2018
Thubutu Kuwa Mkarimu!
April 2018


Angaza Nuru Yako

Thubutu Kuwa Mkarimu!

Picha
dare to be kind

Halo! Mimi ni Claudia na Ninaishi Australia. Ninaangaza nuru yangu kwa kuwa mkarimu kwa wengine.

Ninasimama imara kwa ajili ya Wengine

Mvulana katika darasa langu shuleni anapata wakati mgumu kujifunza. Najitokeza kwa ajili yake wakati watu wanapomchokoza, na ninamsaidia darasani wakati anapohitaji msaada. Mwalimu wangu alisema huu ni mwaka pekee mvulana huyu anajiona kuwa naye ni sehemu ya darasa lake.

Mwanasesere Dubu Mdogo

Wakati mjomba wa mwalimu wangu alipofariki, alikuwa na huzuni sana. Hajui kuhusu Kanisa, kwa hivyo Nilimwambia kuwa Baba wa Mbinguni anampenda. Nilimtengenezea kadi na kumwambia kwamba atamuona mjomba wake tena. Nilimpa mwansesere dubu wangu mdogo maalumu ili kumsaidia katika nyakati za huzuni.

Marafiki wenye Bahati

Jirani yangu Olivia anapata taabu ya kutembea,kuongea, na kusikia. Mama yake Olivia husema kwamba Olivia ana bahati kuwa na rafiki kama mimi. Mimi nina bahati pia!

Kuimba na Roho Mtakatifu

Ninapenda kuimba nyimbo kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto. Familia yangu husema huwasaidia wao kuhisi Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hunipa hisia nzuri za ndani.