Rafiki
Ushuhuda Wangu Mwenyewe
Januari 2024


“Ushuhuda Wangu Mwenyewe,” Rafiki, Jan. 2024, 38.

Imeandikwa na Wewe

Ushuhuda Wangu Mwenyewe

Jina langu ni Chloe na nina umri wa miaka tisa. Mambo yangu ya kupitisha muda ni kucheza tenisi, kuimba na kutengeneza marafiki.

Ninapenda kuwa kanisani na ninapenda kusaidia katika darasa langu la Msingi. Inanifanya nihisi vizuri. Ninapenda pia kuwatumikia wengine. Ninaipenda sana familia yangu. Nilimsaidia mdogo wangu wa kike Anna ajifunze kuendesha baiskeli. Nyakati zingine ninamsaidia mama yangu kusafisha vyombo.

Ninapenda pia kusoma Kitabu cha Mormoni pamoja na Familia yangu. Siku moja niliposoma hadithi ya Amoni, nilimhisi Roho Mtakatifu moyoni mwangu. Usiku huo, niliwaambia familia yangu, “Sasa ninajua kwa nini watu husema kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.” Nilihisi moyoni mwangu kwamba hadithi tulizokuwa tukisoma kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ni kweli zilitokea.

Ninajua Kanisa ni la kweli. Ninajua hadithi ndani ya Kitabu cha Mormoni ni za kweli. Ninajua Manabii wanaitwa na Mungu. Ninajua wamisionari wanaweza kutusaidia tumfuate Yesu. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Picha
Alt text

Kielelezo na Giovanni Abeille