Maandiko Matakatifu
2 Nefi 27


Mlango wa 27

Giza na ukengeufu yataufunika ulimwengu katika siku za mwisho—Kitabu cha Mormoni kitatokea—Mashahidi watatu watakishuhudia kitabu—Mtu aliyeelimika atasema hawezi kukisoma kitabu kilichotiwa muhuri—Bwana atatenda kazi kuu na ya maajabu—Linganisha Isaya 29. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Lakini, tazama, katika asiku za mwisho, au katika siku za Wayunani—ndiyo, tazama mataifa yote ya Wayunani na pia Wayahudi, wote watakaokuja katika nchi hii na wale watakaokuwa katika nchi zingine, ndiyo, hata katika nchi zote za dunia, tazama, watalewa kwa maovu na aina zote za machukizo—

2 Na siku ile itakapofika wataadhibiwa na Bwana wa Majeshi, kwa radi na kwa mtetemeko wa ardhi, na kwa ngurumo, na kwa dhoruba, na kwa tufani, na kwa amwale wa moto unaounguza.

3 Na amataifa yote byapiganayo dhidi ya Sayuni, na yale yanayomuudhi, yatakuwa ni kama ndoto ya maono usiku; ndiyo, itakuwa kwao, hata kama mtu mwenye njaa aotaye, na tazama anakula lakini anaamka na nafsi yake ni tupu; au kama mtu aliye na kiu aotaye, na tazama anakunywa lakini anaamka na tazama anazirai, na nafsi yake ina hamu; ndiyo, hata hivyo ndivyo utakavyokuwa umati wa mataifa yote yapiganayo dhidi ya Mlima Sayuni.

4 Kwani tazama, nyote mnaotenda maovu, kaeni mlipo na mstaajabu, kwani mtalia, na kulia; ndiyo, mtalewa lakini sio kwa mvinyo, mtayumbayumba lakini sio kwa pombe kali.

5 Kwani tazama, Bwana amewamwagia roho ya usingizi. Kwani tazama, mmefunga macho yenu, na mmewakataa manabii; na watawala wenu, na waonaji amewafunika kwa sababu ya uovu wenu.

6 Na itakuwa kwamba Bwana Mungu atawaletea aninyi maneno ya bkitabu, na yatakuwa maneno ya waliokufa.

7 Na tazama, hicho kitabu kitakuwa kimetiwa amuhuri; na katika kitabu hicho patakuwa na bufunuo kutoka kwa Mungu, tangu mwanzo wa dunia hadi cmwisho wake.

8 Kwa hivyo, kwa sababu ya vitu ambavyo vimetiwa amuhuri, vitu viliyotiwa muhuri bhavitatolewa katika siku za uovu na machukizo ya watu. Kwa hivyo kitabu hicho kitawekwa mbali nao.

9 Lakini kitabu hicho atapewa amtu, na atapewa maneno ya kitabu hicho, ambayo ni maneno ya wafu walio mavumbini, na atatoa maneno haya kwa bmwingine;

10 Lakini maneno yaliyotiwa muhuri hatatoa, wala hatatoa hicho kitabu. Kwani kitabu hicho kitatiwa muhuri kwa nguvu za Mungu, na ufunuo uliotiwa muhuri utawekwa kitabuni humo hadi wakati mkamilifu wa Bwana utimie, kwamba yajulikane; kwani tazama, yanafunua vitu vyote tangu msingi wa ulimwengu hadi mwisho wake.

11 Na siku inafika ambapo yale maneno ya kile kitabu yaliyotiwa muhuri yatasomwa kutoka juu ya nyumba; na yatasomwa kwa uwezo wa Kristo; na vitu vyote avitafunuliwa watoto wa watu vile vilivyokuwa miongoni mwa watoto wa watu, na vile vitakavyokuwa hata hadi mwisho wa dunia.

12 Kwa hivyo, katika siku ile ambayo hicho kitabu kitatolewa kwa yule mtu ambaye nimemtaja, kitabu hicho kitafichwa kutokana na macho ya ulimwengu, kwamba hakuna macho yoyote yatakayokiona ila tu amashahidi bwatatu watakiona, kwa nguvu za Mungu, na kwa yule ambaye atapewa kitabu hicho; na watashuhudia ukweli wa kitabu hicho na kwa vitu vilivyomo.

13 Na hakuna yeyote atakayekiona, ila tu wachache kulingana na nia ya Mungu, kushuhudia kuhusu neno lake kwa watoto wa watu; kwani Bwana Mungu amesema kwamba maneno ya waaminifu yatanena ni kama akutoka kwa wafu.

14 Kwa hivyo, Bwana Mungu ataendelea kutoa maneno ya kitabu hicho; na kwa vinywa vya mashahidi wengi kama apendavyo ataimarisha neno lake; na ole ni kwa yule aanayekataa neno la Mungu!

15 Lakini tazama, itakuwa kwamba Bwana Mungu atamwambia yule aliyempa hicho kitabu: Chukua maneno haya ambayo hayajawekwa muhuri na umpatie mwingine, ili amwonyeshe aliyeelimika, akisema: aSoma hii, nakusihi. Na aliyeelimika atasema: Leta hapa kitabu, na nitayasoma.

16 Na sasa, kwa sababu ya utukufu wa ulimwengu na kupata afaida watasema haya, na sio kwa utukufu wa Mungu.

17 Na yule mtu atasema: Siwezi kuleta hicho kitabu, kwani kimetiwa muhuri.

18 Kisha aliyeelimika atasema: Siwezi kukisoma.

19 Kwa hivyo itakuwa kwamba, Bwana Mungu atatoa tena kitabu hicho na maneno haya kwa yule asiye elimika; na yule mtu asiye elimika atasema: Mimi sina elimu.

20 Kisha Bwana Mungu atamwambia: Walioelimika hawatayasoma, kwani wameyakataa, na ninaweza kufanya kazi yangu mwenyewe; kwa hivyo wewe utasoma yale maneno nitakayokupatia.

21 aUsiguse vitu vilivyotiwa muhuri, kwani nitavitoa katika wakati wangu mkamilifu; kwani nitawaonyesha watoto wa watu kwamba ninaweza kufanya kazi yangu mwenyewe.

22 Kwa hivyo, ukishamaliza kusoma maneno yale niliyokuamuru, na kupata wale amashahidi ambao nilikuahidi, basi utakitia kile kitabu muhuri tena, na kukificha kwangu, ili niyahifadhi maneno ambayo hujasoma, hadi nitakapotaka katika hekima yangu kuwafunulia watoto wa watu mambo yote.

23 Kwani tazama, mimi ni Mungu; na mimi ni Mungu wa amiujiza; na nitauonyesha ulimwengu kwamba Mimi bndimi yule jana, leo, na milele; na kwamba mimi sitendi lolote miongoni mwa watoto wa watu ila tu ckulingana na imani yao.

24 Na tena itakuwa kwamba Bwana atamwambia yule atakayesoma yale maneno atakayopewa:

25 aKwa sababu watu hawa wananikaribia kwa kinywa chao, na kwa midomo yao bwananisifu, lakini mioyo yao iko mbali nami, na hofu yao kwangu mimi inafundishwa kwa cnjia ya wanadamu—

26 Kwa hivyo, nitaendelea kufanya kazi ya akushangaza miongoni mwa watu hawa, ndiyo, kazi ya bkushangaza na ya maajabu, kwani hekima ya walio werevu na wenye elimu itaangamia, na ufahamu wa wapiga ramli wao utafichwa.

27 Na aole kwa wale wanaojaribu kumficha Bwana mashauri yao! Na matendo yao yako gizani; na wanasema: Nani anayetuona, na nani anayetujua? Na pia wanasema: Kwa hakika, upinduzi wako wa vitu juu chini utahesabiwa kama udongo wa bmfinyanzi. Lakini tazama, nitawaonyesha, asema Bwana wa Majeshi, kwamba najua matendo yao yote. Kwani kitu kitamwambia aliyekiunda, kwamba hakuniunda? Au kitu kilichojengwa kitamwambia mjenzi, hakuwa na ufahamu?

28 Lakini tazama, asema Bwana wa Majeshi: Nitaonyesha watoto wa watu kwamba ni muda kidogo uliobaki kwamba Lebanoni itageuzwa kuwa shamba lizaalo; na shamba lizaalo litakuwa kama msitu.

29 aNa katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu, na macho ya vipofu yataona kutoka fumboni na giza.

30 Na awapole pia nao wataongezeka, na bshangwe yao itakuwa katika Bwana, na walio masikini miongoni mwa wanadamu watashangilia katika yule Mtakatifu wa Israeli.

31 Kwa hakika jinsi Bwana aishivyo wataona kwamba yule ambaye ahutisha atakuwa bure, na mwenye kudharau ameangamizwa, na kwamba wale wote wanaotafuta uovu wanatengwa;

32 Na wale awanaomkosesha mtu kwa neno, na kumtegea mtego yule anayekemea blangoni, na ckumkataa mwenye haki kwa kitu kisichofaa.

33 Kwa hivyo, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, aliyemkomboa Ibrahimu, kuhusu nyumba ya Yakobo: Sasa Yakobo hataaibika, wala uso wake kugeuka rangi uwe mweupe.

34 Lakini aatakapoona watoto wake, ambao ni kazi ya mikono yangu, kati yake, watatakasa jina langu, na kumtakasa yule Mtakatifu wa Yakobo, na watamheshimu Mungu wa Israeli.

35 Wale nao pia awaliokosea katika roho watafahamu, na wale walionungʼunika bwatajifunza mafundisho ya dini.