Rafiki
Janeelyn Anaacha Kuperuzi
Machi 2024


“Janeelyn Anaacha Kuperuzi,” Rafiki, Machi 2024, 36–37.

Janeelyn Anaacha Kuperuzi

Janeelyn alikuwa anataka kuona video inayofuata. Na iliyofuatia. Na iliyofuatia.

Hadithi hii ilitokea huko Malaysia.

Picha
alt text

Janeelyn anapitisha kidole gumba chake kwenye skrini ya simu. Ghafla video inatokezea. Aliamua kutazama moja, kisha anaendelea kuperuzi tena. Kisha akatua kwenye video nyingine. Ina lugha chafu sana, lakini ilikuwa inachekesha, kwa hiyo aliendelea kutazama. Na kisha aliendelea kuperuzi.

“Janeelyn! Unataka kuja kuchora?” Dada yake mdogo Jojo alimpungia kipande cha karatasi.

Janeelyn alitazama juu. “Sio sasa hivi.”

“SAWA.” Jojo alinuna na kuweka karatasi chini.

Peruzi. Peruzi. Peruzi. Video za wanyama wazuri. Video za watu maarufu. Video za watoto wadogo wakidansi. Na video chache Janeelyn alijua hazikuwa nzuri kutazama. SAWA, labda nyingi kuliko chache. Janeelyn alianza kuhisi kama angepaswa kuacha kuzitazama.

Lakini watu pia waliposti vitu vingi vizuri, aliwaza. Pia hata alijifunza njia mpya za kuchora kutokana na video chache.

“Janeelyn,” Mama alimwita.

“Hmm?” Janeelyn hata hakutazama juu wakati huu.

“Tutakula wali wa kukaangwa kwa chakula cha baharini usiku wa leo,” Mama alisema. “Unaweza kunisaidia kupika?”

Janeelyn alipenda wali uliokaangwa kwa chakula cha baharini. Lakini kwa sasa hakutaka kuinuka.

“Je, ninaweza tu kuandaa meza?” aliuliza. “Ninaweza kusaidia kuosha vyombo baadaye pia.”

“Hiyo ni sawa,” mama alisema. “Lakini unahitajika kuiandaa meza vizuri wakati nitakapokuomba. Na kisha itakuwa ni wakati wa kurudisha simu. Sawa?”

“Sawa,” Janeelyn alisema.

Janeelyn aliendelea kutazama video. Tena, akahisi kwamba hakupaswa kuzitazama. Lakini alikuwa na ari ya kuona video inayofuata. Na iliyofuatia. Na iliyofuatia. Peruzi. Peruzi. Ilikuwa ni vigumu kuacha!

Mwishowe Janeelyn aliweka simu chini. Sawa, labda angeweza tu kumalizia video moja ya mwisho . . . .

Hapana, Janeelyn alijiambia mwenyewe kwa uthabiti. Roho Mtakatifu alikuwa amempa msukumo, na alitaka kusikiliza. Mkono wake bado ulikuwa juu karibu na simu. Ilikuwa jaribu kubwa sana! Janeelyn alifumba macho yake kwa nguvu.

Baba Mpendwa wa Mbinguni, alisali kimya kimya. Ninajaribu sana kumsikiliza Roho Mtakatifu, lakini ninahitaji msaada. Ninataka kuacha kutazama video hizi, lakini sina uhakika wa jinsi ya kufanya hivyo. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Wakati huo huo, Mama alimwita aandae meza. Janeelyn aliruka na kutabasamu. Hiyo ilikuwa njia moja ya kumsaidia kumwondoa kwenye simu.

Janeelyn aliweka sahani kwenye meza. “Mama, niliona vitu fulani vibaya kwenye simu,” Janeelyn aliropoka.

Mama alihamisha macho kutoka kwenye mapishi yake. “Vitu vya aina gani?”

“Vitu tu kama, maneno machafu na video mbaya.” Janeelyn alipandisha na kushusha mabega. “Lakini si zote mbaya.”

“Je, Ulifanya nini wakati ulipoona vitu vibaya? Mama aliuliza.

Janeelyn alikuwa kimya kwa muda. Aliweka kikombe kwenye kila sehemu.

“Niliendelea kutazama,” alisema. “Sijui kwa nini. Lakini Roho Mtakatifu aliniambia niache, kwa hiyo nilisali kwa ajili ya msaada.

Mama aliweka sinia linalotoa mvuke la wali uliokaangwa na chakula cha baharini kwenye meza. “Wakati mwingine huwa ni vigumu sana kuacha kufanya vitu hata wakati tunapojua ni vibaya,” alisema. “Na wakati hilo linapofanyika, jambo zuri tunaloweza kufanya ni kusali.”

Janeelyn alitabasamu. “Kwa hiyo nilifanya jambo sahihi.”

“Hakika.” Mama alimpa Janeelyn vijiko aviweke mezani. “Na intaneti siyo mbaya hivyo. Inaweza kutusaidia tuunganike na marafiki na tushiriki mawazo. Lakini inaweza kuwa vigumu kukaa mbali na vitu vyote vibaya pia. Kuanzia sasa na kuendelea, kama utatazana video, acha tu tuzitazame pamoja. Kwa njia hiyo, mimi pamoja na Baba tunaweza kukusaidia kama umeona kitu kibaya.”

Janeelyn aliitikia kwa kichwa. Wakati uliofuata alitazama video pamoja na Mama na Baba. Hadi wakati huo, kulikuwa na vitu vingi vya burudani ambavyo yeye angeweza kufanya bila simu.

“Unaweza kumwambia kila mtu ni wakati wa chakula cha jioni?” Mama alimuomba.

“Ndiyo! Na baada ya chakula cha jioni, ninaenda kuchora pamoja na Jojo!”

Picha
alt text
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Mitch Miller