2018
Safari ya Mwisho ya Mwokozi, Safari ya Upweke
April 2018


Safari ya Mwisho ya Mwokozi, Safari ya Upweke

Picha
the saviors final lonely journey PDF 1
Picha
the saviors final lonely journey PDF 2
Picha
the saviors final lonely journey PDF 3

Katika maisha Yake yote ya duniani, Mwokozi alipitia safari nyingi—safari Yake kutoka Bethlehemu na kwenda Misri akiwa mtoto mchanga, safari Yake ya siku-40 nyikani, safari Zake nyingi mijini, vijijini, na majumbani kufundisha, kuponya, na kubariki wakati wa huduma Yake, na nyingine nyingi. Lakini kuna safari moja ambayo Mwokozi alipaswa kuipitia peke yake, na ilikuwa safari ambayo ni Yeye pekee ndiye angeweza kuivumilia.

“Katika Jumapili ya Pasaka tunasherehekea tukio kuu na tukufu lililosubiriwa zaidi katika historia ya ulimwengu.

“Ni siku ambayo ilibadilisha kila kitu.

“Katika siku hiyo, maisha yangu yalibadilika.

“Maisha yako yalibadilika.

“Hatima ya watoto wote wa Mungu ilibadilika.”

Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, “Zawadi ya Neema,” Liahona, Nov. 2015, 107.

Kuteseka kusio na Kifani

Picha
Jesus in Gethsemane

Ee Baba Yangu, na Simon Dewey

“Hakuna akili ya kidunia inayoweza kupokea maana yote ya kile ambacho Kristo alifanya katika Gethsemane.

“Tunajua alitoa jasho jingi la damu kwenye kila kinyweleo alipokuwa akinywa mashapo ya kile kikombe kichungu ambacho Baba yake alimpa.

“Tunajua aliteseka, vyote viwili mwili na roho, zaidi ya inavyowezekana mwanadamu kuteseka, isipokuwa tu katika kifo.

“Tunajua kwamba katika njia fulani, zisizoeleweka kwetu, mateso yake yaliridhisha madai ya haki, akikomboa nafsi zenye kutubu kutokana na maumivu na adhabu ya dhambi, na kufanya rehema ipatikane kwa wale waaminio katika jina lake takatifu.

“Tunajua kwamba aliaanguka kifudifudi juu ya ardhi wakati maumivu na mateso ya mzigo usio na mwisho yalimsababisha atetemeke na kutamani kwamba asinywe kikombe kile kichungu.”

Mzee Bruce R. McConkie (1915–85) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “The Purifying Power of Gethsemane”, Ensign, Mei 1985, 9.

Matumizi Binafsi: Japokuwa tunaweza daima tusitambue, Huyu Mwokozi aliteseka aina zote za maumivu wakati wa Upatanisho. Yeye anaelewa kila maumivu ya kimwili, kuanzia mfupa uliovunjika mpaka kwenye ugonjwa wa muda mrefu wenye maumivu makali. Alihisi giza na kukata tamaa kwa maradhi ya akili kama vile mfadhaiko, wasiwasi, uraibu, upweke, na huzuni. Na alilisikia kila jeraha la kiroho kwa sababu alijichukulia juu Yake dhambi zote za wanadamu.

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha, “Katika wakati wa udhaifu tunaweza kulia, ‘Hakuna anayejua jinsi ilivyo. Hakuna anayeelewa.’ Lakini Mwana wa Mungu anajua vizuri kabisa na anaelewa, kwani aliona na kubeba mizigo yetu ya kibinafsi” (“Walibeba Mizigo Yao kwa Urahisi,” Liahona, Mei 2014, 90).

Alikuwa ni Yeye Pekee Aliyeweza

Picha
carrying the cross

Maandamano kuelekea Kalvari, na Bernardo Cavallino, Chrysler Museum of Art

“Kile alichofanya kingeweza tu kufanywa na Mungu. Kama Mwana Pekee wa Baba katika mwili, Yesu alirithi sifa za kiungu. Alikuwa mtu pekee aliyewahi kuzaliwa duniani ambaye angeweza kufanya tendo hili muhimu zaidi na la kiungu. Kama Mtu pekee asiye na dhambi aliyewahi kuishi katika dunia hii, Hakuwa chini ya kifo cha kiroho. Kwa sababu ya uungu Wake, Yeye pia alikuwa na nguvu juu ya kifo cha kimwili. Hivyo Yeye alitufanyia sisi kile ambacho hatuwezi kujifanyia wenyewe. Alifungua kamba baridi za mauti Alifanya pia iwezekane kwetu kuwa na faraja ya juu na safi ya kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Rais James E. Faust (1920–2007), Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, “Upatanisho: Tumaini Letu Kuu,” Liahona, Jan. 2002, 20.

Matumizi Binafsi: Kupitia Upatanisho Wake, Mwokozi alifungua kamba za kifo na alitukomboa wote kutokana na dhambi zetu ili kwamba kila mtu aweze kuwa na uzima wa milele. Yeye tu ndiye aliyekuwa na uwezo wa kutimiza kazi hiyo ya kuogofya na isiyowezekana. Tunapokuwa tunakabiliwa na changamoto kali, tunaweza kupata faraja katika kujua kwamba hakika Mwokozi anaweza kufanya kisichowezekana kiwezekane.

Yeye Hakugeuka

Picha
the burial

Mazishi, na Carl Heinrich Bloch

“Juu ya mlima uitwao Kalvari, wakati wafuasi wasio na msaada wakitazama, mwili Wake wenye majeraha ulipigiliwa msalabani. Bila huruma Alifanyiwa mzaha na kulaaniwa na kubezwa. …

“Saa zake za maumivu zilipita wakati maisha Yake yakififia. Kutoka katika midomo Yake iliyokauka yalitoka maneno, ‘Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema hayo, akakata roho.’ …

“Katika wakati wa mwisho, Bwana angeweza kugeuka. Lakini hakufanya hivyo. Alipita chini ya vitu vyote ili aweze kuokoa vitu vyote. Mwili wake usio na uhai uliharakishwa lakini taratibu uliwekwa ndani ya kaburi la kuazima.”

Rais Thomas S. Monson (1927–2018), “Amefufuka!”, Liahona, Mei. 2010, 89.

Matumizi Binafsi: Aliteseka kutokana na maumivu makali, upweke, na kufa moyo, lakini bado Mwokozi alivumilia na kumaliza safari Yake ya maisha ya duniani kwa upendo—hata kumuomba Baba Yake kuwasamehe wale waliomsulubisha. Kwa sababu ya upendo Wake mkamilifu, tunaweza kukabiliana na majaribu na magumu yetu kwa upendo, na kwa msaada Wake tunaweza pia kuvumilia hadi mwisho.

Mashahidi Wengi wa Ufufuko Wake

Picha
Mary at the tomb

Mwanamke, Kwa nini Unalia? na Mark R. Pugh

“Ninaamini mashahidi wengi wa Ufufuko wa Mwokozi ambao uzoefu na shuhuda zao hupatikana katika Agano Jipya—Petro na wenza wake wale kumi na wawili na mpendwa, msafi Mariamu wa Magdala, miongoni mwao. Ninaamini shuhuda zinazopatikana katika Kitabu cha Mormoni—wa Nefi Mtume pamoja na umati ambao hawakutajwa majina katika Bountiful, miongoni mwao. Na ninaamini ushuhuda wa Joseph Smith na Sidney Rigdon ambao, baada ya shuhuda nyingine nyingi, walitangaza ushahidi mkuu wa kipindi hiki cha mwisho cha mwongozo wa Mungu ‘kwamba yu hai! Kwani tulimuona.’ Chini ya mtazamo wa uoni wote wa jicho Lake, ninasimama mwenyewe kama shahidi kwamba Yesu wa Nazareti ni Mkombozi aliyefufuka, na ninashuhudia kwa yote yatakayofuata kutoka kwenye ukweli wa Ufufuko Wake. Na upokee usadikisho na faraja ya ushahidi kama huo.

Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “Ufufuko wa Yesu Kristo,” Liahona, Mei 2014, 114.

Matumizi Binafsi: japokuwa hatukuwa kati ya wale waliouona mwili uliofufuka na mkamilifu wa Mkombozi, bado tunaweza kusimama kama mashahidi Wake leo. Yeye daima anaweza kuwa lengo la maisha yetu, bila kujali muda au mahali tunapojikuta. Kila mara tunapotoa mioyo na mikono yetu kuwatumikia wengine; kuonyesha upole, ukarimu, na heshima kwa wote; kutetea ukweli; na kutoa shuhuda zetu za injili, tunasimama kama mashahidi wa kweli wa Yesu Kristo.

Hatuna Haja ya Kutembea Peke Yetu

Picha
Christ walking along the shores

Utondoti kutoka Walk with Me, na Greg Olsen, yasinakiliwe

“Mojawapo ya faraja kuu ya kipindi hiki cha Pasaka ni kwamba kwa sababu Yesu alitembea njia hiyo ndefu ya upweke kabisa peke yake, sisi hatuhitaji kufanya hivyo. Safari yake ya upweke ilileta umoja mkubwa kwa tafsiri yetu ndogo ya njia ile—utunzaji wa rehema wa Baba Yetu wa Mbinguni, wenza usioshindwa wa huyu Mwanawe Mpendwa, kipawa kikamilifu cha Roho Mtakatifu, malaika walio mbinguni, wanafamilia pande zote mbili za pazia, manabii na mitume, walimu, viongozi, marafiki. Vyote hivi na zaidi vimetolewa kama wenza kwa safari yetu ya maisha ya duniani kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo na Urejesho wa injili Yake. Ukitangazwa kutoka kilele cha mlima Kalvari ni ukweli kwamba kamwe hatutaachwa peke yetu wala bila msaada, hata kama wakati mwingine tunaweza kuhisi tumeachwa. …

“… Na tusimame na Yesu Kristo ‘nyakati zote na katika mambo yote, na mahali popote [tulipo], hata hadi kifo,’ kwani hakika hivyo ndivyo alivyosimama nasi wakati ili kuwa katika kifo na alipotakiwa kusimama kabisa peke yake.”

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “Hakuna Aliyekuwa Pamoja Naye,” Liahona, Mei 2009, 88.

Matumizi Binafsi: Pasaka Hii, kumbuka safari ya mwisho ya Mwokozi, safari ya upweke. Alijitolea kila kitu alichokuwa nacho ili kwamba wewe na kila mtu duniani aweze kuwa msafi na kupata uzima wa milele. Jifunze kutokana na mfano Wake mkamilifu. Muweke katika mawazo yako na katika moyo wako. Na daima kumbuka kwamba kamwe hauko peke yako. Kwa sababu alivumilia safari Yake ya mwisho kwa ukamilifu wa kipekee, Yeye hatakuacha. Upendo Wake kwako hauna mwisho na haubadiliki, na anasimama tayari kukupatia amani, faraja, na tumaini unapoendelea katika safari yako mwenyewe. Zawadi yake ya Upatanisho haina mwisho, na ilitolewa kwako.