Rafiki
Mti wa uzima
Januari 2024


“Mti wa Uzima,” Rafiki, Jan. 2024, 26–27.

Hadithi za Maandiko

Mti wa uzima

Picha
Alt text

Kielelezo na Andrew Bosley

Picha
alt text

Lehi alikuwa nabii. Mungu alimwambia aichukue familia yake waende nchi ya ahadi. Wakati wakisafiri, alipata ndoto kuhusu mti mzuri. Uliitwa mti wa uzima.

Picha
alt text
Picha
alt text

Mti ulizaa tunda jeupe tamu sana. Lehi alihisi furaha sana alipolila! Alitaka familia yake pia walionje.

Picha
alt text
Picha
alt text

Lehi pia aliona fimbo ya chuma iliyoongoza kwenye mti. Watu walishikilia fimbo ili kufika kwenye mti na kula tunda.

Picha
alt text

Mti katika ndoto ya Lehi ni kama vile upendo wa Mungu. Fimbo ni kama maandiko. Tunaposoma maandiko, tunasonga karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.