Rafiki
Ninaweza Kuwaalika Wengine Kumfuata Yesu
Machi 2024


“Ninaweza Kuwaalika Wengine Kumfuata Yesu,” Rafiki, Machi 2024, 13.

Nenda na Utende

Ninaweza Kuwaalika Wengine Kumfuata Yesu

Kama vile Nefi, unaweza kwenda na kutenda vitu ambavyo Bwana ameamuru. (Ona 1 Nefi 3:7.)

Kuna njia nyingi sana unaweza kuwaalika wengine kumfuata Yesu Kristo. Jaribu wazo moja au mawili kati ya hayo hapo chini. Au andika wazo lako mwenyewe!

Picha
alt text
  • Mwalike mtu fulani kwenda kanisani pamoja nawe.

  • Mtumikie mtu fulani pamoja na rafiki.

  • Mwalike mtu fulani kwenye shughuli ya Kanisa.

  • Tazameni video ya Kanisa pamoja.

  • Tengeneza kazi ya mikono kutoka kwenye shughuli za “Njoo, Unifuate” pamoja na rafiki.

Picha
alt text

Wakati nilipobatizwa, nilimwalika rafiki yangu kutoka shuleni ambaye haudhurii kanisani kwetu. Ilikuwa vyema sana kwamba alikuja pamoja na familia yake.

Sofia D., umri miaka 8, Alberta, Canada

Picha
PDF ya hadithi

Kielelezo na Corey Egbert