Rafiki
Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo
Januari 2024


“Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo,” Rafiki, Jan. 2024, 24–25.

Jifunze kuhusu Kitabu cha Mormoni

Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo

Picha
alt text

Kitabu cha Mormoni ni kitabu cha maandiko. Kama vile Biblia, kinatufundisha zaidi kuhusu Yesu Kristo. Ndiyo maana kinaitwa “ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo.”

Kitabu cha Mormoni kina hadithi za manabii ambao walifundisha kwamba Yesu Kristo angekuja duniani. Kinasimulia pia kuhusu jinsi Alivyotembelea Amerika baada ya Ufufuko Wake na aliwafundisha watu huko. Kinatufundisha pia jinsi tunavyoweza kumfuata.

Yesu anakupenda na atakusaidia. Huu ni ujumbe muhimu wa Kitabu cha Mormoni.

Picha
alt text

Utafutaji wa Maandiko!

  • Kitabu cha kwanza katika Kitabu cha Mormoni ni kipi?

  • Majina ya baba na mama wa Nefi yalikuwa yapi?

  • Akina nani walikuwa ndugu wa kiume katika familia ya Nefi mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni?

Ninaweza kusoma Kitabu cha Mormoni!

Baada ya kusoma, paka rangi sehemu ya picha. Unaweza kusoma maandiko haya yanayoenda sambamba na usomaji wa kila wiki kutoka Njoo, Unifuate.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Jared Beckstrand