2018
Je, ushuhuda ni zaidi ya hisia pekee?
Oktoba 2018


Penye Umuhimu

Je, ushuhuda ni zaidi ya hisia pekee?

Picha
young woman reading the Book of Mormon

Ushuhuda ni kile ambacho Mwokozi alikuwa akikiongelea alipomwambia Petro, “Mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 16:17). Ni uelewa toka kwa Mungu uliofunuliwa kupitia Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu huongea kwa sauti ambayo tunaihisi zaidi kuliko kuisikia, lakini huja kote “mawazoni mwako na katika moyo wako” (M&M 8:2; msisitizo umeongezwa)—mawazoni mwetu na pia katika hisia zetu.

Nabii Joseph Smith alielezea roho ya ufunuo kama hisia za “uelewa msafi utiririkao kwako, [ukikupatia] mawazo ya papo kwa papo” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 132).

Tunapogeuza mawazo yetu na mioyo yetu—mawazo yetu, hisia, na hamu—kwa Mungu, Anaweza kuongea kwenye mawazo yetu na mioyo yetu kwa sauti ndogo, na tulivu ya Roho Mtakatifu. Anapohusisha roho zetu, hisia na mawazo dhahiri huonekana kutiririka kwetu. Huu ndio ushuhuda Anaotupatia.