2018
Kupotea na Kupatikana
April 2018


Kupotea na Kupatikana

Picha
lost and found

Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni hujibu maombi. Wakati familia yangu ikiishi Ujerumani, tulienda Volksmak kijijini kwetu. Volksmak ni mahali ambapo marafiki na majirani hufurahia pamoja kwa kufanya matembezi ya kuona mazingira ya asili kwa pamoja. Wazazi wangu walisema kwamba ningeweza kutembea mbele ya kundi nikiwa na mmoja wa rafiki zangu, na tukaanza msafara huo mrefu.

Baada ya dakika chache sikuweza kumuona mtu yeyote wa familia yangu. Nilimwambia rafiki yangu kwamba ningebaki nyuma kuwasubiri. Punde sikuweza kabisa kumuona rafiki yangu au familia yake, na wazazi wangu bado hawakufika. Nilikuwa peke yangu pale msituni, na nilihisi uoga. Niliamua kuomba kwamba mtu angeniona.

Upande mwingine wa msitu, baba yangu alimsikia Roho Mtakatifu akimuambia, “nenda kamtafute mwanao.” Alihisi jinsi gani nilimhitaji, kwa hivyo aligeuka mara moja na kumwambia mama yangu kwamba alikuwa anaenda kunitafuta. Dakika chache baadaye baba yangu alikuja akikimbia kwenye njia ile ambayo mimi nilikuwa nikisubiri na akaniona. Nilikuwa na furaha kumuona baba yangu! Aliponiambia kuhusu kuwa na hisia kali ya kwamba mimi nilihitaji msaada, nilijua kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa amejibu maombi yangu.

Nina furaha kujua kwamba popote niwapo, ninaweza kuongea na Baba wa Mbinguni. Atanisaidia kuiona njia yangu.