Maandiko Matakatifu
Alma 22


Mlango wa 22

Haruni anamfundisha baba ya Lamoni kuhusu Uumbaji na Anguko la Adamu, na mpango wa ukombozi kupitia Kristo—Mfalme na nyumba yake yote wanaongolewa—Mgawanyo wa ardhi kati ya Wanefi na Walamani unaelezwa. Karibia mwaka 90–77 K.K.

1 Sasa, vile Amoni alikuwa hivyo alikuwa anafundisha watu wa Lamoni bila kikomo, tutarudia historia ya Haruni na ndugu zake; kwani baada ya kuondoka kutoka kwenye nchi ya Midoni aaliongozwa na Roho hadi kwenye nchi ya Nefi, hata kwenye nyumba ya mfalme ambaye alikuwa anasimamia nchi yote bisipokuwa nchi ya Ishmaeli; na alikuwa baba ya Lamoni.

2 Na ikawa kwamba alimwendea kwenye nyumba ya mfalme, na ndugu zake, na akasujudu mbele ya mfalme, na kusema kwake: Tazama, Ee mfalme, sisi ni ndugu za Amoni, ambaye aulimwachilia huru kutoka gerezani.

3 Na sasa, Ee mfalme, ikiwa utasalimisha maisha yetu, tutakuwa watumishi wako. Na mfalme akawaambia: Amkeni, kwani nitamruhusu muishi, na sitakubali muwe watumishi wangu; lakini nitasisitiza kwamba mnitumikie, kwani nimesumbuliwa kidogo rohoni mwangu kwa sababu ya ukarimu mkuu wa maneno ya ndugu yako Amoni; na ninatamani kujua sababu iliyomfanya asitoke na ninyi Midoni.

4 Na Haruni akamwambia mfalme: Tazama, Roho wa Bwana amemtuma mahali pengine; ameenda kwenye nchi ya Ishmaeli, kuwafundisha watu wa Lamoni.

5 Sasa mfalme akamwambia: Ni nini hiki ambacho mmekisema kuhusu Roho wa Bwana? Tazama, hiki ni kitu ambacho kinanisumbua.

6 Na pia, ni nini hiki ambacho Amoni alikisema—aIkiwa mtatubu mtasamehewa, na ikiwa hamtatubu, mtatupiliwa mbali siku ya mwisho?

7 Na Haruni akamjibu na kumwambia: Unaamini wewe kwamba kuna Mungu? Na mfalme akasema: Ninajua kwamba Waamaleki wanasema kwamba kuna Mungu, na nimewaruhusu kwamba wajenge makanisa, kwamba wangekusanyika pamoja kumwabudu. Na sasa ikiwa unasema kuna Mungu, tazama, anitaamini.

8 Na sasa Haruni aliposikia hivi, moyo wake ulianza kufurahi, na akasema: Tazama, kwa hakika vile unavyoishi, Ee mfalme, kuna Mungu.

9 Na mfalme akasema: Mungu ni yule aRoho Mkuu aliyewaleta babu zetu kutoka nchi ya Yerusalemu?

10 Na Haruni akamwambia: Ndiyo, ni yule Roho Mkuu, na aaliumba vitu vyote mbinguni na ardhini. Unaamini hivi wewe?

11 Na akasema: Ndiyo, ninaamini kuwa Roho Mkuu aliumba vitu vyote, na ninataka kwamba uniambie kuhusu hivi vitu vyote, na anitaamini maneno yako.

12 Na ikawa kwamba wakati Haruni alipoona kwamba Mfalme angeamini maneno yake, alianzia tangu Adamu alivyoumbwa, aakisoma maandiko kwa mfalme—vile Mungu alivyomuumba mwanadamu kwa mfano wake mwenyewe, na kwamba Mungu alimpatia amri, na kwa sababu ya dhambi, binadamu alikuwa ameanguka.

13 Na Haruni akamwelezea maandiko kuanzia auumbaji wa Adamu, akimwelezea binadamu alivyoanguka, na hali ya kimwili sasa na pia bmpango wa ukombozi, ambao ulitayarishwa ctangu uumbaji wa ulimwengu, kupitia kwa Kristo, kwa wote ambao wataamini katika jina lake.

14 Na kwa sababu binadamu alikuwa aameanguka hangeweza bkustahili chochote mwenyewe; isipokuwa mateso na kifo cha Kristo chulipia dhambi zao, katika imani na kutubu, na vingine; na kwamba hukata kamba za kifo, kwamba dkaburi halitakuwa na ushindi, na kwamba uchungu wa kifo utashindwa katika matumaini ya utukufu; na Haruni alieleza hivi vitu vyote kwa mfalme.

15 Na ikawa kwamba baada ya Haruni kumwelezea hivi vitu, mfalme alisema: Nitafanya anini ili nipate uzima wa milele ambao umeuzungumzia? Ndiyo, nitafanya nini ili bnizaliwe kwa Mungu, ili hii roho mbovu ingʼolewe nje ya mwili wangu, na nipokee Roho yake, ili niweze kujazwa na shangwe, ili nisitupiliwe nje siku ya mwisho? Tazama, alisema, nitatoa umiliki wangu cwote, ndiyo, nitaacha ufalme wangu, ili nipokee hii shangwe kuu.

16 Lakini Haruni alimwambia: Ikiwa aunatamani kitu hiki, ikiwa utamsujudia Mungu, ndiyo, ikiwa utatubu dhambi zako zote, na umsujudie Mungu, na umlingane kwa imani, ukiamini kwamba utapokea, ndipo utakapopokea bmatumaini ambayo unatamani.

17 Na ikawa kwamba Haruni aliposema maneno haya, mfalme aalisujudu mbele ya Bwana, kwa magoti yake; ndiyo, hata akajilaza kifudifudi ardhini, na bkulia kwa nguvu, akisema:

18 Ee Mungu, Haruni ameniambia kwamba kuna Mungu; na ikiwa kuna Mungu, na ikiwa wewe ni Mungu, unaweza kujitambulisha kwangu, na nitaacha dhambi zangu zote ili nikujue wewe, na kwamba niinuliwe kutoka kwa wafu, na niokolewe siku ya mwisho. Na sasa wakati mfalme alipokuwa amesema maneno haya, alianguka akawa kama amekufa.

19 Na ikawa kwamba wafanyi kazi wake walikimbia na kumwambia malkia yote ambayo yalikuwa yametendeka kwa mfalme. Na akaja mahali ambapo mfalme alikuwa; na alipomwona amelala kama aliyekufa, na pia Haruni na ndugu zake wakisimama kama ndiyo waliosababisha kuanguka kwake, aliwakasirikia, na kuamuru kwamba watumishi wake, au watumishi wa mfalme, wawachukue na kuwaua.

20 Sasa watumishi walikuwa wameona kilichosababisha mfalme kuanguka, kwa hivyo hawakuthubutu kumshika Haruni na ndugu zake; na wakamsihi malkia wakisema: Kwa nini unatuamrisha tuue watu hawa, ikiwa tazama, mmoja wao yu amkuu kuliko sisi zote? Kwa hivyo wanaweza kutuua.

21 Sasa wakati malkia aliona woga wa watumishi, yeye pia alianza kuogopa sana, kwamba maovu yasimjie. Na akawaamrisha watumishi wake kwamba waende na kuita watu, ili wawaue Haruni na ndugu zake.

22 Sasa Haruni alipoona kusudi la malkia, yeye, pia akijua ugumu wa mioyo ya watu, aliogopa kwamba umati utakusanyika pamoja, na kuwe na ubishi mwingi na msukosuko miongoni mwao; kwa hivyo alinyosha mkono wake na kumuinua mfalme kutoka chini, na akamwambia: Simama. Na akasimama, miguu yake ikipata nguvu zake.

23 Sasa hii ilifanyika machoni mwa malkia na watumishi wengi. Na walipoiona walishangaa sana, na kuanza kuogopa. Na mfalme alisimama mbele, na kuanza akuwahudumia. Na aliwahudumia, jinsi kwamba jamii yake yote bilimgeukia Bwana.

24 Sasa kulikuwa na umati uliokusanyika kwa sababu ya amri ya malkia, na kukawa na manungʼuniko mengi miongoni mwao kwa sababu ya Haruni na ndugu zake.

25 Lakini mfalme alisimama mbele miongoni mwao na kuanza kuwahudumia. Na walitulizwa juu ya Haruni na wale ambao walikuwa na yeye.

26 Na ikawa kwamba wakati mfalme aliona kwamba watu wametulia, alisababisha kwamba Haruni na ndugu zake wasimame na kusogea katikati ya umati, na kwamba wawahubirie neno.

27 Na ikawa kwamba mfalme alitoa atangazo nchini kote, miongoni mwa watu wake wote ambao walikuwa kwenye nchi yake yote, ambao walikuwa ndani ya mikoa yote iliyokaribiana, hata karibu na bahari, upande wa mashariki na upande wa magharibi, na ambayo ilitengwa kutoka nchi ya bZarahemla na kipande chembamba cha nyika, ambayo ilinyooka kutoka mashariki ya bahari hadi magharibi ya bahari, karibu na mipaka ya pwani, na mipaka ya nyika ambao ulikuwa kaskazini karibu na nchi ya Zarahemla, kupitia mipaka ya Manti, kupitia kando ya mto wa Sidoni, kutoka mashariki hadi magharibi—na hivyo ndivyo Walamani na Wanefi walivyotenganishwa.

28 Sasa, sehemu kubwa ya Walamani ambao walikuwa awazembe waliishi nyikani, na kuishi kwenye hema; na walikuwa wametawanyika upande wa magharibi, katika nchi ya Nefi; ndiyo, na pia kwenye magharibi ya nchi ya Zarahemla, kwenye sehemu ya ukingo wa bahari, na magharibi kwenye nchi ya Nefi, mahali ambapo babu zao walirithi mbeleni, na hivyo ikipakana na ukingo wa bahari.

29 Na pia kulikuwa na Walamani wengi mashariki karibu na ukingo wa bahari, ambapo Wanefi waliwasukuma. Na hivyo Wanefi walizingirwa na Walamani; ingawaje Wanefi walikuwa wamemiliki sehemu ya kaskazini mwa nchi inayopakana na nyika, kwenye chimbuko ya mto Sidoni, kutoka mashariki, hadi magharibi, ikizunguka upande wa nyika; upande wa kaskazini, hata wakaja kwa nchi ambayo waliita aNeema.

30 Na ilikuwa imepakana na nchi waliyoiita aUkiwa, ikiwa mbali sana kaskazini kwamba iliingia katika nchi iliyokaliwa na watu na kuharibiwa, ambayo bmifupa yake tumeizungumzia, ambayo iligunduliwa na watu wa Zarahemla, ikawa mahali ambapo walishukia ckwanza.

31 Na walikuja kutokea kule juu hadi kwenye nyika ya kusini. Hivyo nchi ya kaskazini iliitwa aUkiwa, na nchi ya kusini iliitwa Neema, ilikuwa nyika ambayo imejazwa na wanyama wa kila aina, ambao wengi wao walitoka katika nchi ya kaskazini kwa ajili ya chakula.

32 Na sasa, ilikuwa tu amwendo wa siku moja na nusu kwa usafiri wa Mnefi, kwenye mpaka miongoni mwa Neema na nchi ya Ukiwa, kutoka mashariki hadi kwenye bahari ya magharibi; na hivyo nchi ya Nefi na nchi ya Zarahemla zilikuwa karibu zimezingirwa na maji, kukiwa na bkijisehemu cha nchi katikati ya nchi iliyo kaskazini na nchi iliyo kusini.

33 Na ikawa kwamba Wanefi walikuwa wameimiliki nchi ya Neema, hata kutokea mashariki hadi kwenye bahari ya magharibi, na hivyo Wanefi kwa hekima yao, na walinzi wao na majeshi yao, walikuwa wamewafungia Walamani upande wa kusini, kwa hivyo wasiwe tena na umiliki kaskazini, ili wasiweze kupita na kuleta vita kaskazini.

34 Kwa hivyo Walamani hawangemiliki kitu kingine isipokuwa tu nchi ya Nefi, na nyika iliyokuwa karibu. Sasa hii ilikuwa hekima kwa Wanefi—kwani Walamani walikuwa maadui kwao, hawangekubali mateso yao yatokee kila upande, na pia ili wapate nchi ambayo wangekimbilia, kulingana na mahitaji yao.

35 Na sasa mimi baada ya kusema haya, narudia tena historia ya Amoni na Haruni, Omneri na Himni, na ndugu zao.