Maandiko Matakatifu
2 Nefi 18


Mlango wa 18

Kristo atakuwa kama jiwe la kujikwaa na mwamba wa kuchukiza—Mtafute Bwana, sio mlio wa wachawi—Tegemea sheria na ushuhuda kwa maongozo—Linganisha Isaya 8. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Tena, neno la Bwana liliniambia: Chukua hati ndefu, na uandike juu yake kwa kalamu ya mwanadamu, kuhusu aMaher-shalal-hash-bazi.

2 Na nilichukua amashahidi waaminifu ili waandike, Uria yule kuhani, na Zekaria mwana wa Yeberekia.

3 Na nilimwendea huyo anabii wa kike; na akapata mimba na akazaa mwana wa kiume. Kisha Bwana akaniambia: Muite jina lake, Maher-shalal-hash-bazi.

4 Kwani tazama, kabla ya huyo amtoto bhajajua kulia, baba yangu, na mama yangu, utajiri wa Dameski na cmateka ya Samaria yatachukuliwa na mfalme wa Ashuru.

5 Bwana alinizungumzia tena, akisema:

6 Kwa vile watu hawa wameyakataa maji ya aShiloa yapitayo polepole, na wanafurahia bResini na mwana wa Remalia;

7 Kwa hivyo sasa, tazama, Bwana ataleta ajuu yao maji ya huo mto, yenye nguvu, na mengi, hata mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; atakuja na kupita juu ya mifereji yake yote, na kingo zake zote.

8 Na ayeye atapita Yuda; atafurika na kuwa zaidi, atafika hata shingoni; na atakaponyosha mabawa yake yatajaa upana wa nchi, Ewe bImanueli.

9 aJiunganishe, Ee ninyi watu, na mtavunjwa vipande vipande; na sikiliza ninyi nyote mtokao nchi za mbali; jiwekeni tayari na silaha, na mtavunjwa vipande vipande; jiwekeni tayari na silaha, na mtavunjwa vipande vipande.

10 Fanyeni shauri pamoja, na hamtafanikiwa; nena neno, na halitatimia; akwani Mungu yu pamoja nasi.

11 Kwani Bwana alinizungumzia hivyo kwa kunionya vikali, na akanishauri kuwa nisitembee katika njia za watu hawa, akisema:

12 Msiseme, aMuungano, kwa wale wote ambao hawa watu watasema, Muungano; wala msiogope woga wao, wala kuogopa.

13 Mtakaseni Bwana wa Majeshi mwenyewe, na aacheni yeye awe hofu yenu, na acheni yeye awe tisho lenu.

14 Na atakuwa akimbilio; lakini bjiwe la kujikwaa, na mwamba wa kuchukiza kwa nyumba zote mbili za Israeli, na mtego na tanzi kwa wakazi wa Yerusalemu.

15 Na wengi miongoni mwao awatajikwaa na kuanguka, na kuvunjwa, na kutegwa, na kukamatwa.

16 Ufunge huo ushuhuda, na ufunge asheria miongoni mwa wanafunzi wangu.

17 Na nitamngojea Bwana, ambaye ahuficha uso wake kutoka kwa nyumba ya Yakobo, na nitamtafuta.

18 Tazama, mimi na watoto ambao Bwana amenipatia ni kwa aishara na maajabu katika Israeli kutoka kwa Bwana wa Majeshi, yule anayekaa katika Mlima Sayuni.

19 Na watakapokuambia: Tafuta ushauri kwa watu wenye apepo wa utambuzi, na kwa bwachawi wanaochungulia na kunongʼona—je, haiwapasi watu kutafuta ushauri ckutoka kwa Mungu ili wanaoishi wasikie dkutoka kwa wafu?

20 Kwa sheria na kwa ushuhuda; na awao wasiponena kulingana na neno hili, ni kwa sababu hakuna nuru ndani yao.

21 Nao awao watapita katikati yake wamedhikika na wakiwa na njaa; na itakuwa kwamba watakapopata njaa, watajikasirisha wenyewe, na kumlaani mfalme wao na Mungu wao na kutazama juu.

22 Na watatazama ardhi na kutazama shida, na giza, kufa moyo, na wataingizwa gizani.