Maandiko Matakatifu
Mosia 27


Mlango wa 27

Mosia anakomesha mateso na anaamrisha usawa—Alma mdogo na wana wanne wa Mosia wanajaribu kuangamiza Kanisa—Malaika anawatokea na kuwaamuru waache mwenendo wao wa uovu—Alma anapigwa na kuwa bubu—Wanadamu wote lazima wazaliwe tena ili kupata wokovu—Alma na wana wa Mosia wanahubiri habari njema. Karibia mwaka 100–92 K.K.

1 Na sasa ikawa kwamba yale mateso ambayo yaliwekelewa kanisa na wasioamini yalikuwa makuu hata kwamba kanisa likaanza kunungʼunika, na kulalamikia viongozi wao kuhusu hilo jambo; na walimlalamikia Alma. Na Alma akamwelezea mfalme wao, Mosia, hii kesi. Na Mosia alishauriana na makuhani wake.

2 Na ikawa kwamba mfalme Mosia alituma tangazo kote nchini kwamba wale wasioamini awasiwatese wale ambao walikuwa wa kanisa la Mungu.

3 Na kulikuwa na amri kali katika makanisa yote kwamba kusiwe na mateso miongoni mwao, na kwamba kuwe na ausawa miongoni mwa watu wote;

4 Kwamba wasikubali kiburi au maringo kuharibu aamani yao; kwamba kila mtu bamheshimu jirani yake jinsi anavyojiheshimu, na kufanya kazi kwa mikono yao wenyewe ili waishi.

5 Ndiyo, na makuhani wao wote na walimu wao wote iliwabidi kufanya akazi kwa mikono yao ili waweze kuishi, katika kila hali isipokuwa wanapougua, au wakiwa na taabu nyingi; na kwa kufanya vitu hivi, walipokea bneema ya Mungu.

6 Na kukawa na amani kubwa tena katika nchi; na watu wakaanza kuongezeka sana, na wakaanza kutawanyika huku na kule usoni mwa dunia, ndiyo, kaskazini na kusini, mashariki na magharibi, wakijenga miji mikubwa na vijiji katika sehemu zote za nchi.

7 Na Bwana aliwatembelea na kuwafanikisha, na wakawa watu wengi na matajiri.

8 Sasa wana wa Mosia walihesabiwa miongoni mwa wale makafiri; na pia amwana mmoja wa Alma alihesabiwa miongoni mwao, yeye akiitwa Alma, kama baba yake; walakini, akawa mtu mwovu na mwenye kuabudu bsanamu. Na alikuwa mtu wa maneno mengi, na aliwaelezea watu maneno mengi ya mzaha; kwa hivyo aliwaongoza watu wengi watende maovu kama yake.

9 Na akawa pingamizi kuu kwa mafanikio ya kanisa la Mungu; aakiiba mioyo ya watu; akisababisha mafarakano miongoni mwa watu; na kumpatia adui wa Mungu nafasi ya kuwatawala kwa uwezo wake.

10 Na ikawa kwamba alipokuwa akienda hivyo ili aangamize kanisa la Mungu, kwani alienda hivyo kwa kisiri na wana wa Mosia ili waangamize kanisa, na kuwapotosha watu wa Bwana, kinyume cha amri za Mungu, au hata mfalme—

11 Na kama vile nilivyowaelezea, jinsi vile awalivyomuasi Mungu, tazama, bmalaika wa Bwana caliowatokea; na alishuka kama kwa wingu; na alizungumza kwa sauti kama radi, iliyosababisha ardhi kutetemeka pale waliposimama;

12 Na walikuwa na mshangao mkuu, hata kwamba wakainama kwenye ardhi, na hawakufahamu maneno yale ambayo aliwazungumzia.

13 Walakini alipaza sauti tena, akisema: Alma, inuka na usimame, kwa nini wewe unalitesa kanisa la Mungu? Kwani Bwana amesema: aHili ni kanisa langu, na nitalijenga; na hakuna lolote litakalolipinga, ila tu watu wangu watende dhambi.

14 Na tena, malaika akasema: Tazama, Bwana amesikia asala za watu wake, na pia sala za mtumishi wake, Alma, ambaye ni baba yako; kwani ameomba kwa imani kubwa kukuhusu ili upate kuelimika kwa ukweli; kwa hivyo, ni kwa sababu hii nimekuja kukusadikisha kuhusu uwezo na mamlaka ya Mungu, kwamba bsala za watumishi wake zijibiwe kulingana na imani yao.

15 Na sasa tazameni, je unaweza kupinga nguvu za Mungu? Kwani tazama, si sauti yangu inatingisha ardhi? Na pia hunioni mbele yako? Na nimetumwa kutoka kwa Mungu.

16 Sasa nakwambia: Nenda, na ukumbuke utumwa wa babu zako katika nchi ya Helamu, na katika nchi ya Nefi; na kumbuka vile vitu vikuu ambavyo amewatendea; kwani walikuwa utumwani, na aamewakomboa. Na sasa nakuambia wewe, Alma, enda njia yako, na usijaribu kuangamiza kanisa tena, ili sala zao zijibiwe, na hivi hata kama wewe mwenyewe utataka kutupiliwa mbali.

17 Na sasa ikawa kwamba haya ndiyo yalikuwa maneno ya mwisho ambayo malaika alimwambia Alma, na akaondoka.

18 Na sasa Alma na wale wengine aliokuwa nao waliinama tena kwenye ardhi kwani mshangao wao ulikuwa mkuu; kwani kwa macho yao walikuwa wameona malaika wa Bwana; na sauti yake ilikuwa kama radi, ambayo ilitingisha ulimwengu; na walijua kwamba hakuna kingine chochote ila tu nguvu za Mungu ambazo zingetingisha ulimwengu mpaka ionekane kama itapasuka.

19 Na sasa mshangao wa Alma ulikuwa mkubwa sana kwamba akawa bubu, asiweze kufungua kinywa chake; ndiyo, na akawa mnyonge, hata kwamba hakuweza kunyosha mikono yake; kwa hivyo alibebwa na wale ambao walikuwa na yeye, akiwa hajiwezi, hata mpaka walipomweka mbele ya baba yake.

20 Na wakamwambia baba yake yote ambayo yaliwatokea; na baba yake alifurahi, kwani alijua kwamba ulikuwa ni uwezo wa Mungu.

21 Na akasababisha kwamba umati ukusanywe pamoja ili ushuhudie yale ambayo Bwana alikuwa amemtendea mwana wake, na pia kwa wale ambao walikuwa na yeye.

22 Na akasababisha kwamba makuhani wakusanyike pamoja; na wakaanza kufunga, na kumwomba Bwana Mungu wao kwamba afungue kinywa cha Alma, ili azungumze, na pia kwamba viungo vyake vipokee nguvu—kwamba macho ya watu yafunuliwe ili waone na watambue wema na utukufu wa Mungu.

23 Na ikawa kwamba baada ya wao kufunga na kuomba kwa muda wa siku mbili kuchwa, viungo vya Alma vilipokea nguvu, na akasimama na akaanza kuwazungumzia, na kuwaalika kwamba wawe na faraja:

24 Kwani, alisema, nimetubu dhambi zangu, na akukombolewa na Bwana; tazama nimezaliwa kwa Roho.

25 Na Bwana akaniambia: Usishangae kwamba wanadamu wote, ndiyo, wanaume na wanawake, mataifa yote, makabila, lugha na watu, lazima awazaliwe mara ya pili; ndiyo, wazaliwe na Mungu, bwabadilishwe kutoka hali yao ya ckimwili na ya kuanguka, kwa hali ya haki, na kukombolewa na Mungu, na kuwa wana na mabinti zake;

26 Na hivyo wanakuwa viumbe vipya; na wasipofanya hivi, ahawawezi kwa vyovyote kurithi ufalme wa Mungu.

27 Nawaambia, isipokuwa hivi, lazima watengwe; na hii najua, kwa sababu karibu mimi nitengwe.

28 Walakini, baada ya kupitia mateso mengi, na kukaribia kifo kwa kutubu, Bwana kwa rehema zake ameonelea kwamba ni vyema kuninyakua ili nisiungue amilele, na nimezaliwa na Mungu.

29 Nafsi yangu imekombolewa kutoka nyongo ya uchungu na vifungo vya uovu. Nilikuwa katika shimo la giza nyingi; lakini sasa naona mwangaza wa ajabu wa Mungu. Nafsi yangu ailisononeshwa na uchungu usio na mwisho; lakini nimenyakuliwa, na nafsi yangu haina maumivu tena.

30 Nilimkataa Mkombozi wangu, na kuyakana yale ambayo yalizungumzwa na babu zetu; lakini sasa ili waone kuwa atakuja, na kwamba yeye hukumbuka kila kiumbe ambacho ameumba, atajidhihirisha kwa wote.

31 Ndiyo, akila goti litainama, na kila ulimi utakiri mbele yake. Ndiyo, hata katika siku ya mwisho, ambapo wanadamu wote watasimama bkuhukumiwa na yeye, kisha watakiri kwamba yeye ni Mungu; na kisha watakiri, wale ambao wanaishi ulimwenguni cbila Mungu, kwamba hukumu ya adhibio isiyo na mwisho ambayo iko juu yao ni ya haki; na watatetemeka, na kutikisika, na kuogopa mbele ya tazamo la jicho lake ambalo huona dkote.

32 Na sasa ikawa kwamba Alma alianza kutoka wakati huu na kwenda mbele kufundisha watu, na wale ambao walikuwa na Alma wakati ambao malaika aliwatokea, wakisafiri kote nchini, wakiwatangazia watu wote vitu vile ambavyo walikuwa wameona na kusikia, na kuhubiri neno la Mungu kwa mateso mengi, wakiteswa sana na wale wasioamini, na wakipigwa na wengi wao.

33 Licha ya haya yote, walilifariji kanisa sana, na kuthibitisha imani yao, na kuwaonya kwa subira kuu na uchungu wazitii amri za Mungu.

34 Na wanne wao walikuwa ni awana wa Mosia; na majina yao yalikuwa ni Amoni, na Haruni, na Omneri, na Himni; haya ndiyo yalikuwa majina ya wana wa Mosia.

35 Na walisafiri katika nchi yote ya Zarahemla, na miongoni mwa watu wote ambao walitawaliwa na mfalme Mosia, wakijibidiisha kuponya majeraha yote ambayo walikuwa wamelifanyia kanisa, wakitubu dhambi zao zote, na kutangaza vitu vyote ambavyo walikuwa wameona, na wakieleza unabii na maandiko kwa wote ambao walitaka kuyasikia.

36 Na hivyo walikuwa vyombo mikononi mwa Mungu kwa kuwezesha wengi kufahamu ukweli, ndiyo, kwa ufahamu wa Mkombozi wao.

37 Na jinsi gani walivyobarikiwa! Kwani awalitangaza amani; walitangaza bhabari njema ya mambo mema; na waliwatangazia watu kwamba Bwana anatawala.