2018
Masomo 4 kutokana na Uletaji wa Kitabu cha Mormoni kupitia Joseph Smith
Oktoba 2018


Kidijitali Pekee

Masomo 4 kutokana na Uletaji wa Kitabu cha Mormoni kupitia Joseph Smith

Akiwa na miaka 24 tu, Joseph Smith alikumbana na changamoto wakati akifanya kazi kutimiza amri za Mungu. Lakini alizishinda kwa msaada wa Mungu, hivyo nasi tunaweza pia.

Picha
young adult woman holding an old Book of Mormon

Kama vijana wakubwa, tunaweza kuombwa kufanya vitu vinavyoonekana kutowezekana pasipo msaada wa Mungu. Vivyo hivyo, Joseph Smith, katika umri wa miaka 24 tu, alikabiliana na changamoto na kuhisi kutoweza kuzishinda wakati akitafuta kutimiza amri muhimu—kuchapisha tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Lakini kwa msaada wa Mungu, alitimiza kila kitu ambacho aliambiwa, na mfano wake unaonyesha njia kadhaa ambazo tunaweza kufanya yasiyowezekana kuwezekana wakati Mungu akiwa upande wetu.

  1. Hatutakiwi kuwa wakuu ili Mungu afanye miujiza kupitia sisi. Wakati Joseph akijiandaa kuchapisha Kitabu cha Mormnoni, alikuwa kijana mkubwa asiye na fedha nyingi au elimu rasmi—achilia mbali uelewa wa jinsi ya kutafsiri na kuchapisha kumbukumbu hiyo muhimu. Lakini, bado alisonga mbele kwa imani na kipawa na nguvu za Mungu kukamilisha kazi ambayo alikuwa amepewa. Kama tutamwamini Baba wa Mbinguni, Anaweza kutuwezesha kufanya kazi Yake.

  2. Mungu akitupatia kazi, Huandaa njia ya kuitimiza. Kwa Joseph, kuchapisha nakala 5,000 za kurasa 590 za kitabu lazima ilionekana kutowezekana. Lakini, wakati ulipofika wa kuchapisha miswada, Bwana alimpatia msukumo Martin Harris kuweka dhamana shamba lake lenye rutuba, akitoa dola 3,000 (sawa na dola 76,000 za leo) kumsaidia Joseph kutimiza kazi yake. Kama Nefi alivyofundisha, “[Bwana] atawatayarishia njia kwamba waweze kutimiza kitu ambacho amewaamuru” (1 Nefi 3:7). Baba wa Mbinguni aliweka rasilimali muhimu kuweza kufikiwa na Joseph ili kukamilisha kazi. Na atafanya hivyo kwetu sisi.

  3. Mungu hutoa nafasi za pili. Joseph Smith alifanya makosa ambayo yalipelekea kupotea kwa kurasa 116 za mswada wa Kitabu cha Mormoni. Kwa sababu ya kupoteza kurasa 116, Joseph pia alipoteza uwezo wa kutafsiri kwa muda. Lakini kwa sababu alichagua kutubu, hatimaye alisamehewa na kupewa nafasi ya pili kutimiza kazi yake. Bwana alisema “Lakini kumbuka, Mungu ni mwenye rehema; hivyo basi, tubu kwa lile ambalo umelifanya ambalo ni kinyume cha amri ambazo nilikupa, na wewe bado u mteule, na wewe tena umeitwa kuifanya kazi” (M&M 3:10). Maisha yetu yatajawa na makosa katika maisha haya, lakini tunapotubu na kuwa na mioyo yetu katika sehemu sahihi, Bwana mara zote atatupatia nafasi nyingine.

  4. Kutegemea shangwe iliyoahidiwa kunaweza kutusaidia kuzishinda changamoto. Bila kujali changamoto Joseph alizotakiwa kukabiliana nazo, alipokea baraka nyingi na kupata furaha ya kweli kipindi chote cha kazi yake ya kuleta Kitabu cha Mormoni. Baada ya Kitabu cha Mormoni kuchapishwa, Kanisa liliundwa na wazazi wa Joseph walibatizwa. Siku hiyo, Joseph alikwenda kwenye kisitu peke yake na kuanza kulia kwa furaha. Kama tutapita katika majaribu tukiwa tumeinua vichwa vyetu, tukiweka tumaini letu lote kwa Mungu, tutaweza pia kupata shangwe na amani.