Rafiki
Msukumo wa Chipsi za Viazi Vitamu
Januari 2024


“Kichwa cha Habari cha Msukumo wa Chipsi za Viazi Vitamu,” Rafiki, Jan. 2024, 14–15.

Msukumo wa Chipsi za Viazi Vitamu

Maya alipata hisia zenye nguvu za kuangalia viambato.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Picha
alt text

Maya alikatakata stroberi na kuziongeza kwenye bakuli la saladi ya matunda. Matunda yalikuwa chakula chake pendwa. Alipenda rangi zote zilizong’ara. Na hakupaswa kuwa na wasiwasi kuhusu kuyala!

Maya alikuwa na mizio mingi ya chakula. Alipaswa kuwa makini kwa sababu kula chakula kisichofaa kungemfanya aumwe sana. Alipokuwa mdogo, alikunywa maziwa ya ng’ombe kwa bahati mbaya na alipata tatizo la kupumua. Ilimbidi aende hospitali. Hakutaka hilo litokee tena.

Nyakati zingine ilikuwa vigumu kula vitu tofauti na vile walivyokula marafiki na familia. Lakini alijua hilo ni muhimu kwake ili kubaki salama.

Maya alipeleka saladi ya matunda juu ya meza. “Saladi iko tayari.”

Baba aligeuza macho yake kutoka kwenye chungu alichokuwa akikoroga. “Vizuri! Wageni wetu watakuwa hapa punde tu.”

Maya alisikia hodi mlangoni na akakimbia kufungua. Familia ya Johnson na wamisionari walimpa tabasamu kutokea barazani. Akina Johnson walikuwa marafiki wa familia. Maya alikuwa mwenye furaha kuwaona tena. Alifungua mlango mpaka mwisho kwa ajili ya kila mmoja kuingia ndani.

Wakati wakisubiri chakula cha usiku, mmoja wa wamisionari alimwonesha Maya mchezo. Hakuweza kujua jinsi mmisionari alivyokuwa akivuta sarafu kutoka sikioni kwake!

Punde muda wa kula uliwadia. Kaka Johnson alitoa sala. Kisha wote wakajipanga ili kujaza sahani zao.

Ilipofika zamu ya Maya, alichota kiasi kikubwa cha saladi ya matunda. Aliacha baadhi ya vyakula alivyojua vilikuwa na maziwa ndani yake.

Kisha alichukua mfuko mkubwa wa chipsi na kumimina kiasi kwenye sahani yake. Zilionekana kama aina ya chipsi ambazo amewahi kula kabla. Aliweka moja mdomoni.

Lakini alipoanza kutafuna, alipata hisia yenye nguvu. Angalia viambato, sauti ilisema akilini mwake.

Picha
alt text

Maya aliacha kutafuna. Aliangalia orodha ya viambato kwenye mfuko. Chipsi zilikuwa na maziwa!

Maya alivuta kitambaa cha mezani na kutema chipsi haraka kadiri alivyoweza. Macho yake yalijawa machozi. Hakuwa ameimeza. Lakini je, jambo baya bado lingetokea?

“Mama! Baba!” Maya aliwakimbilia wazazi. “Nimeweka chipsi yenye maziwa mdomoni mwangu!”

“Usihofu,” mama alisema. “Ngoja tuchukue dawa.” Maya alimeza kidonge alichopewa na Mama na kuvuta pumzi ndefu. Baba alimbeba Maya wakati wakisubiri dawa ifanye kazi.

Baada ya dakika chache, Mama alisema, “Unahisi vipi?”

Maya bado alihisi kuogopa. Lakini hakuna kilichoenda kombo kwenye mwili wake. “Nahisi niko SAWA. Lakini je, naweza kupata baraka?”

“Hakika,” Baba alisema. “Ngoja tuwaombe wamisionari wasaidie.”

Picha
alt text

Maya aliketi juu ya kiti, na Baba na wamisionari waliweka mikono yao juu ya kichwa chake. Walimbariki awe salama. Maya alihisi utulivu. Hisia zake mbaya zote zilitoweka.

“Ulijuaje kuangalia viambato kwenye mfuko?” Mama aliuliza.

“Nilihisi onyo kutoka kwa Roho Mtakatifu!”

Baba alimpa kumbatio kubwa. “Nafurahi ulisikiliza.”

Maya alikubali kwa kichwa. Alijua kwamba Baba wa Mbinguni alimpenda na alimjali.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Chrisanne Serafin