Rafiki
Kusamehe Kama vile Nefi
Januari 2024


“Kusamehe Kama vile Nefi,” Rafiki, Jan. 2024, 4–5.

Kusamehe Kama vile Nefi

Aisea hakutaka kubaki amemkasirikia Josh siku zote.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Aisea alikimbia na kuupiga mpira kwa Timothy, mwanatimu mwenzake. Alitazama wakati Timothy alipourudisha mguu wake nyuma na kuupiga mpira golini.

“Nimefunga!” Timothy alipiga kelele wakati mpira ulipotikisa nyavu.

Aisea alishangilia. Walikuwa wameshinda mchezo!

Alipotembea kutoka uwanjani, alihisi vizuri! Lakini Josh, mmoja wa watoto wa timu pinzani alimwita kwa jina baya.

Picha
alt text

Aisea alishangaa na ilimuumiza. Hakujua kipi cha kusema. Alitazama chini ardhini na kutembea taratibu kuelekea kwa wanatimu wenzake.

“Tumeweza!” Timothy alisema. “Pasi nzuri, Aisea.”

Lakini Aisea hakuhisi vizuri. Hasa baada ya kile ambacho Josh alimwambia! Alihisi huzuni na hasira.

Muda wote uliosalia, Aisea alihisi kama vile uzito mkubwa ulikuwa ukimvuta chini. Aisea hakumpenda tena Josh.

Usiku ule, Aisea aliketi pamoja na familia yake muda wa maandiko ulipofika. Alijaribu kumsikiliza dada yake akisoma. Lakini hakuacha kufikiria kuhusu kile Josh alichokisema.

Aisea alitazama hapa na pale kwenye kurasa za Kitabu chake cha Mormoni. Alitua kwenye andiko katika 1 Nefi. Ilikuwa wakati ambapo kaka zake Nefi hawakuwa wakarimu kwake.

“Na ikawa kwamba niliwasamehe kwa dhati,” maandiko yalisema.*

Picha
alt text

Nefi aliwasamehe kaka zake? Aisea aliwaza. Hata baada ya wao kuwa wachokozi?

Aisea alimfikiria Josh. Hakutaka kubaki na hisia zake mbaya dhidi ya Josh siku zote. Alikuwa na miaka 10 tu!

Aisea alitaka kuwa kama Nefi. Angeweza kumsamehe Josh, kama vile Nefi alivyowasamehe kaka zake. Na ikiwa Josh angesema kitu kibaya tena, angemwambia asifanye hivyo.

Alipata hisia nzuri na amani moyoni. Ilikuwa kana kwamba Roho Mtakatifu alikuwa akisema, “unafanya jambo sahihi.”

“Aisea, umejifunza kipi kutoka kwenye maandiko haya?” Mama aliuliza.

Aisea alitazama juu. “Samahani, nilikuwa ninasoma andiko tofauti,” alisema. Aliwaambia familia yake kile kilichotokea mpirani.

Mama na Baba walimvuta Aisea na kumkumbatia. “Pole, kwa uchokozi wa Josh,” Baba alisema. “Kile alichokisema hakikuwa cha kweli. Lakini ni SAWA kuhisi kuumizwa nacho.”

Aisea alitabasamu. “Asante. Kwa muda nilikuwa na hasira sana. Lakini sasa kwa vile nimesoma maandiko, sitaki kumkasirikia. Nataka kumsamehe. Na tayari ninahisi vizuri!”

“Hiyo inapendeza sana!” Mama alitabasamu pia. “Kusamehe siku zote si rahisi. Lakini uko sahihi. Ni jambo jema.”

Aisea alitazama kwenye maandiko yake. Yalikuwa yamemsaidia! Uzito wa hapo kabla ulikuwa umetoweka. Badala yake moyo wake ulihisi furaha na amani tele.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Alyssa Tallent