2018
Njia za kuelekea kwenye Furaha ya Kweli
April 2018


Njia za kuelekea kwenye Furaha ya Kweli

Kutoka kwenye hotuba ya mwanzo,“Njia za Kuelekea kwenye Furaha,” iliyotolewa katika Chuo Kikuu cha Brigham Young–Hawaii mnamo Juni 8, 2017.

Hebu kila mmoja wetu achague kumpenda Bwana na kufuata njia Zake za kuelekea kwenye furaha.

Picha
couple standing outside the Oakland California Temple

Zaidi ya kitu kingine chochote, Baba wa Mbinguni hutamani furaha yetu ya kweli na ya kudumu.

“Furaha yetu ni kielelezo cha baraka zote anazotupatia—mafundisho ya injili, amri, ibada za ukuhani, mahusiano ya kifamilia, manabii, mahekalu, uzuri wa uumbaji, na hata fursa ya kupitia dhiki. … Alimtuma Mwanawe Mpendwa kufanya Upatanisho ili sisi tuweze kupata furaha katika maisha haya na kupokea ukamilifu wa shangwe katika milele.”1

Watu kila mahali wanatafuta kitu fulani. Katika njia zao wenyewe, kile hasa wanachokitafuta ni furaha. Kama kwa ukweli wenyewe, hata hivyo, wengi huzuiliwa kuipata furaha kwa “sababu tu hawajui mahali pa kuipata” (M&M 123:12).

Kwa sababu hawajui wapi pa kupata furaha ya kweli na ya kudumu, wanaitafuta kwenye mambo ambayo huleta furaha ya muda tu—kununua vitu, kutafuta heshima na sifa kutoka kwa ulimwengu kupitia tabia zisizofaa, au kuzingatia kwenye uzuri wa kimwili na mvuto.

Anasa mara nyingi huchanganywa na furaha. Inaonekana kwamba kadiri watu wanavyozidi kutafuta anasa ya muda, ndivyo wanavyozidi kupungukiwa na furaha. Mara nyingi, anasa hudumu kwa muda mfupi tu.

Kama Rais David O. McKay (1873–1970) alivyosema: “unaweza kupata ile anasa ya muda mfupi, ndiyo, lakini huwezi kupata shangwe, huwezi kupata furaha. Furaha hupatikana kwenye ile njia iliyochakaa, nyembamba kama ilivyo, japo imesonga, iongozayo kwenye uzima wa milele.”2

Bahati mbaya kwa wengi, furaha ni vigumu kuipata. Wanasayansi wanajua kwamba “zaidi ya hali chanya tu, furaha ni hali ya hali njema ambayo hujumuisha kuishi maisha mazuri—ambayo ni, kwa ufahamu wa maana na utoshelevu wa kina.”3

Utafiti unaonyesha kwamba furaha siyo kuruka kutoka uzoefu mmoja kwenda mwingine. Badala yake, kujipatia furaha hasa hujumuisha “juhudi za-muda mrefu kwa kitu cha muhimu zaidi katika maisha.” Furaha husababishwa na mazoea, tabia, na mpangilio wa mawazo ambayo tunaweza kushughulikia moja kwa moja kwa matendo ya makusudi. Sehemu kubwa ya furaha yetu kwa kweli iko “chini ya udhibiti wa mtu binafsi.”4

Acha tufikirie umuhimu wa baadhi ya njia za furaha zinazopatikana ndani ya maandiko na kufundishwa na manabii na mitume wa siku hizi. Kwa uaminifu na kwa uthabiti tukipanda hatua zetu juu ya njia hizo itaturuhusu sisi kufaidi furaha katika safari iliyo mbele yetu.

Wema

Ya kwanza katika njia hizo ni wema, ambayo ni mpangilio wa mawazo na tabia zilizojengwa katika viwango vya juu vya maadili. Inajumuisha usafi wa kimwili na usafi wa kimaadili, ambayo hukupa ustahili wa kuingia kwenye mahekalu matakatifu ya Bwana. Watu wema huwa na heshima tulivu na nguvu ya ndani. Ni wenye kujiamini kwa sababu wao wanastahili kupokea na kuongozwa na Roho Mtakatifu. Wema huanzia ndani ya moyo na akili, na ni mkusanyiko wa maelfu ya maamuzi na matendo madogo madogo kila siku.

“Acha wema uyapambe mawazo yako bila kukoma; ndipo kujiamini kwako kutakuwa imara katika uwepo wa Mungu; na mafundisho ya ukuhani yatatonatona juu ya nafsi yako kama umande utokao mbinguni.

“Roho Mtakatifu atakuwa mwenzi wako daima, na fimbo yako ya kifalme fimbo isiyobadilika ya haki na ukweli; na utawala wako utakuwa utawala usio na mwisho, na usio wa njia ya kulazimisha utatiririka kwako milele na milele” (M&M 121:45–46).

Rais Thomas S. Monson (1927–2018) amefundisha kwamba “hakuna urafiki wenye thamani zaidi kuliko dhamiri safi yako mwenyewe, usafi wako mwenyewe wa maadili—na ni hisia tukufu iliyoje kujua kwamba unasimama katika sehemu yako husika msafi na mwenye kujiamini kwamba unastahili kufanya hivyo.”5

Unyoofu

Njia ya pili ya furaha ni unyoofu. Mzee Richard G. Scott (1928–2015) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha:

“Tambua kwamba furaha ya kudumu huja kutokana na vile ulivyo, siyo kutokana na kile unacho.

“Shangwe halisi huja kutokana na hulka ya haki, na hiyo hujengwa kutokana na maamuzi endelevu ya haki. … Maamuzi yako ya haki huamua wewe ni nani na nini ni muhimu kwako. Yanafanya ufanyaji wa mambo mema uwe rahisi. Kwa furaha sasa na katika maisha yako yote, kwa uthabiti mtii Bwana.”6

Tunaposoma maandiko, tunajifunza kwamba ahadi zilizoahidiwa na Bwana kwetu huchochea kuishi kwa haki. Ahadi hizo hurutubisha nafsi zetu, hutuletea tumaini kwa kututia moyo tusikate tamaa hata katika uso wa changamoto zetu za kila siku za kuishi katika ulimwengu unaofifia katika maadili na unyofu wa tabia. Kwa hivyo, tunahitajika kuhakikisha kwamba mawazo, maneno, na matendo yetu yanatuongoza kwenye njia ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni.

Uaminifu

Njia ya tatu kuelekea kwenye furaha ni uaminifu. Ni muhimu kuelewa kwamba Mungu hutubariki kulingana na imani yetu, ambayo ni chanzo cha kuishi kwa lengo takatifu na mtazamo wa milele. Imani ni kanuni ya matendo ambayo hushawishi bidii. Huonekana katika mtazamo wetu chanya na matamanio ya kuwa radhi kufanya kila kitu ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tufanye. Ni kile kinachotupeleka kupiga magoti kumuomba Bwana mwongozo na hutuhamasisha kuinuka na kutenda kwa kujiamini ili kupata vitu sawa sawa na mapenzi Yake.

Unapoendelea mbele katika safari yako, utajaribiwa kuona kama utafanya mambo yote yale ambayo Bwana Mungu wako atakuamuru (ona Ibrahimu 3:25). Hii ni sehemu ya uzoefu wetu katika maisha ya duniani. Itakuhitaji kwamba usonge mbele ukiwa na imani imara katika Kristo, ukiongozwa na Roho na kuamini kwamba Mungu atakidhi mahitaji yako.

Kumbuka kwamba hupaswi kutetereka katika imani yako—hata katika nyakati za ugumu mkubwa. Unapokuwa imara, Bwana ataongeza uwezo wako wa kuinuka kuwa juu ya changamoto za maisha. Utawezeshwa kushinda misukumo hasi, na utakuza uwezo wa kushinda hata kile kinachoonekana kuwa kikwazo kikubwa.

Utakatifu.

Picha
young adults walking toward the Provo City Center Temple

Utakatifu, ni njia nyingine ya kuelekea kwenye furaha, inahusiana na ukamilifu kiroho na kimaadili. Utakatifu huonyesha usafi wa moyo na nia. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi kila siku kujilisha kiroho ili kwamba tuweze kukuza sifa hiyo ya kiungu?

Rais Harold B. Lee (1899–1973) alijibu: “Tunakuza utu wetu wa kiroho kwa kufanya mazoezi. … Lazima tuwe na mazoezi ya kila siku kwa roho zetu kwa kuomba, kwa kufanya matendo mema ya kila siku, kwa kushiriki na wengine. Lazima tuzilishe roho zetu kila siku kwa kujifunza maandiko kila siku, kwa [jioni ya familia nyumbani], kwa kuhudhuria mikutano, kwa kupokea sakramenti. …

“Mtu mwenye haki hujitahidi kujiendeleza vizuri mwenyewe akijua kwamba anahitajika kutubu kila siku.”7

Elementi nyingine ya muhimu ya utakatifu inahusiana na kufanya na kutunza maagano ya hekaluni. Kama tukiwa waaminifu, maagano haya yanatuinua sisi zaidi ya mipaka ya uwezo wetu na mtazamo wetu wenyewe. Baraka zote zilizoahidiwa za injili ya Yesu Kristo zinaweza kuwa za kwetu kupitia utiifu wetu kwa ibada na maagano tunayofanya mbele ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ndani ya hekalu. Sehemu ya mpangilio wa kuishi “kwa furaha” hujumuisha kujenga hekalu ambamo tunaabudu na kufanya maagano na Bwana (ona 2 Nefi 5:16, 27).

Jambo muhimu la njia hii ni kwamba tunapaswa kuwa waangalifu sana ili kukua kiroho na kuwa wasafi kimaadili.

Utiifu

Kutii amri za Mungu kunahusiana na njia nyingine za kuelekea kwenye furaha. Baada ya Wanefi kuwa wamejitenga kutoka kwa Walamani, walifanikiwa kwa wingi walipotii hukumu, maagizo, na amri “za Bwana katika vitu vyote, kulingana na sheria ya Musa” (2 Nefi 5:10). Mpangilio huu ni kipengele kingine muhimu cha kuishi “kwa furaha.”

Rais Monson amefundisha: “Tunapotii amri, maisha yetu yatakuwa na furaha tele, makamilifu zaidi, na sio ya kutatanisha sana. Changamoto na shida zetu zitakuwa rahisi kuvumilia, na tutapokea baraka za [Mungu] alizoahidi.”8 Alisema pia, “Elimu ambayo sisi tunatafuta, majibu ambayo sisi tunatafuta, na nguvu ambazo tunatamani leo ili kukabiliana na changamoto za ulimwengu changamani na unaobadilika zinaweza kuwa zetu tunapokuwa radhi kutii amri za Bwana.”9

Mwokozi anatusihi:

“Mkinipenda, mtazishika amri zangu. …

“Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye: naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda, na kujidhirihisha kwake” (Yohana 14:15, 21).

Kuwajali wengine na Upendo

Njia ya dhahabu kuelekea kwenye furaha ni moja ya kuwajali wengine na upendo—upendo ambao unajali, una shauku, na kipimo fulani cha hisani kwa kila nafsi inayoishi. Upendo ni njia ya moja kwa moja kuelekea kwenye furaha ambayo itarutubisha na kubariki maisha yetu na maisha ya wengine. Inamaanisha, kama Mwokozi alivyosema, kwamba muwapende hata adui zenu (ona Mathayo 5:44).

Kwa kufanya hivyo, utakuwa unatimiza amri kuu ya kumpenda Mungu. Utaruka juu ya upepo mbaya unaovuma—juu ya kuwa duni, kujishinda- mwenyewe, na ule uchungu. Furaha ya kweli na ya kudumu huja tu tunapochagua ku “mpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote” (Mathayo 22:37; ona pia Kumbukumbu la Torati 6:5; Marko 12:30; Luka 10:27).

Hebu kila mmoja achague kumpenda Bwana na kufuata njia Zake za kuelekea kwenye furaha, ambayo ni “dhumuni na sababu ya kuwepo kwetu.”10

Muhtasari

  1. “Furaha,” Mada za Injili, topics.lds.org.

  2. David O. McKay, katika Ripoti ya Mkutano, Okt. 1919, 180.

  3. “Furaha,” Saikolojia Leo, psychologytoday.com/basics/happiness.

  4. “Furaha,” Saikolojia Leo

  5. Thomas S. Monson, “Mifano ya Haki,” Liahona, Mei 2008, 65.

  6. Richard G. Scott, “Kufanya Maamuzi Sahihi,” Ensign, May 1991, 34.

  7. Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Harold B. Lee (2000), 176, 178.

  8. “Zishike Amri,” Liahona Nov. 2015, 83.

  9. Thomas S. Monson, “Utii Huleta Baraka,” Liahona, May 2013, 92.

  10. Joseph Smith, katika Historia ya Kanisa, 5:134.