Rafiki
Lengo la Kusoma
Januari 2024


“Lengo la Kusoma,” Rafiki, Jan. 2024, 36–37.

Lengo la Kusoma

Anders hakupenda kusoma kwa sauti.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Picha
alt text

Anders alimsikiliza dada yake akisoma wakati wa kujifunza maandiko kama familia. Alijaribu kufuatiliza kwenye kishikwambi chake. Lakini ilikuwa vigumu kufokasi kwenye maneno.

Anders mara zote alipata wakati mgumu kwenye kusoma. Mwaka uliopita, aligundua kwamba alikuwa na dyslexia. Dyslexia ulikuwa ulemavu wa kujifunza ambao ulifanya iwe vigumu kusoma. Ubongo wake ulichanganya maneno na herufi na macho yake yaliruka kila mahala kwenye ukurasa wakati alipojaribu kusoma.

Dada yake alimaliza kusoma mstari wake na kaka yake alisoma mstari uliofuata. Lakini Anders hakusoma. Hakupenda kusoma kwa sauti. Kufanya maneno yawe makubwa kwenye kishikwambi chake kulisaidia kidogo. Lakini hakupenda jinsi alivyosoma taratibu na vibaya. Alifanya makosa mengi! Ilimbidi afanye kazi kubwa kwenye kile kilichoonekana rahisi kwa kila mmoja.

Walipomaliza kusoma, familia ya Anders walitazama video. Ilikuwa kuhusu Programu ya Watoto na Vijana.

“Weka malengo binafsi ambayo yanahitaji uwezo wako wote na yanakupa changamoto,” Mzee Gong alisema kwenye video. “Gundua talanta mpya, vitu unavyopendelea na ujuzi.”*

Anders alifikiria kuhusu malengo ambayo angeweza kuyaweka. Pengine angejifunza jinsi ya kuoka biskuti. Au kucheza soka vizuri!

Kisha aliangalia Kitabu cha Mormoni juu ya meza. Kuwa bora kwenye kusoma haikuonekana kama lengo la kuburudisha. Lakini alitamani aweze kusoma maandiko na familia yake.

“Ninajua ninataka lengo langu liwe lipi,” alimwambia Baba.

“Ni lipi?” Baba aliuliza.

Anders alichukua Kitabu cha Mormoni. “Ninataka kusoma mstari mmoja wa Kitabu cha Mormoni kwa sauti kila siku.”

“Hilo linaonekana kama lengo zuri,” Baba alisema. “Ni lini unataka kuanza?”

“Sasa hivi!”

Anders alikwenda chumbani kwake na kufunga mlango. Hakutaka yeyote amsikie. Kisha alifungua Kitabu cha Mormoni. Alichanganya baadhi ya maneno, lakini ilimchukua dakika tu kumaliza mstari wa kwanza. Haikuwa mbaya sana, aliwaza.

Anders alisoma maandiko kila siku. Ilikuwa vigumu! Hakuhisi kama alikuwa akipiga hatua. Lakini aliendelea kulifanyia kazi.

Ndipo siku moja shuleni, mwalimu wake alisema, “Lo! Nashangaa ni kwa haraka kiasi gani unajifunza.

Anders alitazama juu kutoka kwenye kazi yake ya nyumbani. “Kweli?”

Mwalimu aliitikia kwa kichwa. “Unapiga hatua kubwa sana.”

Anders alitazama chini kwenye maneno yaliyo kwenye karatasi yake. Yalikuwa rahisi kusomeka kuliko yalivyokuwa hapo kabla. Lengo lake la kufanyia mazoezi usomaji wa maandiko lilikuwa likimsaidia kujifunza hata shuleni.

Aliporudi nyumbani, alikimbia kupanda ngazi ili asome maandiko yake. Alipotazama kwenye ukurasa, maneno bado yalionekana kuhama hama. Lakini kwa juhudi ilikuwa rahisi kuelewa kile maneno yalichosema.

Anders alikuwa na shauku kwa ajili ya usomaji wa maandiko kama familia usiku ule.

“Baba,” alisema. “Naweza kusaidia kusoma leo?”

Baba alitoa mgumio wa kuonesha shauku. “Ningependa ufanye hivyo!”

Anders alifuatilia kwa makini wakati kaka zake na dada zake kila mmoja akisoma mstari. Ilipofika zamu yake, alisoma mstari taratibu ili kuhakikisha kwamba alitamka kila neno kwa usahihi. Alipomaliza kusoma, aliinua kichwa. Kila mmoja alikuwa akitabasamu.

Japokuwa hakuwa msomaji mzuri, Anders alijivunia jinsi alivyo. Alijua kwamba akiweka juhudi, Baba wa Mbinguni daima angekuwepo kumsaidia.

Picha
alt text
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Kelly Smith

  • Face to Face with Elder Gerrit W. Gong (worldwide broadcast, Nov. 17, 2019), Gospel Library.