Rafiki
Pasaka ni Nini?
Machi 2024


“Pasaka ni Nini?” Rafiki, Machi 2024, 46–47.

Misingi ya Injili

Pasaka ni nini?

Picha
alt text

Pasaka ni muda maalumu wa kufikiria kuhusu Yesu Kristo.

Wakati wa Pasaka, tunakumbuka kwamba Yesu anajua jinsi tunavyohisi. Alihisi uchungu wetu na huzuni yetu.

Yesu alikufa msalabani kwa sababu Yeye anatupenda. Mwili Wake uliwekwa kaburini.

Baada ya siku tatu, kaburi lilikuwa tupu. Yesu alikuwa hai tena! Tunaliita tukio hili Ufufuko.

Kwa sababu ya Yesu, sisi sote tutaishi baada ya kufa. Tunaweza kuhisi upendo kutoka kwa Baba wa Mbinguni na Yesu kila siku, siyo tu wakati wa Pasaka!