2018
Ishara 6 za Pasaka ya Wayahudi Zinazoweza Kubadilisha Jinsi Unavyoiona Pasaka
April 2018


Ishara 6 za Pasaka ya Wayahudi Zinazoweza Kubadilisha Jinsi Unavyoiona Pasaka

Tunapokumbuka ishara za Pasaka ya Wayahudi, uelewa na furaha yetu juu ya uhakika wa Ufufuko utaongezeka.

Picha
table set with passover meal

Ninaipenda Pasaka, sikukuu ambayo inaadhimishwa kumkumbuka Yesu Kristo aliyewaweka huru watoto wa Mungu kutokana na utumwa wa mauti na jehanamu.

Lakini miaka 1,500 kabla ya Ufufuko, siku takatifu kama hiyo ilikuwa ikiadhimishwa kumkumbuka Yehova aliyewaweka huru wana wa Israeli kutoka katika utumwa wao huko Misri.

Pasaka hukumbuka dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi; Pasaka ya Wayahudi ilikuwa ni kivuli chake. Kwa pamoja, zinaweza kukuza uelewa wetu juu ya Ufufuko. Yafuatayo ni baadhi tu ya mahusiano kati ya Pasaka ya Wayahudi na Pasaka:

Pasaka ya Wayahudi

Pasaka

1. Pasaka ya Wayahudi ilijikita katika kondoo wa pasaka, wa kiume asiye na hila (ona Kutoka12:5), asiyevunjwa mifupa (ona Kutoka 12:46).

1. Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu (ona Yohana 1:29), asiye na dhambi na asiye na mfupa uliovunjwa (ona Yohana 19:36).

2. Mkate usiotiwa chachu, usiokuwa na uharibifu (ona Kamusi ya Biblia, “Chachu”), uliambatana na sherehe ya Pasaka ya Wayahudi (ona Kutoka 12:8, 15).

2. Yesu ni Mkate wa Uzima, ambao ndani yake hakuna uchafu (ona Yohana 6:35).

3. Mboga chungu, ishara ya utumwa wa Waisraeli, ziliambatana na sherehe ya Pasaka ya Wayahudi (ona Kutoka 12:8).

3. Yawezekana tukawa chini ya utumwa wa dhambi, lakini kwa sababu Yesu alikunywa kikombe kichungu (ona M&M 19:18), tunaweza kushinda kupitia Upatanisho Wake (ona 1 Wakorintho 15:22).

4. Karamu ya Pasaka ya Wayahudi ilitakiwa kuliwa kwa haraka (ona Kutoka 12:11).

4. Mwili wa Mwokozi ulitayarishwa kwa haraka kwa ajili ya mazishi (ona Yohana 19:31).

5. Waaminio waliopaka damu ya kondoo juu ya viunzi vya milango yao waliokolewa kutokana na kifo cha kimwili (ona Kutoka 12:7, 13).

5. Waaminio ambao kiishara hunywa damu ya Mwana Kondoo kila wiki wakati wa sakramenti na “daima kumkumbuka” (M&M 20:77, 79) wanaweza kuokolewa kutokana na kifo cha kiroho na cha kimwili (ona Mosia 4:2).

6. Siku baada ya mzaliwa wa kwanza kuuawa, uhuru ulitangazwa kwa mateka wa Kiisraeli (ona Kutoka 12:29–32).

6. Siku baada ya mzaliwa wa kwanza kuuawa, Yesu alitangaza uhuru kwa wale mateka katika Ulimwengu wa Roho (ona M&M 138:18, 31, 42).