Maandiko Matakatifu
Alma 13


Mlango wa 13

Wanaume wanaitwa kama makuhani wakuu kwa sababu ya imani yao kuu na matendo mema—Watapaswa kufundisha amri—Kupitia haki wanatakaswa na kuingia katika pumziko la Bwana—Melkizedeki alikuwa mmoja wa hawa—Malaika wanatangaza habari njema kote nchini—Watatangaza ujio halisi wa Kristo. Karibia mwaka 82 K.K.

1 Na tena, ndugu zangu, ningetaka nikumbushe fikira zenu kuhusu ule wakati ambao Bwana Mungu aliwapatia watoto wake amri hizi; na ningetaka mkumbuke kwamba Bwana Mungu aaliwatawaza makuhani, kulingana na mpango wake mtakatifu, ambao ni ule mpango wa Mwana wake, kufundisha watu vitu hivi.

2 Na makuhani hao walitawazwa kulingana na ampango wa Mwana wake, katika bhali ambayo watu wangejua ni vipi watakavyomtumainia Mwana wake kwa ukombozi.

3 Na hivi ndivyo jinsi walivyotawazwa—awakiitwa na bkutayarishwa tangu cmsingi wa ulimwengu kulingana na dufahamu wa mbeleni wa Mungu, kwa ajili ya imani yao kuu na vitendo vyao vyema; mwanzoni wakiruhusiwa ekuchagua baina ya mema na maovu; kwa hivyo wao wakiwa wamechagua mema, na kufanya mazoezi ya imani fkuu, gwameitwa kwa mwito mtakatifu, ndiyo, kwa ule mwito mtakatifu ambao ulitayarishwa, na kulingana na, matayarisho ya ukombozi wao.

4 Na hivyo awameitwa kwa mwito huu mtakatifu kwa ajili ya imani yao, wakati wengine wangemkataa Roho wa Mungu kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao na upofu wa fikira zao, wakati, kama isingekuwa kwa sababu hii wangekuwa na bmamlaka makuu kama ndugu zao.

5 Au kwa kifupi, hapo mwanzoni walikuwa katika hali asawa na ndugu zao; hivyo mwito huu mtakatifu ukiwa umetayarishwa tangu msingi wa ulimwengu kwa wale ambao hawangeshupaza mioyo yao, kupitia na katika upatanisho wa Mwana wa Pekee, ambaye alitayarishwa—

6 Na hivyo kuitwa na mwito huu mtakatifu, na kutawazwa ukuhani mkuu wa mpango mtakatifu wa Mungu, kufundisha watoto wa watu amri zake, ili nao pia waingie katika apumziko lake—

7 Ukuhani huu mkuu ukiwa kwa ule mpango wa Mwana wake, mpango ambao ulikuwa tangu msingi wa ulimwengu; au kwa maneno mengine, ahaukuwa na mwanzo wa siku au mwisho wa miaka, ukiwa ulitayarishwa tangu milele hadi milele, kulingana na bufahamu wake wa mbele wa vitu vyote—

8 Sasa awalitawazwa kwa njia hii—wakiwa wameitwa kwa mwito mtakatifu, na kutawazwa kwa agizo takatifu, na kuchukua ukuhani mkuu juu yao wa mpango mtakatifu, ambao ni mwito, na agizo, na ukuhani mkuu, usio na mwanzo au mwisho—

9 Hivyo wakawa amakuhani wakuu milele, kulingana na mpango mtakatifu wa Mwana wa Pekee wa Baba, ambaye hana mwanzo wa siku au mwisho wa miaka, ambaye amejaa bneema, ukweli, na haki. Na hivyo ndivyo ilivyo. Amina.

10 Sasa, kama vile nilivyosema kuhusu mpango huu mtakatifu, au huu aukuhani mkuu, kulikuwa na wengi ambao walitawazwa na kuwa makuhani wakuu wa Mungu; na ilikuwa kwa ajili ya imani yao kuu na btoba, na haki yao mbele ya Mungu, wao wakichagua kutubu na kutenda haki badala ya kuangamia;

11 Kwa hivyo waliitwa kulingana na mpango huu mtakatifu, na awakatakaswa, na bmavazi yao yakaoshwa na kuwa meupe kupitia damu ya Mwanakondoo.

12 Na wao, baada ya akutakaswa na bRoho Mtakatifu, na mavazi yao kufanywa meupe, yakiwa csafi na bila doa mbele ya Mungu, hawangetazama ddhambi bila ekukerwa; na kulikuwa na wengi, wengi sana, ambao walifanywa safi na kuingia katika pumziko la Bwana Mungu wao.

13 Na sasa, ndugu zangu, ningetaka kwamba mjinyeyekeze mbele ya Mungu, na mzae amatunda yanayostahili toba, ili ninyi pia muingie katika hilo pumziko.

14 Ndiyo, jinyenyekeeni hata kama wale watu waliokuwa katika siku za aMelkizedeki, ambaye pia alikuwa kuhani mkuu kulingana na ule mpango ambao nimeuzungumzia, ambaye pia aliuchukua ukuhani mkuu milele.

15 Na ilikuwa ni kwa huyu Melkizedeki ambaye aIbrahimu alilipa bzaka; ndiyo, hata baba yetu Ibrahimu alilipa zaka ya fungu la kumi ya mali yote aliyokuwa nayo.

16 Sasa haya amaagizo yalitolewa kwa namna hii, ili watu wamtazamie Mwana wa Mungu, ambayo ikiwa ni bmfano wa mpango wake, au ukiwa mpango wake, na ili wamtazamie mbele kwake kwa ondoleo la dhambi zao, ili waingie katika pumziko la Bwana.

17 Sasa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme katika nchi ya Salemu; na watu wake walikuwa wametumbukia katika uovu na machukizo; ndiyo, wote walikuwa wamepotea njia; walikuwa wamejaa kila aina ya uovu;

18 Lakini Melkizedeki akiwa na imani kuu, na kuipokea ofisi ya ukuhani mkuu kulingana na ampango mtakatifu wa Mungu, aliwahubiria watu wake toba. Na tazama, walitubu; na Melkizedeki aliimarisha amani nchini katika siku zake; kwa hivyo aliitwa mwana mfalme wa amani, kwani alikuwa mfalme wa Salemu; na alitawala chini ya baba yake.

19 Sasa, kulikuwa na awengi mbele yake, na pia kulikuwa na wengi baadaye, lakini bhapakuwa na yeyote aliyekuwa mkuu zaidi; kwa hivyo, wamemtaja yeye zaidi.

20 Sasa hakuna haja ya kurudia jambo hili; yale ambayo nimesema yametosha. Tazama, amaandiko yako mbele yenu; bmkiyapinga itakuwa ni kwa maangamizo yenu.

21 Na sasa ikawa kwamba baada ya Alma kusema maneno haya kwao, alinyosha mkono wake kwao na kuongea kwa sauti kuu, akisema: Sasa ndiyo wakati wa akutubu, kwani siku ya wokovu inakaribia;

22 Ndiyo, na sauti ya Bwana, kwa amdomo wa malaika, inatangazia mataifa yote; ndiyo, inaitangaza, kwamba wawe na habari njema kuu ya shangwe kuu; ndiyo, anaitangaza habari hii njema miongoni mwa watu wake wote, ndiyo, hata kwa wale ambao wametawanyika kote usoni mwa dunia kwa hivyo wametujia.

23 Na wametufahamisha kwa misemo iliyo awazi, ili tufahamu, ili tusikose; na hii ni kwa sababu sisi ni bwazururaji katika nchi ngeni; kwa hivyo, tumeheshimiwa zaidi, kwani tumeelezewa habari hii njema katika pande zote za shamba letu la mizabibu.

24 Kwani tazama, amalaika wanawatangazia wengi sasa katika nchi yetu; na hii ni kwa lengo la kutayarisha mioyo ya watoto wa watu ili wapokee neno lake atakaporudi katika utukufu wake.

25 Na sasa tunasubiri tu kusikia habari njema tukihubiriwa kwa mdomo wa malaika, kuhusa kuja kwake; kwani wakati unakuja, na ahatujui ni lini. Namwomba Mungu kwamba iwe katika siku zangu; lakini ikiwa sasa au baadaye, nitaifurahia.

26 Na itafahamishwa kwa watu wenye ahaki na watakatifu, kwa mdomo wa malaika, wakati wa kuja kwake, kwamba maneno ya babu zetu yatimizwe, kulingana na yale ambayo waliyozungumza kumhusu, ambayo yalikuwa ni kulingana na roho ya unabii iliyokuwa ndani yao.

27 Na sasa, ndugu zangu, anatamani kutoka sehemu za ndani kabisa za moyo wangu, ndiyo, kwa wasiwasi mwingi na hata kwa uchungu, kwamba msikilize maneno yangu, na mtupe dhambi zenu, na kwamba msiahirishe siku ya toba yenu;

28 Lakini kwamba mtajinyenyekeza mbele ya Bwana, na mliite jina lake takatifu, na akukesha na kusali daima, kwamba bmsijaribiwe zaidi ya yale ambayo mnaweza kuvumilia, na hivyo mwongozwe na Roho Mtakatifu, katika kuwa wanyenyekevu, cwapole, watiifu, wenye subira, wenye upendo na wenye uvumilivu;

29 aMkimwamini Bwana; mkitumaini kwamba mtapokea uzima wa milele; mkiwa na bupendo wa Mungu daima katika mioyo yenu, kwamba muinuliwe katika siku ya mwisho na muingie katika cpumziko lake.

30 Na ikiwezekana Bwana awape toba, kwamba msijiteremshie ghadhabu yake, kwamba msifungiwe na minyororo ya ajehanamu, kwamba msipate bmauti ya pili.

31 Na Alma aliwazungumzia watu maneno mengi, ambayo hayajaandikwa katika kitabu hiki.