Maandiko Matakatifu
2 Nefi 17


Mlango wa 17

Efraimu na Shamu wanashambulia Yuda—Kristo atazaliwa na Bikira—Linganisha Isaya 7. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Na ikawa katika siku za Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, kwamba Resini, mfalme wa Shamu, na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, walienda kushambulia Yerusalemu, lakini hawakuiweza.

2 Na nyumba ya Daudi, ikaambiwa: Shamu imeungana na aEfraimu. Na moyo wake ukatetemeka, na moyo wa watu wake, jinsi vile miti ya kichaka hupeperushwa na upepo.

3 Kisha Bwana akamwambia Isaya: Nenda sasa ukamlaki Ahazi, wewe na mwana wako aShear-yashubu, huko mwisho wa mfereji wa dimbwi la juu katika njia kuu ya uwanja wa dobi;

4 Na umwambie: Sikiliza, na utulie; ausiogope, wala usifadhaike moyoni kwa sababu ya hii mikia miwili ya mwenge itokayo moshi, kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na ya mwana wa Remalia.

5 Kwa sababu Shamu, Efraimu, na mwana wa Remalia, wamekusudia maovu juu yako, wakisema:

6 Hebu twende dhidi ya Yuda na kuichokoza, na tuigawanye kati yetu, na tuweke mfalme kati yake, ndiyo, mwana wa Tabeeli.

7 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu: Haitasimama, wala kutimika.

8 Kwani kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski, Resini; na katika muda wa miaka sitini na tano Efraimu itaangamizwa isiwe tena kikundi cha watu.

9 Na kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Kama ahamtaamini kwa hakika hamtaimarishwa.

10 Tena, Bwana akazungumza zaidi na Ahazi, akamwambia:

11 Itisha aishara kutoka kwa Bwana Mungu wako; iwe chini kwenye shimo, au juu kwenye mawingu.

12 Lakini Ahazi akasema: Sitaitisha, wala asitamjaribu Bwana.

13 Na akasema: Sikilizeni sasa, Enyi nyumba ya Daudi; Je, ni kitu kidogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?

14 Kwa hivyo, Bwana mwenyewe atakupatia ishara—Tazama, aBikira atapata mimba, na atazaa mwanamume, na atamwita kwa jina bImanueli.

15 Atakula siagi na asali, ili ajue kukataa maovu na kuchagua mema.

16 Kwani kabla huyo amtoto hajajua kukataa maovu na kuchagua mema, nchi ile ambayo unaichukia itakataliwa na wafalme wake bwawili.

17 Bwana aatakuteremshia, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, nyakati ambazo hazijawahi kuoneka tangu siku ile bEfraimu alipoondoka kutoka Yuda, mfalme wa Ashuru.

18 Na itakuwa kwamba katika siku ile Bwana ataipigia amiunzi nzi aliye sehemu za mbali za Misri, na kwa nyuki aliye katika nchi ya Ashuru.

19 Na watakuja, na watapumzika wote katika mabonde yaliyo na ukiwa, na katika mashimo ya miamba, na kwenye miiba yote, na juu ya vichaka vyote.

20 Na siku ile ile Bwana aatawanyoa kwa wembe ulioajiriwa, na hao ngʼambo ya mto, na bmfalme wa Ashuru, kichwa, na malaika wa miguu; na pia atamaliza ndevu.

21 Na itakuwa kwamba katika siku ile, mtu aatalisha ngʼombe mmoja na kondoo wawili;

22 Na itakuwa kwamba, kwa wingi wa maziwa watakayotoa atakula siagi; kwani kila mmoja aliyesalia katika nchi ile atakula siagi na asali.

23 Na itakuwa kwamba katika siku ile, kila mahali patakuwa, ambapo palikuwa mizabibu elfu inayo gharama afedha elfu, ambapo patakuwa na mbigili na miiba.

24 Na watu wataenda huko na mishale na pinde, kwa sababu nchi yote itakuwa mbigili na miiba.

25 Na vilima vyote vitakavyolimwa kwa jembe, hapatafika huko woga wa mbigili na miiba; lakini hapo patakuwa mahali pa kuelekeza ngʼombe, na mahali pa kukanyagwa na akondoo.