Maandiko Matakatifu
2 Nefi 1


Kitabu cha Pili cha Nefi

Historia ya kifo cha Lehi. Kaka za Nefi wanamwasi. Bwana anamwonya Nefi akimbilie nyikani. Safari zake nyikani na kadhalika.

Mlango wa 1

Lehi atoa unabii kuhusu nchi ya uhuru—Uzao wake utatawanywa na kuchapwa kama utamkataa yule Mtakatifu wa Israeli—Anawasihi wanawe wajivike mavazi ya silaha ya haki. Karibia mwaka 588–570 K.K.

1 Na ikawa kwamba baada ya mimi, Nefi, kumaliza kufundisha kaka zangu, ababa yetu, Lehi, naye pia aliwaelezea vitu vingi, na akawaambia, jinsi Bwana alivyowafanyia mambo makuu kwa kuwatoa kutoka nchi ya Yerusalemu.

2 Na aliwazungumzia kuhusu amaasi yao majini, na huruma za Mungu katika kuhifadhi maisha yao, kwamba hawakuzama.

3 Na pia aliwaelezea kuhusu nchi ya ahadi, ambayo walipokea—jinsi Bwana alivyokuwa na huruma katika kutuonya kwamba tukimbie kutoka nchi ya Yerusalemu.

4 Kwani, tazama, alisema, nimeona aono, ambalo najua kwamba Yerusalemu imeangamizwa; na kama tungebaki bYerusalemu tungekuwa ctumeangamia pia.

5 Lakini, akasema, ingawa tumepata masumbuko, tumepokea anchi ya ahadi, nchi ambayo ni bbora zaidi ya nchi zingine zote; nchi ambayo Bwana Mungu ameagana na mimi kwamba itakuwa urithi wa uzao wangu. Ndiyo, Bwana cameagana na mimi kuhusu nchi hii, na kwa watoto wangu milele, na pia wale wote ambao watatolewa kutoka nchi zingine kwa mkono wa Bwana.

6 Kwa hivyo, mimi, Lehi, natoa unabii kulingana na mahimizo ya Roho aliye ndani yangu, kwamba hakuna ayeyote atakayekuja katika nchi hii ila tu wale ambao wataletwa na mkono wa Bwana.

7 Kwa hivyo, anchi hii imewekwa wakfu kwa yule atakayeletwa na yeye. Na ikiwa kwamba watamtumikia kulingana na amri ambazo amewapatia, itakuwa nchi ya buhuru kwao; kwa hivyo, hawatatekwa nyara kamwe; au sivyo, itakuwa ni kwa sababu ya uovu; kwani uovu ukiwepo, nchi citalaaniwa kwa sababu yao, lakini kwa wale watakatifu itabarikiwa milele.

8 Na tazama, ni hekima kwamba hii nchi ifichwe kutokana na ufahamu wa mataifa mengine; kwani tazama, mataifa mengi yangeinyakua hii nchi, hata kwamba pasiwe na mahali pa kurithiwa.

9 Kwa hivyo, mimi, Lehi, nimepokea ahadi, kwamba akama wale ambao Bwana Mungu atawatoa kutoka nchi ya Yerusalemu watatii amri zake, bwatafanikiwa katika nchi hii; na watafichwa kutokana na mataifa mengine, ili wapokee nchi hii. Na kama cwatatii amri zake watabarikiwa usoni mwa nchi hii, na hakuna yeyote atakayewaudhi, wala kuwanyangʼanya nchi yao ya urithi; na wataishi salama milele.

10 Lakini tazama, wakati ukitimia watakapofifia katika kutoamini, baada ya kupokea baraka nyingi kutoka mkono wa Bwana—wakiwa na ufahamu wa uumbaji wa dunia, na watu wote, wakielewa kazi kuu na ya maajabu ya Bwana tangu uumbaji wa ulimwengu; na wakipewa nguvu za kutenda vitu vyote kwa imani; wakiwa na amri zote tangu mwanzo, na wakiwa wameletwa kwa wema wake usio na kikomo katika nchi hii ya ahadi—tazama, nasema, kama siku itafika ambapo watamkataa yule Mtakatifu wa Israeli, yule aMasiya wa kweli, Mkombozi wao na Mungu wao, tazama, hukumu za yule mwenye haki zitakuwa juu yao.

11 Ndiyo, atawaletea amataifa mengine, na atayapatia nguvu, na ataondoa kutoka kwao nchi ile ambayo ni mali yao, na atawasababishia bkutawanywa na kupigwa.

12 Ndiyo, wakati kizazi kitakapopita hadi kingine kutakuwa na aumwagaji wa damu, na mapigo makali miongoni mwao; kwa hivyo, wana wangu, ningetaka mkumbuke; ndiyo, ningetaka kwamba msikilize maneno yangu.

13 Ee kwamba ninyi mngezinduka; zindukeni kutoka usingizi mzito, ndiyo, hata kutoka usingizi wa ajehanamu, na mjifungue bminyororo ambayo mmefungiwa, ambayo ni minyororo inayowafunga watoto wa watu, kwamba wanachukuliwa mateka hadi kwenye lile cshimo la milele lenye mateso na huzuni.

14 Zindukeni! na muinuke kutoka mavumbini, na msikie maneno ya amzazi dhaifu, ambaye viungo vyake hivi karibuni lazima mvitie kwenye bkaburi kimya lenye baridi, ambalo hakuna msafiri yeyote anayeweza kurejea kutoka humo; siku chache zimebaki na nitaenda cnjia ya ulimwengu wote.

15 Lakini tazama, Bwana aameikomboa nafsi yangu kutoka jehanamu; nimeuona utukufu wake, na nimezingirwa milele katika bmikono ya cupendo wake.

16 Na ninatamani kwamba mkumbuke kuchunguza asheria na hukumu za Bwana; tazama, huu ndiyo wasiwasi wa nafsi yangu tangu mwanzoni.

17 Moyo wangu umechoshwa na huzuni mara kwa mara, kwani naogopa kwamba kutokana na ugumu wa mioyo yenu Bwana Mungu wenu atawateremkia kwa aghadhabu yake timilifu, hata kwamba bmtengwe na kuangamizwa milele.

18 Au, kwamba laana itawapata kwa muda wa avizazi vingi; na muadhibiwe kwa upanga, na kwa njaa, na mchukiwe, na kuongozwa kulingana na nia na utumwa wa bibilisi.

19 Enyi wana wangu, kwamba vitu hivi visiwajie, lakini kwamba muwe watu awateule na wa kuheshimika na Bwana. Lakini tazama, nia yake itendeke; kwani bnjia zake ni takatifu milele.

20 Na amesema kwamba: aKama mtashika bamri zangu cmtafanikiwa nchini; lakini kama mtakataa amri zangu mtatengwa kutokana na uwepo wangu.

21 Na sasa ili nafsi yangu ifurahi ndani yenu, na ili moyo wangu uondoke ulimwengu huu ukifurahishwa nanyi, kwamba nisishushwe chini kaburini kwa hofu na huzuni, basi, inukeni kutoka mavumbini, wana wangu, na muwe awanaume, na muamue kwa mawazo na kwa moyo bmmoja, mkiungana kwa vitu vyote, ili msiingie utumwani;

22 Ili msilaaniwe kwa laana kali; na pia, ili msijiletee ghadhabu ya Mungu wa ahaki, kwa kuangamizwa, ndiyo, kuangamizwa milele kwa roho na mwili.

23 Zindukeni, wana wangu; jivikeni asilaha za haki. Jifungueni minyororo ambayo imewafunga, na mtoke fumboni, na muinuke kutoka mavumbini.

24 Msimwasi ndugu yenu tena, ambaye maono yake yamekuwa matukufu, na ambaye ametii amri tangu wakati tulipoondoka Yerusalemu; na ambaye amekuwa chombo mikononi mwa Mungu, katika kutuleta hadi kwenye nchi ya ahadi; kwani kama sio yeye, lazima tungeangamia kwa anjaa huko nyikani; walakini, mlitaka bkumtoa uhai wake; ndiyo, na ameteseka kwa hofu nyingi kwa sababu yenu.

25 Na ninaogopa na kutetemeka zaidi kwa sababu yenu, kwamba atateseka tena; kwani tazama, mmemlaumu kwamba alitaka awe na uwezo na mamlaka juu yenu; lakini najua kwamba hakutaka awe na uwezo wala amamlaka juu yenu, lakini alitaka kumtukuza Mungu, na ustawi wenu wa milele.

26 Na mmenungʼunika kwa sababu amekuwa wazi kwenu. Mmesema kwamba ametumia aukali; na mnasema kwamba amewakasirikia; lakini tazama, ukali wake ulikuwa ukali wa nguvu za neno la Mungu, ambalo lilikuwa ndani yake; na lile mnaloliita hasira lilikuwa ukweli, kulingana na ule ulio ndani ya Mungu, ambao hangezuia, akidhihirisha kwa ujasiri kuhusu maovu yenu.

27 Na ni lazima kwamba anguvu za Mungu ziwe na yeye, hata kwamba lazima mtii akiwaamrisha. Lakini tazama, sio yeye, bali ilikuwa bRoho wa Bwana iliyokuwa ndani yake, ambayo cilifungua kinywa chake ili azungumze hata kwamba hangefunga kinywa chake.

28 Na sasa mwana wangu, Lamani, na pia Lemueli na Samu, na pia wana wangu ambao ni wana wa Ishmaeli, tazama, kama mtasikiliza sauti ya Nefi hamtaangamia. Na kama mtamsikiliza nitawaachia abaraka, ndiyo, hata baraka yangu ya kwanza.

29 Lakini ikiwa hamtamsikiza ninaondoa baraka yangu ya akwanza, ndiyo, hata baraka yangu, na itakuwa juu yake.

30 Na sasa, Zoramu, nakuzungumzia wewe: Tazama, wewe ni amtumishi wa Labani; walakini, wewe umetolewa kutoka nchi ya Yerusalemu, na ninajua kwamba wewe ni rafiki wa kweli wa mwana wangu Nefi, milele.

31 Kwa hivyo, kwa vile umekuwa mwaminifu uzao wako utabarikiwa apamoja na mbegu yake, hata kwamba wataishi kwa mafanikio kwa muda mrefu katika nchi hii; na hakuna chochote, ila tu ni uovu miongoni mwao, kitakachowadhulumu au kusumbua mafanikio yao usoni mwa nchi hii milele.

32 Kwa hivyo, kama utatii amri za Bwana, Bwana ameweka nchi hii wakfu kwa usalama wa uzao wako na uzao wa mwana wangu.