2018
Mng’aro angavu huko Jamhuri ya Czech
Oktoba 2018


Angaza Nuru Yako

Mng’ao Angavu huko Jamhuri ya Czech

Imeandaliwa na Sharon Goodrich, Majarida ya Kanisa

Picha
Shining Bright in the Czech Republic

Sisi ni watoto wa Msingi katika Jamhuri ya Czech. Hivi ndivyo tung’aavyo kwa uangavu katika nchi yetu.

Wakati mmoja nilipoteza glavu yangu ninayoipenda sana. Nilikuwa na huzuni sana. Mimi pamoja na mama yangu tulisali, lakini hatukuipata. Nilijaribu kuwa na imani. Wiki moja baadae, kaka yangu mdogo aliipata glavu yangu mtaani! Mungu alijibu sala zetu. Ninampenda Yeye na ninajua anaishi.

Andre W., miaka 9

Nina marafiki shuleni ambao si waumini wa Kanisa lakini ambao bado wanaheshimu viwango vyangu. Kuna wakati nilisema lazima tusali, na walikubali! Nilikuwa mwenye furaha sana.

Ivana A., miaka 11

Mimi pamoja na rafiki zangu tulikuwa tukishuka ngazi. Wakati tulipofika kwenye lifti, nilipata hisia ambazo si za utulivu na nikawaomba rafiki zangu tusiitumie. Lakini waliamua kuitumia hivyo hivyo. Mimi nilitumia ngazi. Nilipofika chini, rafiki zangu hawakuwepo pale. Lifti ilikuwa imekwama! Iliwachukua muda kabla hawajatoka nje. Nilikuwa na furaha kwamba hakuna madhara yoyote makubwa yalitokea. Pia nilihisi furaha kwamba nilimfuata Roho Mtakatifu.

Amalie N., miaka 10

Ufukweni, wingu lilianza kuwa jeusi. Upepo ulivuma na kutengeneza mawimbi makubwa! Kulikuwa na ngurumo, radi na mvua ya mawe. Kila mtu alikimbia kujikinga. Hatukudhurika na dhoruba. Njiani kurudi nyumbani, tuliona pinde tatu za mvua. Tunajua kwamba Mungu alitusaidia na kutulinda.

Jakub B., miaka 10

Shuleni nina rafiki ambaye hakuna mtu mwingine anataka kuwa rafiki yake. Watoto wengine walianza kusema vitu vya kejeli kwake ambavyo vilimfanya ajihisi mbaya. Nilimwambia mwalimu na nilimwalika rafiki yangu kucheza nami. Ilimfanya rafiki yangu kuwa na furaha!

Ludmila V., miaka 8

Nilimkasirikia mama yangu kwa sababu sikutaka kuoga na kwenda kulala. Siku iliyofuata nilijisikia vibaya kutokana na uchaguzi wangu mbaya. Mama alisema tunaweza kusali na kumwomba Baba wa Mbinguni atusamehe. Tulipiga magoti na kusali. Nilijihisi vyema. Nilijifunza kwamba tunaweza kutubu, na kwa sababu ya Yesu Kristo, tukasamehewa.

Samuel H., miaka 5

Nilitoa ushuhuda wangu kanisani. Nilijipa ujasiri! Tangu wakati huo, nimemhisi Roho.

Eliska K., miaka 11

Wakati nguruwe wangu wa guinea alipoumwa, nilisali kwa ajili yake. Nina shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa sababu alitusaidia.

Aneta P., mika 10