Maandiko Matakatifu
2 Nefi 4


Mlango wa 4

Lehi anashauri na kubariki uzao wake—Anafariki na kuzikwa—Nefi anashangilia wema wa Mungu—Nefi anamwamini Bwana milele. Karibia mwaka 588–570 K.K.

1 Na sasa, mimi, Nefi, ninazungumza kuhusu ule unabii ambao baba yangu alitaja, kuhusu aYusufu, ambaye alipelekwa hadi Misri.

2 Kwani tazama, kwa kweli alitoa unabii kuhusu uzao wake wote. Na hakuna aunabii mwingi mkubwa, zaidi ya yale aliyoandika. Na alitoa unabii kutuhusu sisi, na vizazi vyetu vya baadaye; na umeandikwa kwenye mabamba ya shaba nyeupe.

3 Kwa hivyo, baada ya baba yangu kukoma kuzungumza kuhusu unabii wa Yusufu, akaita wana wa Lamani, wanawe, na mabinti zake, na akawaambia: Tazameni, wana wangu, na mabinti zangu, ambao ni wana na mabinti za amzaliwa wa kwanza wangu, ningependa kwamba ninyi msikilize maneno yangu.

4 Kwani Bwana Mungu amesema kwamba: aKadiri mtakavyo tii amri zangu mtafanikiwa nchini; na msipotii amri zangu mtatengwa kutokana na uwepo wangu.

5 Lakini tazameni, wana wangu na mabinti zangu, siwezi kufa kabla sijawapatia abaraka; kwani tazameni, ninajua kwamba kama mtalelewa kulingana na bnjia inayo wapasa hamtaiacha.

6 Kwa hivyo, kama mmelaaniwa, tazameni, ninawaachia baraka yangu, kwamba ile laana iondolewe kwenu na iwe ajuu ya wazazi wenu.

7 Kwa hivyo, kwa sababu ya baraka yangu Bwana Mungu ahatakubali kwamba mwangamie; kwa hivyo, batawarehemu ninyi na uzao wenu milele.

8 Na ikawa kwamba baada ya baba yangu kumaliza kuzungumzia wana na mabinti za Lamani, alisababisha wana na mabinti za Lemueli kusimama mbele yake.

9 Na akawazungumzia, akisema: Tazama, wana wangu na mabinti zangu, ambao ni wana na mabinti za mwana wangu wa pili; tazama ninawapatia baraka kama ile ambayo niliwapatia wana na mabinti za Lamani; kwa hivyo, ninyi hamtaangamizwa kabisa; lakini uzao wenu utabarikiwa mwishowe.

10 Na ikawa kwamba baada ya baba yangu kukoma kuwazungumzia, tazama, aliwazungumzia wana wa aIshmaeli, ndiyo, na hata nyumba yake yote.

11 Na baada ya kukoma kuwazungumzia, alimwambia Samu, akisema: Heri wewe, na uzao wako; kwani wewe utarithi nchi kama vile kaka yako Nefi. Na uzao wako utahesabiwa na uzao wake; na wewe utakuwa kama kaka yako, na uzao wako kama uzao wake; na wewe utabarikiwa katika siku zako zote.

12 Na ikawa kwamba baada ya baba yangu, Lehi, kumaliza kuzungumzia jamaa yake yote, kulingana na mawazo ya moyo wake na Roho wa Bwana ambaye alikuwa ndani yake, akawa mzee. Na ikawa kwamba alifariki, na akazikwa.

13 Na ikawa kwamba muda mfupi baada ya kifo chake, Lamani na Lemueli pamoja na wana wa Ishmaeli walinikasirikia kwa sababu walirudiwa na Bwana.

14 Kwani mimi, Nefi, nilishurutishwa kuwazungumzia, kulingana na neno lake; kwani nilikuwa nimewazungumzia vitu vingi, na pia baba yangu, kabla ya kifo chake; maneno mengi ambayo yameandikwa kwenye amabamba yangu mengine; kwani sehemu kubwa zaidi ya historia imeandikwa kwenye mabamba yangu mengine.

15 Na katika ahaya ninaandika mambo ya nafsi yangu, na maandiko mengi ambayo yamechorwa kwenye mabamba ya shaba nyeupe. Kwani moyo wangu unayafurahia maandiko, na moyo wangu bhuyatafakari, na kuyaandika kwa cajili ya kujifunza na faida ya watoto wangu.

16 Tazama, anafsi yangu hufurahia vitu vya Bwana; na bmoyo wangu huyatafakari mara kwa mara vitu ambavyo nimeviona na kuvisikia.

17 Walakini, ingawa Bwana ana awema mkubwa, hata kunionyesha kazi yake kuu na ya maajabu, moyo wangu unalia: Ewe mimi mtu bmwovu! Ndiyo, moyo wangu unahuzunishwa kwa sababu ya mwili wangu; moyo wangu unahofishwa na dhambi zangu.

18 Nimezingirwa, kwa sababu ya majaribio na dhambi ambazo azinaninasa kwa urahisi.

19 Na ninapotaka kushangilia, moyo wangu huugua kwa sababu ya dhambi zangu; walakini, ninajua ninayemwamini.

20 Mungu wangu amekuwa tegemeo langu; ameniongoza katika masumbuko yangu nyikani; na amenihifadhi hata kutoka kilindi kikuu cha maji.

21 Amenijaza aupendo wake, hata kwa kumaliza mwili wangu.

22 Amewafadhaisha amaadui wangu, hata kuwasababisha kutetemeka mbele yangu.

23 Tazama, amesikia kilio changu mchana, na kunipatia ufahamu usiku kwa amaono.

24 Na kwa mchana animesali kwa ujasiri; ndiyo, nimepaza sauti yangu juu; na malaika wakateremka na kunihudumia.

25 Na kwenye mabawa ya Roho yake mwili wangu aumebebwa na kuchukuliwa kwenye milima mirefu zaidi. Na macho yangu yameona vitu vikuu, ndiyo, hata vikuu sana kwa mwanadamu; kwa hivyo niliamriwa kwamba nisiviandike.

26 Ee basi, kama nimeona mambo makuu hivi, kama Bwana katika ufadhili wake kwa watoto wa watu amewafariji wanadamu kwa huruma kuu hivi, akwa nini moyo wangu ulie na nafsi yangu kusita katika bonde la hofu, na mwili wangu kuwa mnyonge, na nguvu zangu kufifia, kwa sababu ya masumbuko yangu?

27 Na kwa nini anitumikie dhambi, kwa sababu ya mwili wangu? Ndiyo, kwa nini niyakubali bmajaribio, hata kwamba yule mwovu apate nafasi moyoni mwangu ya kuangamiza camani na kusumbua nafsi yangu? Kwa nini nikasirishwe na adui yangu?

28 Amka, nafsi yangu! Usilemewe na dhambi tena. Shangilia, Ewe moyo wangu, na usimpatie aadui wa nafsi yangu mahali.

29 Usikasirike tena kwa sababu ya maadui zangu. Usipungukiwe na nguvu kwa sababu ya masumbuko yangu.

30 Shangilia, Ewe moyo wangu, na umlilie Bwana, na kusema: Ewe Bwana, nitakusifu milele; ndiyo, nafsi yangu itashangilia ndani yako, Mungu wangu, na amwamba wa wokovu wangu.

31 Ewe Bwana, je, utaikomboa nafsi yangu? Je, utaniopoa kutoka mikononi mwa maadui zangu? Je, utanifanya kwamba nitetemeke nikiona adhambi?

32 Na milango ya jehanamu ifungwe mbele yangu daima, kwa sababu amoyo wangu umevunjika na nafsi yangu imepondeka! Ewe Bwana, je, usiifunge milango ya haki yako mbele yangu, ili bnitembee katika mapito ya bonde iliyo chini, hata niwe mkali kwenye njia iliyo wazi!

33 Ewe Bwana, je, utanizingira na joho la haki yako! Ewe Bwana, je, utanitayarishia njia ya kutorokea maadui wangu! Je, utaninyooshea mapito yangu! Je, utaniwekea kikwazo kwa njia yangu—lakini kwamba unifanyie njia zangu ziwe wazi, na usizibe njia yangu, lakini njia za adui yangu.

34 Ewe Bwana, nimekuamini, na anitakuamini milele. Sitaweka btumaini langu kwenye mkono wa mwanadamu; kwani ninajua amelaaniwa yule anayeweka ctumaini lake kwa mkono wa mwanadamu. Ndiyo, amelaaniwa yule anayeweka tumaini lake kwa mwanadamu au amfanyaye kuwa mkono wake.

35 Ndiyo, ninajua kwamba Mungu humsaidia anayeomba bila akizuizi. Ndiyo, Mungu wangu atanipatia, bnikiomba cbila kasoro; kwa hivyo nitakupazia sauti yangu; ndiyo, nitakulilia, Mungu wangu, mwamba wa haki yangu. Tazama, nitakupazia sauti yangu milele, dmwamba wangu na Mungu wangu asiye na mwisho. Amina.