2018
Kukubali kwetu Kuunga mkono
Oktoba 2018


Mpaka Tutakapokutana Tena

Kukubali kwetu Kuunga mkono

Kutoka katika hotuba ya mkutano mkuu wa Oktoba 2005.

Mwongozo wa kiroho kwa kiasi kikubwa hutegemea kuwa katika mtazamo sawa na … manabii, waonaji, na wafunuzi.

Picha
raised hands

Ninatamani kuongea kuhusu ofisi takatifu za hao viongozi wa ukuhani ambao “wameitwa na kuteuliwa” (M&M 55:1) kuongoza Kanisa katika siku hii. …

… Ndugu zangu [katika Akidi ya Mitume Kumi na Wawili], bila kuwa na tofauti yoyote, ni watu wazuri, wenye kuheshimika, na wenye kuaminika. Ninaijua mioyo yao. Wao ni watumishi wa Bwana. Nia yao pekee ni kufanya kazi katika wito wao mkuu na kujenga Ufalme wa Mungu duniani. Ndugu zetu wanaotumikia katika siku na wakati huu wamethibitishwa, wamejaribiwa na ni wa kweli. … Mioyo yao ni misafi sana, uzoefu wao ni mkubwa sana, mawazo yao ni mazuri sana, na hekima yao ya kiroho ni ya kina kwamba inatia faraja kuwa tu katika uwepo wao.

… [Wakati nilipoitwa, nilishauriwa] kwamba kitu muhimu zaidi ambacho sina budi kukifanya ni kila mara kuwa katika mtazamo sawa na ndugu zangu. … Hiyo inawiana na kitu ambacho nilitaka kukifanya kwa moyo wangu wote.

… Nimehitimisha kwamba mwongozo wa kiroho kwa kiasi kikubwa hutegemea kuwa katika mtazamo sawa na Rais wa Kanisa, Urais wa Kwanza, na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili—wote ambao katika hao wamekubaliwa … kama manabii, waonaji na wafunuzi. Sijui ni kwa namna ipi tunaweza kuwa katika mtazamo sawa kikamilifu na Roho wa Bwana kama hatuko katika mtazamo sawa na Rais wa Kanisa na manabii wengine, waonaji, na wafunuzi. …

Ushauri wangu kwa waumini wa Kanisa ni kumuunga mkono Rais wa Kanisa, Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Viongozi wengine Wakuu wenye Mamlaka kwa moyo na nafsi zetu zote. Kama tutafanya hivyo, tutakuwa katika bandari salama. …

Pia tunahitajika kuwaunga mkono na kuwakubali viongozi wa maeneo yetu, kwa sababu wao pia “wameitwa na kuteuliwa.” Kila muumini wa Kanisa hili anaweza kupokea ushauri toka kwa askofu au rais wa tawi, kigingi au rais wa misheni, na Rais wa Kanisa pamoja na wenzake. Hakuna hata mmoja kati ya ndugu hawa aliomba wito wake. Hakuna aliyekamilika. Hata hivyo wao ni watumishi wa Bwana, walioitwa na Yeye kupitia wale walio na haki ya ufunuo. Wale walioitwa, kukubaliwa, na kutengwa wana haki ya kupata ukubali wetu wa kuungwa mkono . …