Maandiko Matakatifu
1 Nefi 22


Mlango wa 22

Israeli itatawanyika kote usoni mwa ulimwengu—Wayunani watalea na kulisha Israeli kwa injili katika siku za mwisho—Israeli itakusanywa na kuokolewa, na waovu wataungua kama kapi—Ufalme wa ibilisi utaangamizwa, na Shetani atafungwa. Karibia mwaka 588–570 K.K.

1 Na sasa ikawa kwamba baada ya mimi, Nefi, kuvisoma vitu hivi vilivyochorwa kwenye amabamba ya shaba nyeupe, kaka zangu walinijia na kuniambia: Nini maana ya vitu hivi ambavyo umevisoma? Tazama, je, vitaeleweka kulingana na vitu vya kiroho, ambavyo vitatimizwa kulingana na roho na sio mwili?

2 Na mimi, Nefi, niliwaambia: Tazama avilidhirihishwa kwa nabii kwa sauti ya bRoho; kwani kwa Roho vitu vyote vinafunuliwa kwa cmanabii, ambavyo vitawajia watoto wa watu kulingana na mwili.

3 Kwa hivyo, vitu ambavyo nimesoma ni vitu vinavyolingana na vitu vya amuda na vya kiroho; kwani inaonekana kwamba nyumba ya Israeli, sasa au baadaye, bitatawanyika usoni mwote mwa dunia, na pia miongoni mwa mataifa yote.

4 Na tazama, tayari kuna wengi ambao wamepotea kutokana na ufahamu wa wale ambao walioko Yerusalemu. Ndiyo, sehemu kubwa ya amakabila yote byamepotoshwa; na yametawanyika hapa na pale katika cvisiwa vya bahari; na pale yalipo hakuna yeyote baina yetu ajuaye, ila tunajua kwamba yamepotoshwa.

5 Na kwa vile wamepotoshwa, vitu hivi vimetabiriwa juu yao, na pia kuhusu wale wote ambao watatawanywa baadaye na kuchanganyika, kwa sababu ya yule Mtakatifu wa Israeli; kwani watashupaza mioyo yao dhidi yake; kwa hivyo, watatawanywa miongoni mwa mataifa yote na awatachukiwa na watu wote.

6 Walakini, baada ya wao akulelewa na bWayunani, na Bwana kunyoshea Wayunani mkono wake na kuwainua kama bendera, na cwatoto wao wamebebwa mikononi mwao, na mabinti zao wamebebwa mabegani mwao, tazama vitu hivi ambavyo vimezungumziwa ni vya muda; kwani hayo ndiyo maagano ya Bwana na baba zetu; na inatuhusu katika siku zijazo, na pia kaka zetu wote ambao ni wa nyumba ya Israeli.

7 Na inamaanisha kwamba wakati unafika kwamba baada ya nyumba yote ya Israeli kutawanywa na kuchanganywa, kwamba Bwana Mungu atainua taifa shupavu miongoni mwa aWayunani, ndiyo, hata usoni mwa nchi hii; na kwa wao uzao wetu butatawanywa.

8 Na baada ya uzao wetu kutawanywa Bwana Mungu ataanza kutenda kazi ya amaajabu miongoni mwa bWayunani, ambayo itakuwa ya cthamani kubwa kwa uzao wetu; kwa hivyo, unalinganishwa na wao wakilishwa na Wayunani na wakibebwa mikononi mwao na mabegani mwao.

9 Na pia itakuwa yenye athamani kwa Wayunani; na sio tu kwa Wayunani lakini bkwa cnyumba yote ya Israeli, kwa kujulisha dmaagano ya Baba wa Mbingu kwa Ibrahimu, akisema: Katika euzao wako makabila yote ya dunia fyatabarikiwa.

10 Na ningetaka, kaka zangu, kwamba mngejua kwamba makabila yote ya dunia hayawezi kubarikiwa isipokuwa aweke mkono wake awazi machoni mwa mataifa.

11 Kwa hivyo, Bwana Mungu ataendelea kuweka mkono wake wazi machoni mwa mataifa yote, katika kutimiza maagano yake na injili yake kwa wale ambao ni wa nyumba ya Israeli.

12 Kwa hivyo, atawatoa tena utumwani, na awatakusanyika pamoja katika nchi yao ya urithi; na watatolewa kutoka fumboni na kutoka bgizani; na watajua kwamba cBwana ni dMwokozi wao na Mkombozi wao, eMwenyezi Mkuu wa Israeli.

13 Na damu ya lile kanisa kuu na la amachukizo, ambalo ni kahaba wa ulimwengu wote, itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe; kwani bwatapigana wenyewe kwa wenyewe, na upanga wa mikono cyao utaangukia vichwa vyao vyenyewe, na watalewa kwa damu yao wenyewe.

14 Na kila ataifa ambalo litapigana nawe, Ee nyumba ya Israeli, watageukiana mmoja dhidi ya mwingine, na bwataanguka kwenye shimo walilochimba kutega watu wa Bwana. Na wote cwatakaopigana dhidi ya Sayuni wataangamizwa, na yule kahaba mkuu, ambaye ameharibu njia sahihi za Bwana, ndiyo, lile kanisa kuu la machukizo, litaanguka dmavumbini na muanguko wake utakuwa mkuu.

15 Kwani tazama, asema nabii, wakati unafika kwa haraka kwamba Shetani hatakuwa na nguvu yoyote mioyoni mwa watoto wa watu; maana siku inafika kwamba wote wenye kiburi na wale wanaotenda maovu watakuwa kama akapi; na siku inafika ambayo lazima bwachomwe.

16 Kwani wakati unafika mapema ambapo utimilifu wa aghadhabu ya Mungu utakuwa juu ya watoto wa watu wote; kwani hatakubali kwamba waovu wawaangamize walio watakatifu.

17 Kwa hivyo, aatawahifadhi walio wa bhaki kwa nguvu zake, hata kama ghadhabu yake timilifu ije, na watakatifu wahifadhiwe, hata katika maangamizo ya maadui wao kwa moto. Kwa hivyo, watakatifu hawapaswi kuogopa; na hivyo ndivyo asemavyo nabii, wataokolewa, hata kama ni kwa moto.

18 Tazama, kaka zangu, nawaambia, kwamba vitu hivi lazima vitimizwe karibuni; ndiyo, hata damu, na moto, na ukungu wa moshi lazima uje; na ni lazima itendeke usoni mwa dunia hii; na inawajia binadamu kulingana na mwili ikiwa watashupaza mioyo yao dhidi ya yule Mtakatifu wa Israeli.

19 Kwani tazama, watakatifu hawataangamia; kwani wakati lazima kwa hakika ufike kuwa wale ambao wanapinga Sayuni wataondolewa mbali.

20 Na Bwana kwa kweli atawatayarishia watu wake njia, kwa kutimiza maneno ya Musa, ambayo alizungumza, akisema: Bwana Mungu wenu atawainulia nabii, kama mimi, yeye mtamsikiliza kwa vitu vyote atakavyowaambia. Na itakuwa kwamba wale wote ambao hawatamsikiliza anabii bwataondolewa kutoka miongoni mwa watu.

21 Na sasa mimi, Nefi, ninawatangazia, kwamba huyu anabii aliyetajwa na Musa ni yule Mtakatifu wa Israeli; kwa hivyo, atapitisha bhukumu kwa haki.

22 Na watakatifu hawapaswi kuogopa, kwani wao hawatachanganyika. Lakini ni ufalme wa ibilisi, ambao utajengwa miongoni mwa watoto wa watu, ambao ni ufalme ulioimarishwa miongoni mwa wale wanaoishi—

23 Kwani kwa haraka wakati utafika ambapo amakanisa yote ambayo yamejengwa ili kupata faida, na wote waliojengwa kwa kupata mamlaka juu ya mwili, na wale ambao walijengwa ili wapate bsifa machoni mwa ulimwengu, na wale wanaotafuta tamaa za mwili na vitu vya ulimwengu, na kutenda kila aina ya uovu; ndiyo, mwishowe, wale wote ambao ni wa ufalme wa ibilisi ndiyo wanapaswa kuogopa, na kutetemeka, na ckutapatapa; wao ndiyo lazima washushwe chini mavumbini; wao ndiyo lazima dwatachomwa kama kapi; na haya ni kulingana na maneno ya nabii.

24 Na wakati unafika kwa haraka kwamba wale watakatifu lazima waongozwe kama andama wa zizini, na yule Mtakatifu wa Israeli lazima atawale kwa mamlaka, na uwezo, na nguvu, na utukufu mkuu.

25 Na aanawakusanya watoto wake kutoka pembe nne za ulimwengu; na anahesabu kondoo wake, na wanamjua; na kutakuwa na zizi moja na bmchungaji mmoja; na atalisha kondoo wake, na kwake watapata cmalisho.

26 Na kwa sababu ya haki ya watu wake, aShetani hana nguvu; kwa hivyo, hawezi kufunguliwa kwa muda wa bmiaka mingi; kwani hana nguvu juu ya mioyo ya watu, kwani wanaishi katika haki, na yule Mtakatifu wa Israeli canatawala.

27 Na sasa tazama, mimi, Nefi, ninawaambia kwamba lazima vitu hivi vyote vitimizwe kulingana na mwili.

28 Lakini, tazama, mataifa yote, makabila yote, lugha zote, na watu wote wataishi salama katika Yule Mtakatifu wa Israeli ikiwa awatatubu.

29 Na sasa mimi, Nefi, ninakoma; kwani sitathubutu kuzungumza zaidi kuhusu vitu hivi.

30 Kwa hivyo, kaka zangu, ningetaka mfikirie kwamba vile vitu vilivyoandikwa kwenye amabamba ya shaba nyeupe ni vya kweli; na vinashuhudia kwamba lazima mtu atii amri za Mungu.

31 Kwa hivyo, msidhani kwamba mimi na baba yangu ndiyo pekee tumeshuhudia, na kuyafundisha. Kwa hivyo, kama mtatii aamri, na kuvumilia hadi mwisho, mtaokolewa katika siku ya mwisho. Na hivyo ndivyo ilivyo. Amina.