Maandiko Matakatifu
2 Nefi 8


Mlango wa 8

Yakobo anaendelea kusoma kutoka katika Isaya: Katika siku za mwisho, Bwana ataifariji Sayuni na kukusanya Israeli—Waliokombolewa watakuja Sayuni kwa shangwe kuu—Linganisha Isaya 51 na 52:1–2. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Nisikizeni mimi, ninyi ambao mnatafuta haki. Tazameni amwamba kutoka ambapo mlichongwa, na kwenye shimo mlikotolewa.

2 Tazameni Ibrahimu, ababa yenu, na bSara, aliyewazaa; kwani nimemwita pekee, na kumbariki.

3 Kwani Bwana atafariji aSayuni, atafariji sehemu zake zote zenye ukiwa; na atasababisha bnyika yake kuwa kama Edeni, na jangwa lake kama bustani ya Bwana. Shangwe na furaha itakuwa ndani yake, pia na shukrani na sauti ya uimbaji.

4 Nisikilizeni, watu wangu; na mnipe sikio, Ee taifa langu; kwani asheria itatoka kwangu, na nitafanya hukumu zangu kubaki kama bmwangaza kwa watu.

5 Utakatifu yangu iko karibu; awokovu wangu umesonga mbele, na mkono wangu utahukumu watu. bVisiwa vitaningoja, na watauamini mkono wangu.

6 Elekezeni macho yenu mbinguni, na mtazame huko chini duniani; kwani ambingu bzitatoweka kama moshi, na dunia citazeeka kama vazi; na wale wanaoishi ndani yake watakufa vivyo hivyo. Lakini wokovu wangu utakuwa milele, na haki yangu haitaondolewa.

7 Nisikilizeni mimi, ninyi ambao mnajua haki, wale watu ambao nimeandika sheria yangu moyoni mwao, amsiogope mzaha wa wanadamu, wala msiogope matusi yao.

8 Kwani nondo atawala kama vazi, na mchango kuwala kama manyoya. Lakini haki yangu itakuwa milele, na wokovu wangu utakuwa kutoka kizazi hadi kizazi.

9 Inuka, inuka! Vaa anguvu, Ee mkono wa Bwana; inuka kama katika siku za kale. Kwani wewe sio yule aliyemchinja Rahabu, na kuumiza joka?

10 Kwani wewe sio yule ambaye amekausha bahari, maji ya kilindi kikuu; ambaye amesababisha kilindi cha bahari kuwa anjia ya wale waliokombolewa kupitia?

11 Kwa hivyo, wale awaliokombolewa na Bwana watarejea, na kuja Sayuni bwakiimba; na shangwe isiyo na mwisho na utakatifu itakuwa juu ya vichwa vyao, na watapokea furaha na shangwe; huzuni na ckuomboleza zitatoweka.

12 aMimi ndimi; ndiyo, mimi ndimi yule anayekufariji. Tazama, wewe ni nani, kwamba bumwogope mwanadamu, atakayekufa, na mwanadamu, ambaye atafanywa kuwa kama cnyasi?

13 Na akumsahau Bwana muumba wako, ambaye ametandaza mbingu, na kujenga msingi wa dunia, na ameendelea kuogopa kila siku, kwa sababu ya hasira ya mdhalimu, kama aliye tayari kukuangamiza? Na hasira ya mdhalimu iko wapi?

14 Mateka mkimbizi anaharakisha, ili afunguliwe, na kwamba asife shimoni, wala kwamba asikose mkate wake.

15 Lakini mimi ni Bwana Mungu wako, ambaye amawimbi yake yalizuka; Bwana wa Majeshi ni jina langu.

16 Na nimeweka maneno yangu kinywani mwako, na kukuficha katika kivuli cha mkono wangu, ili nipande mbingu na kujenga msingi wa dunia, na kuambia Sayuni: Tazama, ninyi ni awatu wangu.

17 Inuka, inuka, simama wima, Ee Yerusalemu, ambaye amekunywa kutoka mkono wa Bwana akikombe cha bhasira yake—umekunywa mabaki ya kikombe cha kuogopesha—

18 Na hakuna yeyote miongoni mwa wanawe wote aliozaa anayeweza kumwongoza; wala yule anayemchukua kwa mkono wake, miongoni mwa wana wale wote aliolea.

19 Hawa awana wawili wamekujia, ambao watakuhurumia—ukiwa na uangamizo wako, na njaa na upanga—na ni kwa kupitia nani nitakayekufariji?

20 Wana wako wamezimia, ila tu hawa wawili; wanangoja kwenye njia zote; kama ndume wa kichakani kwenye wavu, wamejaa hasira ya Bwana, kemeo la Mungu wako.

21 Kwa hivyo sikiliza haya sasa, wewe uliyesumbuka, na akulewa, na sio kwa mvinyo:

22 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana wako, Bwana na Mungu wako aanatetea maslahi ya watu wake; tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kuogopesha, mabaki ya kikombe cha hasira yangu; wewe hutakinywa tena.

23 Lakini aMimi nitakiweka mkononi mwa wale wanaokusumbua; wale ambao wameiambia nafsi yako: Inama chini, ili tupite juu—na wewe umelaza mwili wako chini na ukawa kama njia kwa wale waliopita.

24 aInuka, inuka, vaa bnguvu zako, Ee cSayuni; vaa mavazi yako maridadi, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; kwani tangu sasa wasiotahiriwa na walio wachafu dhawatakuingia.

25 Jitingishe kutoka mavumbini; ainuka, kaa chini, Ee Yerusalemu; jifungue kutokana na bvifungo vya shingo lako, Ee binti mateka wa Sayuni.