Rafiki
Nguvu katika Kitabu cha Mormoni
Januari 2024


“Nguvu katika Kitabu cha Mormoni,” Rafiki, Jan. 2024, 2–3

Kutoka Urais wa Kwanza

Nguvu katika Kitabu cha Mormoni

Imetoholewa kutoka, “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuwaje Bila Hicho?” Liahona, Nov. 2017, 60–63; na “Ushiriki wa Akina Dada katika Kuikusanya Israeli,” Liahona, Nov. 2018, 68–70.

Picha
alt text

Ninapofikiri juu ya Kitabu cha Mormoni, ninafikiria neno nguvu. Kweli za Kitabu cha Mormoni zina nguvu ya kuponya, kufariji, kuimarisha, na kufurahisha nafsi zetu.

Kitabu cha Mormoni ni . . .

  • Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo. Manabii wengi waliokiandika walimwona Yesu Kristo. Kitabu cha Mormoni kinajumuisha shuhuda zao juu Yake.

  • Kumbukumbu ya huduma Yake kwa watu walioishi Amerika ya Kale miaka mingi iliyopita.

  • Cha kweli!

Ninakualika usome Kitabu cha Mormoni. Unaposoma, ninakuhimiza uwekee alama kila mstari unaomzungumzia Mwokozi. Utakuwa karibu Naye zaidi kupitia mchakato huu. Na mabadiliko, hata miujiza, vitaanza kutokea.

Kumtafuta Yesu katika Kitabu cha Mormoni

Picha
alt text

Rais Nelson ametualika tutafute jina la Yesu Kristo wakati tunaposoma Kitabu cha Mormoni. Yesu ana majina mengi katika maandiko. Haya ni baadhi unayoweza kuyatafuta!

Picha
PDF ya hadithi

Kushoto: Mmoja Mmoja na Walter Rane; kulia: kielelezo na Apryl Stott