2018
Vikapu na Chupa
April 2018


Kwenye Mimbari

Vikapu na Chupa

Picha
Sister Okazaki

Picha ya Dada Okazaki heshima ya Maktaba ya Historia ya Kanisa; picha zingine kutoka Getty Images

Picha
baskets and bottles of fruit

Mungu ametupatia zawadi nyingi, utofauti mkubwa, na tofauti nyingi, lakini jambo la muhimu ni kile tunachojua kuhusu kila mmoja—kwamba sote tu watoto Wake.

Changamoto yetu kama waumini wa Kanisa ni kwetu sote kujifunza kutoka kwa kila mmoja, ili kwamba sote tupendane kila mmoja na kukua pamoja.

Mafundisho ya injili ni ya msingi. Ni ya muhimu, lakini kirobota ni hiyari. Ngoja nieleze mfano rahisi ili kuonyesha tofauti kati ya mafundisho ya kanisa na kirobota cha utamaduni. Hapa kuna chupa ya pichi za Utah, iliyotengenezwa na mama nyumbani wa Utah ili kuilisha familia yake wakati wa majira ya theluji. Akina mama nyumbani wa Hawaii hawahifadhi matunda kwenye chupa. Wanaangua matunda ya kutosha kwa siku chache na kuyatunza ndani ya vikapu kama hiki kwa ajili ya familia zao. Kikapu hiki kina embe, ndizi, nanasi, na mapapai … yaliyoanguliwa na mama nyumbani wa Kipolinesia ili kulisha familia yake wakati hali ya hewa ambapo tunda huiva kipindi chote cha mwaka.

Kikapu na chupa ni vyombo tofauti, lakini vilivyomo vinafanana: tunda kwa ajili ya familia. Je, chupa ni sahihi na kikapu si sahihi? La, vyote viwili ni sahihi. Vyote ni vyombo sahihi kwa utamaduni na mahitaji ya watu hao. Na vyote ni sahihi kwa vile vilivyomo ndani yake, ambavyo ni matunda.

Sasa, tunda ni nini? Paulo anatuambia: “Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, [na] upole kiasi” [Wagalatia 5:22–23]. Katika udada wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, katika undugu wa akidi za ukuhani, katika unyenyekevu wa kuja pamoja kupokea sakramenti, tunda la Roho hutuunganisha katika upendo, shangwe, na amani bila kujali Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama huko Taipei au Tonga, bila kujali akidi ya ukuhani iko Montana au Mexico, na bila kujali mkutano wa sakramenti uko Fiji au Ufilipinio.

… Nilipoitwa kwenye Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, Rais [Gordon B.] Hinckley alinishauri: “unaleta sifa ya kipekee katika urais huu. Utatambulika kama mtu anayewawakilisha wale walio nje ya mipaka ya Marekani na Kanada. … Wataona ndani yako uwakilishi wa umoja wao na Kanisa.” Alinipa baraka kwamba ulimi wangu ungelegezwa nitakapoongea na watu.4

… [Nilipoongea katika nchi zingine,] niliweza kuhisi Roho akipeleka maneno yangu kwenye mioyo yao, na niliweza kuhisi “tunda la Roho” likinirudishia upendo wao, shangwe yao, na imani yao. Niliweza kuhisi Roho akituunganisha.

Wakina kaka na wakina dada, iwe matunda yako ni mapichi au mapapai, na iwe unayaleta ndani ya chupa au kikapu, tunakushukuruni kwa kuyatoa kwa upendo. Baba wa Mbinguni, na tuwe kitu kimoja na tuwe wako,5 Ninaomba katika jina takatifu la Mwokozi wetu, Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Chieko N. Okazaki, Angaza! (1993), 7.

  2. Ona Okazaki, Angaza!, 48–50; Gregory A. Prince, “‘Daima Kuna Pambano’: Usahili na Chieko N. Okazaki,” Mazungumzo: Shajara ya Wazo la Kimormoni 45, no. 1 (Kuchipua 2012): 114–115.

  3. “Tanzia: Okazaki, Chieko,” Deseret News, Agosti. 7, 2011.

  4. Ona Prince, “Daima kuna Pambano,” 121 Gordon B. Hinckley alikuwa Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza wakati Dada Okazaki alipoitwa mnamo 1990.

  5. Ona Mafundisho na Maagano 38:27.