Maandiko Matakatifu
2 Nefi 6


Mlango wa 6

Yakobo aeleza historia ya Wayahudi: Uhamisho wa Kibabilonia na marejeo; huduma na kusulubiwa kwa yule Mtakatifu wa Israeli; msaada uliopokelewa kutokana na Wayunani; na uamsho wa siku za mwisho kwa Wayahudi watakapomwamini Masiya. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Maneno ya Yakobo, kaka yake Nefi, ambayo aliwazungumzia watu wa Nefi:

2 Tazameni, ndugu zangu wapendwa, mimi, Yakobo, nikiwa nimeitwa na Mungu, na kutawazwa wake mtakatifu, na nikiwa nimetawazwa na kaka yangu Nefi, ambaye mnamtegemea kama amfalme au mlinzi, na ambaye pia mnamtegemea kwa usalama, tazameni mnajua kwamba nimewazungumzia vitu vingi zaidi.

3 Walakini, nawazungumzia tena; kwani ninajali ustawi wa nafsi zenu. Ndiyo, wasiwasi wangu ni mkubwa kwenu; na ninyi mnajua imekuwa hivyo tangu mwanzo. Kwani nimewashauri kwa bidii zote; na nimewafundisha maneno ya baba yangu; na nimewazungumzia ninyi kuhusu vitu vyote vilivyoandikwa, tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

4 Na sasa, tazameni, ningewazungumzia kuhusu vitu vilivyo, na vile vitakavyokuja; kwa hivyo, nitawasomea maneno ya aIsaya. Na ni maneno yale ambayo kaka yangu anataka niwasomee. Na ninawazungumzia kwa manufaa yenu, ili mjifunze na kulitukuza jina la Mungu wenu.

5 Na sasa, maneno ambayo nitasoma ni yale ambayo Isaya alizungumza kuhusu nyumba yote ya Israeli; kwa hivyo, yanaweza kulinganishwa nanyi, kwani ninyi ni wa nyumba ya Israeli. Na kuna vitu vingi ambavyo vimezungumzwa na Isaya ambavyo vinaweza kulinganishwa nanyi, kwa sababu ninyi ni wa nyumba ya Israeli.

6 Na sasa, haya ndiyo maneno: aHivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu: Tazama, nitawainulia Wayunani mkono wangu, na kuwapeperushia watu bbendera yangu; na watawaleta wana wenu mikononi mwao, na kuwabeba mabinti zenu mabegani mwao.

7 Na wafalme watakuwa baba walezi wenu, na malkia wao watakuwa mama walezi wenu; watainamisha nyuso zao mbele zenu zikielekea udongoni, na kuramba mavumbi ya miguu yenu; nanyi mtajua kwamba Mimi ni Bwana; kwani wale awanaonisubiri hawataaibika.

8 Na sasa mimi, Yakobo, nitazungumza kuhusu maneno haya. Kwani tazama, Bwana amenionyesha kwamba wale waliokuwa aYerusalemu, kule tulipotoka, wameuawa na bkupelekwa utumwani.

9 Walakini, Bwana amenionyesha kwamba awatarejea tena. Na pia amenionyesha kwamba Bwana Mungu, aliye Mtakatifu wa Israeli, atajidhihirisha kwao katika mwili; na baada ya kujidhihirisha watampiga na bkumsulubu, kulingana na maneno ya malaika aliyenizungumzia.

10 Na baada ya wao kushupaza mioyo yao na kukaza shingo zao kwa yule Mtakatifu wa Israeli, tazama ahukumu za yule aliye Mtakatifu wa Israeli zitawateremkia. Na siku inakuja kwamba watachapwa na kusumbuliwa.

11 Kwa hivyo, baada ya wao kufukuzwa hapa na pale, kwani hivyo ndivyo asemavyo malaika, wengi watasumbuka sana mwilini, na hawatakubaliwa kuangamia, kwa sababu ya sala za walio waaminifu; watatawanywa, na kupigwa, na kuchukiwa; walakini, Bwana atawarehemu, kwamba awakati bwatakapomfahamu Mkombozi wao, cwatakusanywa pamoja tena katika nchi yao ya urithi.

12 Na heri aWayunani, wale ambao nabii ameandika juu yao; kwani tazama, kama watatubu na hawapigani na Sayuni, na wasijiunge na lile kanisa kuu la bmachukizo, wataokolewa; kwani Bwana Mungu atatimiza cmaagano yake aliyoagana na watoto wake; na ni kwa sababu hii nabii ameandika maneno haya.

13 Kwa hivyo, wale wanaopigana dhidi ya Sayuni na watu wa agano la Bwana wataramba mavumbi ya miguu yao; na watu wa Bwana ahawataaibika. Kwani watu wa Bwana ni wale bwanaomsubiri; kwani bado wanangoja kuja kwa Masiya.

14 Na tazama, kulingana na maneno ya nabii, Masiya ataanza tena kwa mara ya apili kuwakomboa; kwa hivyo, batajidhihirisha kwao kwa uwezo na utukufu mkuu, kwa ckuangamiza maadui wao, wakati siku ile itakapofika ambapo watamwamini; na hatamuangamiza yeyote yule atakayemwamini.

15 Na wale wasiomwamini yeye awataangamizwa, kwa bmoto, na kwa dhoruba, na kwa matetemeko ya ardhi, na kwa vita, na kwa ctauni, na kwa njaa. Na watajua kwamba Bwana ni Mungu, yule Mtakatifu wa Israeli.

16 aKwani mawindo yatanyangʼanywa kutoka wale wenye nguvu, au bmateka halali kukombolewa?

17 Lakini Bwana asema hivi: Hata amateka wa shujaa watanyakuliwa, na mawindo ya waovu kukombolewa; kwani bMwenyezi Mungu catawakomboa watu wake wa agano. Kwani hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Nitashindana na wale wanaoshindana nawe—

18 Na nitawalisha wale wanaowadhulumu, kwa miili yao wenyewe; na watalewa kwa damu yao wenyewe kama vile kwa mvinyo mtamu; na miili yote itafahamu kwamba mimi Bwana ndiye Mwokozi wako na aMkombozi wako, yule bMwenye Enzi wa Yakobo.