2018
Mahala Pesa ya Zaka Huenda
Oktoba 2018


Kile Tunachoamini

Mahala Pesa ya Zaka Huenda

Je, nini hutokea kwenye pesa unayolipa kwa ajili ya zaka?

Picha
where tithing money goes
  • Unapata pesa.

  • Unachangia asilimia 10 ya pato lako kwa ajili ya zaka (ona M&M 119).

  • Unampa zaka yako mmoja wa washiriki wa uaskofu au rais wa tawi au unaiwasilisha kwa kutumia mtandao kupitia donations.lds.org.

  • Katika Makao Makuu, Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi ndiyo Baraza linalosimamia Matumizi ya Zaka (ona M&M 120). Kama wanavyoelekezwa na Bwana, wanafanya maamuzi yenye mwongozo wa kiungu juu ya jinsi gani zaka hizi takatifu zitatumika.

Zaka zinaweza kutumika kwa ajili ya:

  • Kujenga na kutunza mahekalu, makanisa na majengo mengine ya Kanisa.

  • Kuendesha programu za elimu za Kanisa

  • Kuchapisha maandiko na nyenzo zingine

  • Kufanya utafiti wa historia ya familia

  • Kusaidia juhudi za kiustawi na misaada ya kibinadamu

  • Kufanya kazi ya umisionari

  • Kusaidia katika shughuli za kanisa kwa ajili ya ushirika kati ya waumini wa kata au tawi

Vielelezo na David Green