rangi nyingi. Ndege wa Raggiana wa paradiso yuko kwenye bendera ya nchi.

Imba-Imba

Picha
alt text

Makabila katika Papua New Guinea hukushanyika kuimba, kucheza dansi, kushiriki tamaduni na kufanya urafiki. Zaidi ya makabila 100 huunganika kwenye imba-imba kila mwaka!

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Zhen Liu