Maandiko Matakatifu
Moroni 8


Mlango wa 8

Ubatizo wa watoto wachanga ni uovu wa machukizo—Watoto wachanga wameokolewa na Kristo kwa sababu ya Upatanisho—Imani, toba, unyenyekevu na upole wa moyo, kupokea Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho yanaelekeza kwa wokovu. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Barua ya ababa yangu Mormoni, iliyoandikwa kwangu, Moroni; na iliandikwa kwangu mara baada nilipoitwa kwa huduma. Na kwa njia hii aliniandikia, akisema:

2 Mwana wangu mpendwa, Moroni, ninafurahi sana kwamba Bwana wako Yesu Kristo amekuwa mwangalifu kwako, na amekuita kwa huduma yake, na kwa kazi yake takatifu.

3 Ninakukumbuka wewe kila siku katika sala zangu, siku zote nikisali kwa Mungu Baba katika jina la Mtoto wake Mtakatifu, Yesu, kwamba yeye, kupitia kwa auzuri wake na bneema usio na mwisho, atakulinda kupitia uvumilivu wa imani kwa jina lake milele.

4 Na sasa, mwana wangu, ninakuzungumzia kuhusu lile ambalo linanisikitisha sana; kwani ninasikitishwa kwamba augomvi unaweza kutokea miongoni mwenu.

5 Kwani, ikiwa nimejulishwa ukweli, kumekuwa na ugomvi miongoni mwenu kuhusu ubatizo wa watoto wenu wachanga.

6 Na sasa, mwana wangu, ninataka ufanye kazi kwa bidii, ili hili kosa kubwa litolewe miongoni mwenu; kwani, kwa kusudi hili nimeandika hii barua.

7 Kwani mara moja nilipojua vitu hivi kuwahusu nilimwuliza Bwana kuhusu jambo hili. Na aneno la Bwana lilinijia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, likisema:

8 Sikiliza maneno ya Kristo, Mkombozi wako, Bwana wako na Mungu wako. Tazama, nilikuja duniani sio kuwaita walio na haki bali wenye dhambi kwenye toba; wenye aafya hawahitaji tabibu, bali wale walio wagonjwa; kwa hivyo, bwatoto wachanga ni cwazima, kwani hawana uwezo wa kutenda ddhambi; kwa hivyo laana ya eAdamu imetolewa kwao ndani yangu, kwamba haina uwezo juu yao; na sheria ya fkutahiriwa imeisha kwa ajili yangu.

9 Na katika njia hii Roho Mtakatifu alidhihirisha neno la Mungu kwangu; kwa hivyo, mwana wangu mpendwa, ninajua kwamba ni mzaha wa unadhiri mbele ya Mungu, kwamba mbatize watoto wachanga.

10 Tazama ninakwambia kwamba kitu hiki utafundisha—toba na ubatizo kwa wale ambao awanawajibika wenye uwezo wa kutenda dhambi; ndiyo, fundisha wazazi kwamba lazima watubu na wabatizwe, na wajinyenyeze kama bwatoto wao wachanga.

11 Na awatoto wao wachanga hawahitaji toba yoyote, wala ubatizo. Tazama, ubatizo upo katika toba ili kutimiza amri kwa bmsamaha wa dhambi.

12 Lakini awatoto wachanga ni wazima katika Kristo, hata kutokea mwanzo wa dunia; ikiwa si hivyo, Mungu ni Mungu wa upendeleo, na pia Mungu wa kugeuka, na mwenye bkupendelea watu; kwani ni watoto wangapi wachanga wamekufa bila kubatizwa!

13 Kwa hivyo, ikiwa watoto wachanga hawangeweza kuokolewa bila ubatizo, hao lazima wangeenda kwenye jehanamu ya milele.

14 Tazama ninawaambia, yule ambaye anadhani kwamba watoto wachanga wanahitaji ubatizo yuko kwenye nyongo chungu na katika kifungo cha uovu; kwani hana aimani, wala tumaini, wala hisani; kwa hivyo, ikiwa atakufa kama bado anafikiria hivyo, ataenda jehanamu.

15 Kwani kutisha ni uovu kudhani kwamba Mungu huokoa mtoto mmoja kwa sababu ya ubatizo, na mwingine lazima aangamie kwa sababu hakubatizwa.

16 Laana iwe kwa wale ambao wataharibu njia za Bwana kwa utaratibu huu, kwani wataangamia wasipotubu. Tazama, naongea kwa ujasiri, nikiwa na auwezo kutoka kwa Mungu; na siogopi kile watu wanachoweza kufanya; kwani bupendo ulio kamili chutupa nje hofu.

17 Na nimejaa na ahisani, ambayo ni upendo usio na mwisho; kwa hivyo, watoto wote ni kama mimi; kwa hivyo, ninapenda bwatoto wachanga na upendo ulio kamili; na wote wako sawa na washiriki wa wokovu.

18 Kwani najua kwamba Mungu si Mungu wa kupendelea, wala kiumbe akinachobadilika; lakini habadiliki kutoka milele hadi milele byote.

19 aWatoto wachanga hawawezi kutubu; kwa hivyo, ni uovu wa kutisha kukana rehema safi ya Mungu kwao, kwani wote ni wazima ndani yake kwa sababu ya brehema yake.

20 Na yule anayesema kwamba watoto wachanga wanahitaji ubatizo anakana huruma za Kristo, na huweka bure aupatanisho wake na nguvu ya ukombozi wake.

21 Ole kwa hawa, kwani wako katika hatari ya kifo, ajehanamu, na maumivu ya bmilele. Ninazungumza kwa ujasiri; Mungu ameniamrisha. Yasikilize na uyafuate, au yatatumiwa kwako kwa kiti cha chukumu cha Kristo.

22 Kwani tazama kwamba watoto wote wachanga ni awazima katika Kristo; na pia wale wote ambao hawana bsheria. Kwani nguvu ya cukombozi huja kwa wote ambao hawana sheria; kwa hivyo, yule ambaye hahukumiwi, au yule ambaye hayuko chini ya hukumu yoyote, hawezi kutubu; na kwa hao ubatizo hauleti chochote—

23 Lakini ni mzaha mbele ya Mungu, kukana huruma za Kristo, na nguvu za Roho Mtakatifu wake, na kuweka tumaini katika akazi zisizo na uhai.

24 Tazama, mwana wangu, kitu hiki kisifanyike; kwani atoba ni kwa wale ambao wako chini ya hukumu na chini ya laana ya sheria iliyovunjwa.

25 Na matokeo ya kwanza ya atoba ni bubatizo; na ubatizo huja na imani kwa kutimiza amri; na kule kutimiza amri huleta ckusamehewa kwa dhambi;

26 Na kusamehewa kwa dhambi huleta aunyenyekevu, na upole wa moyo; na kwa sababu ya unyeyekevu na upole wa moyo huja bRoho Mtakatifu, cMfariji ambaye hujaza dtumaini na upendo kamili, eupendo ambao huvumilia kwa fsala ya gbidii, mpaka mwisho utakapokuja, wakati hwatakatifu wote watakapoishi na Mungu.

27 Tazama, mwana wangu, nitakuandikia tena ikiwa sitaenda nje tena mapema dhidi ya Walamani. Tazama, akiburi cha taifa hili, au watu wa Wanefi, kimeleta uangamizo wao isipokuwa watubu.

28 Waombee, mwana wangu, kwamba toba ije kwao. Lakini tazama, ninaogopa isiwe Roho amekoma akujitahidi nao; na katika sehemu hii ya nchi wanataka kuweka chini nguvu zote na mamlaka ambayo inatoka kwa Mungu; na bwanamkana Roho Mtakatifu.

29 Na baada ya kukataa elimu kubwa hivyo, mwana wangu, lazima waangamie karibuni, kwa kutimiza unabii ambao ulizungumzwa na manabii, na pia maneno ya Mwokozi wetu mwenyewe.

30 Kwaheri, mwana wangu, mpaka nitakapokuandikia, au nitakapokutana nawe tena. Amina.