Maandiko Matakatifu
2 Nefi 22


Mlango wa 22

Katika siku ile ya milenia watu wote watamsifu Bwana—Ataishi miongoni mwao—Linganisha Isaya 12. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Na katika siku ile utasema: Ee Bwana, nitakusifu; ingawa ulinikasirikia hasira yako imegeuka, na unanifariji.

2 Tazama, Mungu ni wokovu wangu; anitatumaini, na wala sitaogopa; kwani Bwana bYehova ndiye nguvu yangu na wimbo wangu; pia amekuwa wokovu wangu.

3 Kwa hivyo, kwa shangwe utateka amaji kutoka visima vya wokovu.

4 Na katika siku ile utasema: aMsifuni Bwana, liiteni jina lake, tangazeni matendo yake miongoni mwa watu, taja jina lake ili liinuliwe.

5 aMwimbieni Bwana; kwani ametenda vitu vyema; haya yanajulikana ulimwenguni kote.

6 Pazeni sauti na amlie, ewe mkazi wa Sayuni; kwani mkuu ni yule Mtakatifu wa Israeli aliye baina yenu.