2018
Malkia Esta
Oktoba 2018


Hadithi za Maandiko Matakatifu

Malkia Esta

Kutoka Esta 2–8.

Picha
Esther the Queen 1
Picha
Esther the Queen 2
Picha
Esther the Queen 3

Esta alikuwa malkia. Alikuwa ameolewa na mfalme wa Uajemi.

Mfalme alikuwa na rafiki ambaye alikuwa mtu mbaya. Alimdanganya mfalme kuweka sheria kwamba Wayahudi wote lazima wauwawe! Mfalme hakujua kwamba mke wake, Esta, alikuwa Myahudi.

Esta aliamua kumuomba mume wake, mfalme, kuwaokoa watu wake. Lakini alikuwa na wasiwasi kwamba angekasirika. Esta aliwaomba Wayahudi wote kufunga na kusali kwa ajili yake. Kisha Esta akaenda kwa mfalme. Mfalme hakukasirika!

Esta alimwalika mfalme na rafiki zake waje kwenye karamu. Katika karamu, Esta alimwambia mfalme kwamba yeye alikuwa ni Myahudi. Mfalme alikasirika kwamba rafiki yake alikuwa amemdanganya. Angewaambia Wayahudi kwamba wangeweza kujilinda. Esta alisaidia kuokoa watu wake!

Tunaweza kusali kumwomba Baba wa Mbinguni msaada. Tunaweza kuwa jasiri na shupavu, kama Esta.